mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,188
- 1,090
Mamlaka ya Mapato wamekuwa wakijitahidi sana kukusanya mapato (kodi) kwa kutumia mbinu mbalimbali ili kufikia malengo ya mwezi na mwaka. Mpanuko wa mahitaji ya fedha katika nchi umekuwa ukiongezeka kila leo na kila mwaka, hivyo mahitaji ya fedha yamekuwa makubwa hata kupelekea nchi kukopa zaidi. Dawa ya deni ni kulipa. Sasa nchi inalipaje? Kwa kukusanya mapato (kodi) na tozo.
Kwa mujibu wa idadi ya watu katika nchi, takwimu zinaonyesha kwamba wanaolipa kodi ni kundi dogo sana la wafanyabiashara wasiofika milioni 4 kati ya wananchi milioni 60. Hii ni janga na msingi wa umaskini mkubwa wa nchi. Lazima TRA iongeze wigo wa walipa kodi katika nchi. Bado wafanyabiashara wengi wenye vipato hawalipi kabisa kodi. Na ili hili lifanyike, kuna haja kubwa ya kufanyia mfumo na sheria za kodi marekebisho hapa nchini.
Kukamua wafanyabiashara wachache ni kuua uchumi. Wafanyabiashara wadogo na wa kati ndio nguzo ya uchumi wa mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea. Zipo taarifa za ukwepaji mkubwa wa kodi za forodha unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa wenye kukingwa na vivuli vya viongozi wakubwa. Hii ni kansa kubwa. Tunapoteza mabilioni ya fedha sababu ya upendeleo au uswahiba usio na uzalendo.
Misamaha ya kodi pia inapaswa kufanyiwa marekebisho. Kunapaswa kufanyika ukaguzi maalum kwa maslahi mapana ya Taifa kuhusu misamaha ya kodi. Nchi yetu ni maskini sana kuendelea kutoa misamaha ya kodi isiyo na tija katika kuondoa umaskini ama kuongeza mapato. Na katika hili, mamlaka ya Waziri wa Fedha au viongozi wa kisiasa yapaswa kupunguzwa ili kuondoa ukakasi wa dhamira, nia, na matamanio yenye kuakisi matumizi mabaya ya mamlaka, fursa, na rushwa. Tutazidi kusonga mbele.