Mapenzi yawe ni ya muda maalumu tu ili kuepusha mateso ya kihisia ya muda mrefu

Mapenzi yawe ni ya muda maalumu tu ili kuepusha mateso ya kihisia ya muda mrefu

Kusema kirahisi tu kwamba ndoa za mababu zetu zilidumu bila ushahidi wowote unatupa wakati mgumu kukuamini . Huenda babu na bibi yako uliwaona wako pamoja uzeeni we ukaweka conclusion Kwamba ndoa za zamani zilidumu
Watu wanasahau kuwa uvumilivu wa Mwanamke wa zamani ni tofauti na waliopo zama hizi ambapo wengi wameshaaminishwa kuwa Mwanamke na Mwanaume ni sawa.

Hivyo Mwanamke wa zamani aliwazidi hawa wa leo kwa uvumilivu tu lakini Mwanaume ni yule yule.
 
Wasichotaka kujifunza wengi wetu ni kuwa Mwanamke wa zamani hakuwa anapewa hadhi sana na jamii...na tena huku kwetu (Africa) ndio tulichelewa sana kurekebesha hali na hata sasa bado kuna viashiria hivyo.

Mwanamke wa zama hizo hakuwa na maamuzi zaidi ya kumtegemea Mwanaume kwa karibu kila jambo...ndio maana zile hazikuwa haswa ndoa bali ilikuwa ni Mwanaume anateua tu Wanawake wa kuishi nao.

Ni ujio wa hizi dini kubwa mbili ndio ukawagawa Watu, Upande mmoja wakaaminishwa kuwa Mungu anataka kuishi na Mke mmoja tu na msiachane mpaka mmoja wenu aage dunia, na kundi lingine wakaaminishwa kuwa Mungu anaruhusu kuoa hata Wake wanne.

Hivyo tuangalie haswa wakati huu uliopo sasa ambapo Mwanamke anaamini kwamba nae amezitambua haki zake.

Ndio maana hoja yangu hapa ni kwa nini tuendelee kudanganyana kwa maneno matamu ambapo ni suala la muda tu kabla ya kila Mmoja kumuangalia Mwenza wake kama shetani?
 
Mkuu hii proposal yako inaweza ikaja kutumika miaka mia badae badaa ya mapenzi kukosa nguvu
Mkuu kwa heshima naomba utumie neno""kuisha nguvu kabisa""maana hapa tulipo yameshakosa tayari.
 
Siku zote mwanzo huwa mzuri na kila mmoja (haswa Mwanaume) huwa kipofu wa siku za mbele (future)...Mwanamke anapambwa kuliko kipande cha almasi.

"And I will keep you warm through the shadows of the night Let me touch you with my love I can make you feel so right And baby through the years Even when we're old and gray I will love you more each day 'Cause you will always be the lady in my life "
 
Yaani ujiandae mapemaa na deadline yako,

Sijui nani alitunga sheria ya umilele.
 
Back
Top Bottom