Nafikiri kuwa APR kwanza wamecheza mpira na ku-dominate mchezo kwa kiasi kikubwa. Wamekosa kosa magoli na pia tuseme ukweli, wanatakiwa wapewe maua yao.
Mimi sio mchambuzi ila kiukweli ambacho hakisemwi Sana na wachezaji wa zanzibar kuunawa mpira katika eneo la kipa mara 3 kwa mimi nilivyoona ila refa kapeta. Na chakushangaza ni kuwa hata huyu shiboud mchezaji wa APR alilalamika Sana maana ipo sehemu alibambikiwa yeye kuwa ndo kaanza kuunawa mpira badala ya mchezaji wa zanzibar.
Pia wachezaji 3 wa zanzibar walionyesha mchezo wa hovyo kwa kwenda kuwapiga wachezaji wa APR ila chakushangaza, only kadi nyekundu zikatoka kwa mchezaji mmoja tu wa zanzibar. Wengine hawakupewa kadi na niseme tu kuwa wachezaji wa APR si wagomvi, ingekuwa ni simba au yanga, nadhani uwanja ungegeuka kuwa wa vitasa.
Kuhusu magoli yaliyofungwa na APR, ningekuwa mimi ni refa ningekubali lile bao Maana wakati mshika kibendera ananyoosha juu, ni kweli kulikuwa na offside ya mchezaji wa APR ila aliefunga bao yeye ndo hakuwa offside Hivyo tofauti yake ndo hapo.
Ushauri
Ingekuwa vizuri Zaidi kama mashindano haya ya mwaka ujao, walau kuwe na waamuzi ambao si wa Tanzania au nchi yoyote mwanachama mualikwa katika kombe hilo inaweza kuwa ni Bora zaidi. Mfano Kuchukua waamuzi toka hapo Malawi, zambia, south africa au hata hapo sudan. Hii inaweza shawishi nchi nyingi kuleta wachezaji wao na kuomba kualikwa.
Udhamini
Bado kuna umimi Sana Katika hili kombe, inatakiwa kuangalia kwa mapana kuhusu kombe hili KWA:-
1: kuongeza udhamini na fedha
2: matangazo ya muda mrefu hata miezi miwili kabla. Hata Azam TV wanaweza
3: liwe kombe kama la kawaida na sio kuweka vigezo vingi vya uzanzibari Sana
4: kuomba wadhamini wajitokeze kwa wingi na kuweza kutangaziwa bidhaa zao bure kwenye sehemu ya matangazo ya uwanja.
5: kutangaza utalii kwa kupunguza gharama za utalii zanzibar na hata timu zote shiriki kuweza kutembelea sehemu mbali mbali za utalii na kutangazwa kwenye media mbali mbali.
6: kuruhusu mfumo huru wa mechi zote kusiwepo na masuala ya siasa siasa kama Sasa muda wote ni matangazo ya uwanja, mara rais na kuandaliwa na serikali