Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu
ZFF wamekuja na mfumo mpya wa Mapinduzi Cup!
Michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa 2025 itashirikisha timu za Taifa na sio vilabu kama ilivyozoeleka ambapo michuano hiyo itachezwa kwa mtindo wa makundi, nusu fainali na fainali itakayopigwa Januari 13, 2025 na mechi zote zitapigwa katika uwanja wa Gombani Pemba huku Bingwa akitarajiwa kutia kibindoni kitita cha Tsh. Milioni 100.
Hayo yameelezwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mapinduzi Cup 2025, Dkt. Suleiman Mahmoud Jabil na kubainisha kuwa timu zitakazoshiriki ni wenyeji Zanzibar Heroes na Kilimanjaro Stars, Kenya (Harambee Stars), Uganda (The Cranes), Burundi na Burkina Faso.