Wasichotaka kujifunza wengi wetu ni kuwa Mwanamke wa zamani hakuwa anapewa hadhi sana na jamii...na tena huku kwetu (Africa) ndio tulichelewa sana kurekebesha hali na hata sasa bado kuna viashiria hivyo.
Mwanamke wa zama hizo hakuwa na maamuzi zaidi ya kumtegemea Mwanaume kwa karibu kila jambo...ndio maana zile hazikuwa haswa ndoa bali ilikuwa ni Mwanaume anateua tu Wanawake wa kuishi nao.
Ni ujio wa hizi dini kubwa mbili ndio ukawagawa Watu, Upande mmoja wakaaminishwa kuwa Mungu anataka kuishi na Mke mmoja tu na msiachane mpaka mmoja wenu aage dunia, na kundi lingine wakaaminishwa kuwa Mungu anaruhusu kuoa hata Wake wanne.
Hivyo tuangalie haswa wakati huu uliopo sasa ambapo Mwanamke anaamini kwamba nae amezitambua haki zake.
Ndio maana hoja yangu hapa ni kwa nini tuendelee kudanganyana kwa maneno matamu ambapo ni suala la muda tu kabla ya kila Mmoja kumuangalia Mwenza wake kama shetani?