Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari

Tekinolojia ni nzuri sana isee uzuri YouTube ina video za mapinduzi hayo sehemu mbalimbali hapo unguja kuanzia mnazi mmoja, darajani, bububu na kwingineka unaweza kuona live kilichokuwa kinaendelea ni mauaji ya halaiki kwa waarabu hapo zanzibar kwa askari waliopindua walikuwa wanvuta bangi, na wengine walivaa gauni na mashera imagine ni wazi ni kama gang alafu waarabu waliuliwa kwa makundi na kutupwa kwenye visima na wengine walibakwa wengine walikimbia na majaazi na wengi waliuliwa pwani walipokuwa wanakimbia kunusuru maisha yao.

Kiukweli zanzibar ipo salama sababu ya muungano na si kitu kingine karume alitumia akili sana kumuomba nyerere waunganishe nchi sababu alijua kabisa usalama wake ulikuwa mashakani pamoja na hivyo bado walimpata na kumuuwa..
duh !。
p
 
Mkuu Kishinajari, Kishnajr anayazungumzia Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni Mzee Sukari, mimi hapa ni reporter tuu nikiripoti kilichosemwa na nilichokisikia, na links nimekuwekea ili na wewe usikilize mwenyewe, sasa muongo ni nani kati ya mimi niliyeripoti nilichosikia na aliyesema?. Tuheshimiane, kuitana waongo hakusaidii, kama unaujua ukweli useme!。
p
Aliyeuona uongo akausadiki ilihali anajua kbs kuwa ni uongo,na yeye ni muongo pia.
Hvi na wewe ni muongo km hujijuw
 
Aliyeuona uongo akausadiki ilihali anajua kbs kuwa ni uongo,na yeye ni muongo pia.
Hvi na wewe ni muongo km hujijuw
ili jambo liwe uongo ni lazima ukweli ujulikane, ukiambiwa kitu na shuhuda aliyeshuhudia utaamini ni ukweli unless aje shuhuda mwingine kukanusha kuwa huo ni ushuhuda wa uongo,ukisema jambo fulani ni uongo, unausema ukweli kukanusha huo uongo!。 Ukweli ni upi?。
P
 
Nimekuwekea na link hii uangalie live waarabu walivyokuwa wanafanywa na kukimbia ovyo kujinusuru..

View: https://youtu.be/Ss-lfLLzV-k?si=h_65vXtkETR6Zk7s

some of these videos sio za kweli kwasababu shooting color film ilikuwa ikifanywa 16mm real, na was very expensive, hivyo the authenticity of hizo videos ni doubtiful na sijui kwanini mpaka leo mashuhuda wa Mapinduzi hayo Matukufu ya Zanzibar hawausemi ukweli wa ni nini haswa kilichojiri。 Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1
P
 
some of these videos sio za kweli kwasababu shooting color film ilikuwa ikifanywa 16mm real, na was very expensive, hivyo the authenticity of hizo videos ni doubtiful na sijui kwanini mpaka leo mashuhuda wa Mapinduzi hayo Matukufu ya Zanzibar hawausemi ukweli wa ni nini haswa kilichojiri。 Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1
P
wakili msomi kwa karne hii na tekinolojia ilivyokuwa ni rahisi sana kuconvert colorless video za zamani kuziweka rangi ikaonekana kwenye uhalisia..
Hizo clip ni za zanzibar nimekaa huko nayajua hayo maeneo vyema na zipo clip nyingi tofauti tofauti.
 
Wanabodi,

Nafuatia makala maalum kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 1964, zinazorushwa mfululizo na Idhaa ya KIswahili ya BBC kila siku kuanzia 1:00-1:30.

Katika kipindi cha leo, Mmoja wa askari aliyekuwa zamu ikulu ya Sultani, kwa jina maarufu la Mzee Sukari, anasimulia first hand information kuhusu mapinduzi hayo! akihojiwa na Baruan Muhuza wa BBC. Amekiri kuwa Sultani hakufukuzwa Zanzibar, alikuwa akitafutwa hivyo alitoroka mwenyewe!, na baada ya Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar, waarabu hawakufukuzwa Zanzibar, bali walijiondokea wenyewe!

Huu ni ushuhuda uliotolewa na shuhuda halisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambae simulizi yake ni tofauti na urongo mwingi tuliolishwa na maandishi ya mahasidi wa Mapinduzi.

Kesho kutafanyika mjadala maalum kuhusu Mapinduzi hayo Matukufu ya Zanzibar utakaoanza saa 12:45-1:30.
Baada ya mapinduzi Zanzibar - BBC Swahili - BBC.com
Zanzibar na miaka 51 ya Mapinduzi - BBC Swahili


Siku ya kilele, kutatolewa nishani maalum za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, sijui kama yule shujaa halisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Field Marshal John Okello, atakumbukwa!

Paskali
Mwana JF, Paskali, anakutakia wewe na familia yako HERI YA SIKUKUU YA MAPINDUZI MATUKUFU
YA ZANZIBAR!
Paskali
 
Back
Top Bottom