Episode 2.
Ulikuwa ni muendelezo wa Nandipha na Thabo Bester kuendelea kufahamiana.
Kila mmoja alikuwa na namba ya mwenzie ivyo waliendelea kuwasiliana, lakini kikapita kipindi wakapotezana.
Nandipha alikomaa na chuo,
Huku mtaani Bester akiendelea kuwaibia watu kwa njia mbalimbali za udanganyifu,
alikuwa akitumia majina mengi kama, Thabo Bester, Thabo Magagulu, Kelly Johnson, Rufus Mahopo, Tom kelly, Thomas Bester, Thomas Better, TK, Thomas Kelly Young, Kelly Young na Thomas Magagulu. Yote hayo ni majina yake.
Mwaka 2012 Thabo Bester alikutana na mwanamke alipokwenda kununua gari kwenye kampuni ya BMW,
mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina la Nomfundo Thyulu alikuwa akifanya kazi hapo na alikuwa mwanamitindo pia.
Bester alizungumza kwa Lugha ya kutongoza, NAMFUNDO akajaa, penzi likazaliwa.
NAMFUNDO alimpenda BESTER na zaidi BESTER alikuwa ni mzungumzaji mzuri mwenye maneno ya kulaghai hasa linapokuja swala la kitu anachokitaka.
Ndipo weekend moja walipo kubaliana kuonana,
Bester alikwenda Cape Town, akalipia hotel na usiku ulipofika Bester aliamka akimuacha NAMFUNDO kitandani, alikwenda mpaka sebleni alichukua kisu kisha akarudi chumbani.
Hatua kadhaa kutoka alipolala NAMFUNDO, BESTER alinyanyua kisu chake lakini wakati huo NAMFUNDO alishituka usingizini na ndipo walipoanza kugombania kisu.
Ni kweliii
Mvutano uliendelea na kisha kisu kikatua kwenye kifua cha NAMFUNDO, damu nyingi zikaanza kumtoka.,
hapo ndipo Bester anapoamua kuchukua simu, pesa, na Laptop ya NAMFUNDO na kutoka nje ya hotel.
Kabla ya kufungua mlango mkubwa wa nje macho ya Bester yana gongana na mtu mmoja ambaye alikuwa ni msimamizi wa hotel hiyo.
Sasa tayari yalikuwa ni majira ya saa 10 alfajiri.
Ana mwambia ana hitaji usafiri ili aweze kuwahi anapokwenda.!!
Msimamizi wa hotel aliamua kumpatia Bester lift sababu yeye pia alikuwa anataka kwenda kununua baadhi ya mahitaji,
ambayo asubuhi hiyo yangetumika kuandalia breakfast ya hotelini hapo.
Wakiwa njiani Bester ali msisitiza msimamizi kwamba mchumba wake amemuacha chumbani amelala.
Hivyo aliomba asisumbuliwe mpaka yeye atakapo rudi hotelini hapo.
Yalipofika majira ya saa8 mchana msimamizi akapata wasiwasi baada ya kuona Bester hakurudi mpaka muda huo.
na ndipo msimamizi alipolazimisha chumba hicho kufunguliwa.
NAMFUNDO alikutwa akiwa amefariki na swala la kumpata Bester likabaki kitendawili.
Bester hakuishia hapo aliwatapeli tena wanawake wawili pesa nyingi na kisha akawabaka wote kwa mpigo,
na kutokomea zake kama afanyavyo siku zote.
Mara hii Askari waliifahamu sura ya Bester kupitia CCTV Camera ambazo kabla au baada ya tukio Camera ziliinasa Sura ya Bester.
Thabo Bester akakamatwa na kuhukumiwa kifungo jera, akiwa jera ndipo kesi ya Namfundo Thyulu ilipo ibuka.
"Umemuua mwanamke huyo kwa kumchoma kisu na kuiba mali zake"Hakimu alisema Huku akisoma makosa mengine ambayo yange mfunga Thabo Bester miaka 50 jera.
Bester alisimama na kujitetea.Akisema...
"Nimekuwa mtu ninayekosa haki tokea udogoni mwangu, Kwanza mama akatoroka na kuniacha na bibi, bibi naye alikuwa ni mraibu wa pombe.
Marafiki zake walio onyesha kunisaidia walinifungia ndani week nzima na kunibaka, nilipo mwambia bibi hakutaka kusikia habari hizo.
Thabo Bester alisema.Na aliendelea kusema
Nimezaliwa South Africa ni nyumbani lakini hapo nyumbani Hakuna mtu anayenipenda,
utotoni nimekuwa nikiitwa chokolaa, nililichukia sana hilo jina nilifanya kila nililoweza ili kuukwepa umaskini.
Bester ambaye siku hii aliongea mbele ya pirato kwa huzuni kubwa, alisema maisha yake yametawaliwa na maumivu makubwa na sio Furaha,
Aliongeza kwamba aliendelea tena kubakwa mara kadhaa na Jamaa wakaribu na bibi yake mpaka ikabidi aende kwa Daktari na kufanyiwa oparesheni sehemu ya haja kubwa.
Alipachukia nyumbani na hiyo ndio ikawa sababu ya kuwa kijana wa mtaani.
Bester ali endelea kusema tena
"Nilihama nyumbani na kwenda mtaani niliona huko ni sehemu sahihi, nilijitafutia Chakula huko na marafiki ambao walikuwa ndio Ndugu niliowatazama.
Na ndipo nilipoanza kuonyeshwa njia ya kutengeneza pesa kwa kutumia cheki fake,
Bester ali endelea kusema kuwa ali fanya yote haya sababu ya hali ngumu ya maisha.
Bester hakuishia hapo aliendelea kujitetea juu ya kuhusiswa na kumua NAMFUNDO, alisema yeye na NAMFUNDO ni watu waliopendana asingeweza kumuua mpenzi wake,
siku hiyo walikuwa na ugomvi wa kimapenzi juu ya NAMFUNDO kumuona yeye na mwanamke mwingine.
ugomvi wa wivu ni jambo linalotokea kwenye mapenzi, nikawaida siku lichukulia kama tukio kubwa".
Bester alisema..Aliongeza kwamba..Wakiwa hotelini mida ya usiku alikwenda sebleni na kuchukua kisu Kwaajili ya kumenya tunda lililo karibu na kitanda chao.
na ndipo NAMFUNDO alipomuona ameshika kisu !!.
Pengine baada ya ugomvi alihisi mimi nataka kumpiga, nisingeweza kufanya ivyo huku nimeshika kisu ikiwa najua madhara ya kisu".
Bester alijitetea kwamba ilitokea kama ajali tu, baada ya mvutano kisu kikatua kwenye kifua cha NAMFUNDO.
kwa hofu akaondoka na kumuacha mpenzi wake akiwa na jeraha la kisu ambalo lilisababisha kifo chake.
Licha ya Bester kujitetea hakimu hakutaka kuelewa chochote, akampiga mvua ya miaka 50 jera.
You are very cruel"Hakimu alisema huku akijitayarisha kwa kushika nyundo na kusoma hukumu hiyo.
Thabo Bester alikwenda gerezani na kukitumikia kifungo hicho kwenye gereza la Mangaung, gereza ambalo lipo chini ya ulinzi mkali, likilindwa na kampuni ya kimataifa G4s.Story za Bester zikaishia hapo.
Salute to wisdom,
I will be back. I mean no one to nobody.