Pole sana Mkuu kwa lilokukuta.
Naelewa ni ngumu kudeal na hali jii ikiwa imetokea in real life tofauti na ukisimuliwa.
My view:
Kwa hali ilivyo sasa Binti amekuwa bidhaa adimu inayotafutwa sana, kama ilivyo ada bidhaa adimu huuzwa ghali. Yaani wewe na mume mwenzio nyote mnamtaka binti, binti yuko safe ila ninyi hamna uhakika na hatma ya hisia zenu. Cha kufanya ni kubadili mchezo au kupindua meza.
- Binti kawa muwazi kuwa mko wawili na anawapenda wote (inawezekana,huenda wote mnamhudumia vyema maana binadamu n wabinafsi sana).
- Binti ni muoga kufanya maamuzi maana vitu unavyompa ni karibia sawa na anavyopewa na jamaa wa kwao (ana hofu ya kupoteza kimojawapo hivyo anakuwa kama fisi, anataka vyote).
Ushauri wangu:
Warning: kufuata ushauri huu inabidi uwe una uwezo wa kudhibiti hisia zako (self constrain).
Bila kupepesa macho Binafsi naamini anaeua kwa Upanga basi hufa kwa Upanga!
- Binti ameua kwa Upanga, nakushauri Usilalamike tena kwake kama mmeongea inatosha
Cha kufanya ili muelewane vyema fanya alichokifanya yeye exactly kilekile usizidishe.
Tafuta pisi nyingine na hakikisha anajua akiuliza majibu yako yawe kama yake kuwa umewapenda wote na unashindwa kuchagua mmoja.
Hii itawasaidia wote,
Itamsaidia Binti kuelewa ur point of view, kuwa umejisikiaje, umeumiaje, na umefikiria vitu gani kwa alichokifanya
Pili, Itakusaidia wewe kuwa katika nafasi nzuri, sababu baada ya hili kuna uwezekano ukafanikiwa kumlazimisha binti (kifikra) kufanya maamuzi and mostly in ur favor sababu ndo upo karibu nae, akikukosa itamuuma zaidi kuliko yule aliembali na sababu ya ubinafsi wake atalazimika kukuchagua ili kutetea Maslahi yake ikiwa na pamoja na kutokukupoteza.
Pia ukifanya hivyo itakupa 'alternative' hutakuwa ukimtegemea binti pekee, utampatia msaidizi...hivyo wewe ndiye utakae kuwa ni golden card! na utamfanya yeye ndio asiwe na uhakika wa hatma ya hisia zake.
Mwisho wa yote maamuzi ya kuamua aidha binti atakuwa mama watoto wako au la itategemea na mwenendo wake baada ya hatua hizo, akitulia na kuegema kwako atakufaa, vinginevyo piga moyo konde kuna mwingine utampenda na atakupenda sana.
Goodluck!