Mapenzi yaninatesa, ninayempenda anawasiliana na mimi akitaka yeye

Mapenzi yaninatesa, ninayempenda anawasiliana na mimi akitaka yeye

Maji Chai

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2018
Posts
265
Reaction score
362
Habarini wakuu

Nampenda mtoto mmoja hivi, she's not so beautiful ila ndo hivyo moyo umependa jamani ila ananinyanyasa mno kwakweli.

Hajibu text zangu mpaka pale anapojisikia, nampigia hapokei yaani yeye ananitafuta akipenda yeye.

Amekuwa akifanya mengi ya ajabu ila nikihoji anakuja juu naishia kuomba msamaha mimi.

Jamani nateketea, sijui niliingiaje huku.

1620809683692.png

Lakini pia ni matamu sana ukibahatika kuyapata mapenzi ya kweli. Saa zote una tabasamu tu hata ukiwa usingizini tabasamu la nguvu. Au nasema uongo ndugu zangu? 😜😜
 
Pole sana mkuu hii situation nnayo ata mimi, ndo maana hadi mda huu nko macho.
Usingizi hauji ni stress tupu.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nkajua ni mimi tu hapa nshaomba msamaha kwa kosa ambalo hata sijui ni lipi sijasamehewa naambiwa ana mengi kichwani maisha haya jamani
Mkikuwa mtaacha huu ujinga. Yani unateseka kisa mwanamke? Unakosa usingizi kisa mwanamke?

Hapo mnalazimisha mapenzi nyie shtukeni hampendwi mna force watu ambao wana watu wao wanaowapenda.

Nyie endeleeni kushika mapembe wenzenu wanakamua. Wakati hajibu text zako na wewe unakesha kwa kukosa usingizi mwenzako yupo huko anazungusha mauno ya shetani wala hana habari na wewe.
 
Maneno makali haya sema kweli mtu anakata viuno mi naumia huku this is bullshit
 
Naam vinginevyo yanini kupoteza muda wako kwa asiyekupenda? Penzi halilazimishwi unaona anakuzingua piga kimya.
Mzee kila nkijaribu wapi, halafu ni kama ashajua kwamba nampenda ile kinoma yani ndo maana anafanya hivi,yani anajua kabisa anitafute asinitafute am very weak kwake lazima ntamsumbua wee ndo apokee niomgee naye,anajua kabisa siwezi lala bila kumwambia usiku mwema ila leo nakausha tuone,labda ntaanza kumsahau polepole.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nkajua ni mimi tu hapa nshaomba msamaha kwa kosa ambalo hata sijui ni lipi sijasamehewa naambiwa ana mengi kichwani maisha haya jamani
Mapenzi ndivyo yalivyo jombaa unayempenda hakupendi, Naye kuna mtu anampenda ambaye hampendi, na wewe kuna mtu anakupenda ila humpendi.

Kama unadhani ni rahisi kumpenda usiyempenda ungeanza wewe kumwelewa yule usiyemwelewa.
 
Back
Top Bottom