Mapenzi yanapo waunganisha watu wawili na kupelekea mushkeri katika jamii

Mapenzi yanapo waunganisha watu wawili na kupelekea mushkeri katika jamii

Episode 3.

Maisha yaliendelea wakati huo Nandipha alihitimu elimu yake ya chuo Kikuu katika chuo cha Wits.

Nandipha alipata shahada ya Sayansi ya Afya katika Sayansi ya Tiba, Shahada ya Tiba na Shahada ya Upasuaji.Lakini pia ilipofika 2014 Nandipha aliolewa na Daktari mwenzie aliyefahamika kwa jina la Dr Mkhuseli Magudumana.
FwkaPtcWYAAznS-.jpeg


Unadhani movie ya Thabo Bester na Dr.Nandipa imeishia hapa.? .

Thabo Bester akiwa gerezani, maisha ya uko yaliendelea kama yuko uraiani.

Alianzisha genge lingine la utapeli lililokuwa linamuingizia pesa kila kukicha, ndani ya gereza hilo aliweza kutumia Smartphone na Laptop kwa namna aliyoijua yeye.

kusomea tasnia ya habari na mitindo na usimamizi wa makampuni makubwa.

Akaandaa wasifu wake na mara hii alijiita Tom kelly Motsepe, katika wasifu huo alijitambulisha kama mwenyekiti na mtendaji mkuu wa kampuni ya 21st Century Media, kampuni ambayo aliifanya ionekane kama tawi teuzi la kampuni halisi ambayo ni 21st Century Fox.

Wasifu ulizidi kuonyesha kwamba mwenyekiti huyo ambaye ni Tom Motsepe alikuwa akiishi marekani.

Wasifu ulionyesha kama mshauri wa uwekezaji wa South Africa, mfanya biashara mbunifu na kiongozi makini mwenye ujuzi thabiti wa kuendesha chapa ya kimataifa.

Ana shahada ya uzamili katika utawala wa biashara na usimamizi kutoka chuo Kikuu cha Cap Town, na shahada ya uzamili katika uwekezaji na zamana kutoka chuo Kikuu cha harvard chuo kilichopo marekani katika mji wa Massachusetts.

Thabo Bester ambaye katika wasifu huo alikuwa kama Tom K Motsepe aliufanya wasifu wake uonyeshe kampuni kadhaa zilizo anzishwa na yeye.

Ilionyesha kuwa alianzisha kampuni yenye jina kubwa akiwa kijana Mdogo wa miaka21.
Pia yeye ni mtaalam katika uchimbaji wa madini uwekezaji na vyombo vya habari.

Alianza kwa kuposti mitandaoni kwa kufungua Website, account za social media zote zikiwa na jina la Tom Motsepe.
Aliposti Picha tofauti katika mtandao wa Twitter, Picha ambazo zilieditiwa kwa kubandikwa sura kwenye miili ya watu wengine.
Picha moja ilionekana Location na vazi alilolivaa katika Picha hiyo ndio hilohilo alilolivaa msanii Michael B Jordan wa marekani.

Najua unajiuliza Vipi kuhusu Dr Nandipha.Jibu ili hapa..

Nandipha akiwa kama Mke, sasa alifanya kazi katika Hospitali ya Edenvale na baadae akafanya kazi katika Hospitali ya Far East Rand.Akafanikiwa kupata Watoto wawili ambao ni Aziza na Ayana.
Dr nandipha jina lake lilikua kwa kasi sana na akawa mwanamke mwenye mafanikio makubwa hapo South Africa.

Alifahamika na kupendwa na kila mtu, hata ikafikia wakati alipata mualiko kwenye siku ya kuzaliwa ya aliyekuwa rais wa pili wa South Africa ambaye ni Thabo Mbeki..

Dr.Nandipha akawa mwanamke wa hadhi ya juu, alikuwa ni mtu wa vacation,
alipenda kwenda kula maisha nje ya nchi .

Alikuwa na Jumba la kifahari lenye thamani ya Rand milioni12 sawa na bilioni 1.5 kwa pesa za kitanzania.

Nandipha alifanikiwa kuona machapisho mbali mbali ya Tom Motsepe katika mitandao na hapo ndipo alipoamua kumtafuta.
Perhaps!!.

Dr Nandipha.Alifahamu wazi kuwa mtu anayejiita Tom Motsepe ndiye Thabo Bester.
"Hili nimejaribu kuliwaza mimi"Anyway mawasiliano ya Nandipha na Thabo Bester yalirudi tena.Nandipha alifungua clinical yake na kuipa jina la Optimum Medical.

Bester akiwa gerezani aliweza kuitangaza vyema kampuni yake mtandaoni.

Ilikuwa maarufu tayari
Mwaka 2018 uzinduzi wa kampuni ya 21st Century Media ulifanyika kwa kiingilio kinono na watu wengi walihudhuria uzinduzi huo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na wanawake wenye hadhi ya juu hapo Johannesburg,
lakini pia na watu mashuhuri ambao ni Amanda Du Pont na Yvonne Chaka Chaka.

Uongozi ulisema mwenyekiti wa kampuni hiyo alikuwa marekani ivyo wakati wa uzinduzi wangezungumza naye kupitia simu kwa screen iliyopo ukumbini hapo.

Nikweli kiongozi huyo alipigiwa simu wakati wa ufunguzi huo,
ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa ivyo walimwimbia Happy Birthday kwa mtindo wa kumsurprise huku wakimtaka asilie kwa surprise hiyo.

Hawa kujua!!
.
Tarehe ya mkutano huo ilikuwa ni June 13 mwaka 2018 na Thabo Bester tarehe yake ya kuzaliwa ni June 13. There's a lot of fraud.Mtu huyo aliyeonekana kwenye screen kubwa kama Tom Motsepe ndio Thabo Bester aliyekuwa gerezani.


Huu ni utapeli wa next level, Baada ya hafla hiyo kuisha.
.
Mwaka huohuo 2018 kampuni hiyo ilitangaza mkutano ulio julikana kama " Woman in Media"Wageni rasmi wakiwa ni watu maarufu kutoka marekaniAmbao ni Taraji P Henson na Halle Berry huku Bonang Matheba kutokea South Africa akitajwa kuwa mshehereshaji.

Katika mkutano huu teketi ziliuzwa kwa kila mtu mmoja kwa Rand 1250 sawa na laki moja na20 kwa pesa za kitanzania.

Huu ulikuwa ni mpango mwingine wa Thabo Bester kujizolea mamilioni ya pesa.
Ila mpango huu ulishindikana baada ya Taraji P Henson na Halle Berry kukanusha kwamba hawahusiki na mkutano huo.
Bonang Matheba ambaye ni mtu maarufu hapo SA naye pia aliamua kujitoa baada ya kuona ukanusho wa Taraji na Halle Berry kwamba hawatokuwepo katika mkutano huo.

Kitumbua kikaingia mchanga..
Na huo ndio ukawa Mwanzo wa kampuni hiyo kupoteza uhaminifu kwa watu.

Sasa Binafsi nikajiuliza mtu aliyemsaidia Thabo Bester kufungua kampuni ni nani?

Niliamini Thabo Bester asingeweza kufanya yote hayo akiwa mwenyewe!

lazima kungekuwa na mtu ambaye kazi yake ilikuwa ni kuwaaminisha watu juu ya kampuni.

Ni kweli nilipo kuja kubaini,
Mwanamke huyu alikuwa ni mkurugenzi wa kampuni hiyo ya 21st Century Media,

ali fahamika kwa maijina ya phumudzo thenga.

Kazi yake kubwa ilikuwa ni kuzungumza na watu uso kwa uso walipotaka kuonana na ungozi wa kampuni hiyo,

Watu walipotaka kupata maelezo machache kutoka kwa bos, hapo Phumudzo Thenga alipiga simu kwa Thabo Bester ambaye yuko gerezani.

Thabo Bester alizungumza kama Tom Motsepe alisema yako marekani na ndiko anakoishi.

Watu walio taka kujiunga na kampuni hiyo waliaminishwa na kuamini

Thabo Bester huko Gerezani alikuwa na chumba kizuri kilichopakwa rangi nyeupe, wakati mwingine alikibadilisha kwa kuweka tambala jeupe nyuma.
Chumba hicho alikitumia kupiga Picha na kuzungumza na watu.

Sasa swala la kampuni kuonekana kuwa na udanganyifu, baada ya Taraji P Henson na Halle Berry kukanusha hawahusiki na hilo,

Bester aliamua kuachana na mpango huo na kuendelea na mipango mingine.
Ndipo Dr Nandipha aliibuka na kumfikia Bester aliyekuwa gerezani na kuanza kutembelea.

Mwaka 2019 mipango ya kumtoa Bester Gerezani ilianza kusukwa chini ya usimamizi wa Bester mwenyewe.

"You can get out of poverty if you'll help me"Bester alisema kwa askari mmoja akijaribu kumshawishi awe sehemu ya mpango wake wa kutoroka.
FwkQoxlWIAAgJ0n.jpeg
FwklRxNWcAEa-JJ.jpeg


I Wii be back, I mean no Malice to nobody.

Salute to wisdom.
 
Back
Top Bottom