Midimay
JF-Expert Member
- Apr 12, 2015
- 3,036
- 5,039
Kuna hila mbaya sana zinaendelea dhidi ya Wafugaji wa Kimaasai yanayofanyika ndani ya Wizara ya MaliAsili na Utalii. Hila hizo zinafanyika kupitia taasisi za serikali iliyo chini ya wizara hiyo. Taasisi hiyo ni Wakala wa Misitu(TFS), Idara ya Wanayama pori na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Kabla hata Wamasai wa Ngorongoro hawajajua mustakabali wao, tayari Wizara hiyo kupitia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo, imetangaza kuchukua maeneo mengi ya wafugaji wa kimaasai kuwa mapori ya akiba.
Ni mwaka jana tu wizara hiyo hiyo pia kupitia hotuba ya Waziri ilitangaza maeneo mengine katika Wilaya za Monduli na Longido kupandishwa hadhi kuwa maeneo ya akiba.
Maeneo yote hayo yanapandishwa hadhi katika Wilaya ambazo tayari zina maeneo kibao ya hifadhi.
Tuchukulie mfano wilaya ya Monduli ambayo ardhi yake imechukuliwa na hifadhi ya Taifa ya Lake Manyara, Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na pori kubwa kwa ajili ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Wilaya hiyo hiyo tena ndio kuna pori la Lolkisale, Mto wa Mbu, Esimingor, Eneo la Engaruka na Orduvai ambayo yote wizara inataka kuyapandisha hadhi kuwa maeneo ya kuyahifadhi.
Wizara inataka wananchi wa wilaya ya Monduli wafanye shughuli za kiuchumi katika ardhi ipi?
Wanataka waelee hewani?
Katika hotuba ya mwaka huu, maeneo yote yaliyoombwa kupitia idara ya Wanyama pori kwa asilimia 90 wanaishi Wamaasai.
Hii wizara ina ajenda gani mbaya na wamaasai?
Hayo mapepo yakemewe kwa nguvu zote.
Wamaasai ni binadamu kama binadamu wengine.
Wanahitaji ardhi kwa ajili ya shughuli zao za kiuchumi za kila siku.