kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Ukiangalia watu wanaliofanya na kushangilia mapinduzi kule Burkina Faso, Mali na Niger ni vijana ambao sanduku la kura limeshindwa kuwapatia viongozi wanaowachagua. Chaguzi zetu zinafadhiliwa na wakoloni wetu wa zamani kwa manufaa yao.
Chaguzi zetu ni mwanya wa kupenyeza mamluki kwenye uongozi wa juu wa taifa. Miaka 60 ya bara la Afrika kuwa huru hali ya maisha imesalia ileile bila sababu za msingi. Nadhani vijana wa Afrika wanataka kujaribu njia mpya katika kujitafutia nafuu badala ya ile ya kupanda boti na kwenda Ulaya kutafuta nafuu.
Vijana wanaofikiri kufuata njia ya mali Burkina Faso na Niger wako kila nchi barani Afrika, ni muda tu ndio unakuwa kikwazo kwao. Wamachinga, bodaboda na wakosa ajira ni makundi ya kuchungwa sana. Siku kama ikitokea yale maeneo ya wazi yamejaa, ardhi ya wazi imejaa na mishahara ya watumishi ikizidi kupungua uwezo wa kununua bidhaa siku hadi siku iko siku tunaweza kuona hali tofauti kabisa.