SoC04 Mapinduzi ya soka Tanzania: Njia kuu za kuleta maendeleo na mafanikio

SoC04 Mapinduzi ya soka Tanzania: Njia kuu za kuleta maendeleo na mafanikio

Tanzania Tuitakayo competition threads

Fad114

New Member
Joined
Jun 14, 2024
Posts
1
Reaction score
2
Michezo haswa soka, ina uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko makubwa katika Tanzania. Michezo ni zaidi ya burudani tu kwani inaweza kuwa injini ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hata hivyo, ili kufikia hilo ni muhimu kufanya mabadiliko katika tasnia ya michezo. Katika makala hii, nitaangazia changamoto ambazo soka la Tanzania inakumbana nao na njia mbalimbali za kuboresha sekta hiyo.

CHANGAMOTO KATIKA SOKA LA TANZANIA
1. Uwanja na Miundombinu: Viwanja duni na miundombinu mibovu ni moja wapo ya changamoto kubwa katika maendeleo ya michezo nchini Tanzania. Kwenye nchi yetu kuna viwanja rasmi 21 ila viwanja vilivyokidhi vigezo vya kuchezewa mechi za kimataifa ni vitatu tu kikiwemo kiwanja cha Azam complex(Binafsi). Asilimia kubwa ya viwanja vimekuwa na changamoto ya pitch bora hii inapelekea michezo mengine kushindwa kuchezeka hasa kipindi cha mvua.Ukosefu huu wa Viwanja pia uliturudisha nyuma na kuchangia ukosefu wa faida kwenye maandalizi yetu ya mashindano ya AFCON U-17 2019 na kama tusipoliangazia hili basi tutakosa kupata ukubwa tunaohitaji kuelekea AFCON 2027.Sambamba na hilo changamoto ya viwanja inapelekea timu kupata changamoto ya makato makubwa ya viwanja endapo zitashiriki michuano ya kimataifa kama vile CAF champions league na Confederation cup mfano Singida BS FC msimu 2023/24 ililazimika kukodi uwanja wa Azam complex kwenye mechi mbili za Shirikisho kwasababu ya ukosefu wa viwanja bora mikoani na ilipelekea kupotezea asilimia kadhaa na faida ya mchezo huo kutokana na uwanja na hii ni changamoto kwa timu nyingi hapa Tanzania.

2. Ungaji mkono wa Mashabiki: Mashabiki ndio kitovu cha soka hivyo basi bila mashabiki hakuna maendeleo ya soka nchini. Kama nchi na uongozi mzima wa michezo kuna ukosefu wa hamasa na ushawishi wa mashabiki ambayo walipaswa kuwa moyo wa michezo.Katika nchin yetu kitu kikubwa kinachotunyonya ni Usimba na Uyanga Kwani asilimia kubwa ya wanasoka wanakosa hamasa ya kuspport timu za mikoani kwao na kubaki kushabikia Simba na Yanga pekee .Hii inatokana na uridhi pia msukumo mkubwa ambao timu hzo mbili kubwa uliokuwa nazo na inapelekea kurudi nyuma Kwa timu changa za mikoa kwasababu ya ukosefu wa mapato muhimu ya wanachama na mapato ya getini pia.

3. Ushawishi wa Wazazi: Wazazi wengi hawaelewi umuhimu wa kushirikisha watoto wao katika michezo na badala yake wanaamini ya kwamba shule pekee ndio mkombozi wa maisha ya watoto wao na hii inapelekea kuwasukuma watoto kwenye ndoto zisizondani yao na mwishowe kukosa hamasa katika kile wanachofanya. Ni jambo zuri kusimamia elimu ya darasani Kwa watoto lakini ni Jambo zuri zaidi kuwaelekeza watoto katika njia ya vipaji vya na kuwapa elimu ya darasani pia. Hali hii husababisha upungufu wa vipaji vya michezo na kuzuia ukuaji wa soko letu.

NJIA ZA KUBORESHA SEKTA YA MICHEZO
1. Uwekezaji katika Miundombinu
: Ili kuweza kufikia nchi ya ahadi katika michezo,Serikali na wadau wa sekta binafsi wanapaswa kuwekeza katika ujenzi na ukarabati wa viwanja na miundombinu ya michezo ili kutoa fursa bora kwa wachezaji na timu.Maboresho haya yanatakiwa kuanza katika pitch na kila eneo la ndani na nje ya uwanja.Ingawa kumekuwa na mgogoro mkubwa juu ya maboresho ya viwanja ambavyo vipo chini ya CCM ila inabidi kuwepo na sulisho kwa aidha viwanja viwe chini ya serikali na vikarabatiwe kwa hadhi ya juu ama CCM iboreshe viwanja vyake kwa kutumia fedha za mikopo na fedha hizo zitarudishwa kupitia timu zitakazotumia Viwanja hvyo kama sehemu ya makubaliano.

2. Kuhamasisha Mashabiki: Kuna haja kubwa ya kuandaa kampeni za kuhamasisha mashabiki na kutoa motisha kama vile zawadi na mikutano ya kipekee na wachezaji zinaweza kusaidia katika kuongeza ushiriki wa mashabiki na kujenga jamii imara ya michezo.Timu za kila mkoa zinabidi ziandae program maalumu ya kuvutia jamii hyo kushabikia timu zao na kuwa na mapenzi nayo na hii itafanya kazi hasa kwa watoto kupitia Wazazi wao.Tofauti kubwa Kati yetu na nchi za magharibi ni mchango wa mashabiki kwenye timu za kila mkoa na ili tuweze kujenga Ligi Bora na Timu ya taifa imara inabidi kuwepo na hamasa kwa mashabiki kusapoti timu za mikoani.Hili pia linaweza kufanikiswa kwa kuwepo na vikao Kati ya timu na wananchi kila mwezi katika maeneo ya mkusanyiko ili waweze kuelezeana changamoto na namna ya Kuboresha na kupitia ushirikisho huu wa mashabiki itaongeza mapenzi na hamasa ya mashabiki kwenye hizi timu za mikoani.Pia kuwepo na kadi za wanachama zinazopatikana Kwa bei rahisi ambayo itasaidia kuongeza idadi ya watu na mapato kwa timu pia. Mechi za kirafiki baina ya timu hizi za mikoani na timu za kijamii pia zinaweza kuchangia hamasa ya mashabiki kujiingiza katika timu.

3. Uandaaji wa academy zenye misingi ya kielimu na michezo: Ili kuweza kujenga misingi imara ya kimichezo na kutengeneza jamii ya kimichezo kuna haja kubwa ya kuwepo na academy Bora nchini katika kila mkoa na academy hizo ziwekwe katika misingi ya kielimu za darasani na michezo.Watoto katika academy hizo wanatakiwa kupewa elimu muhimu ya darasani kama vile hesabu, lugha(Kiswahili na kingereza) na afya ya mwili Kwani ndo vitu muhimu vya kujifunza na ambavyo vitaweza kuwasaidia katika kutimiza ndoto zao na kukuza vipaji vyao,Kwani kukaa darasani na kusoma masomo yote yalioandaliwa na wizara ya elimu ni upotevu wa muda na kupoteza vipaji vya watoto.Program hzi ziwe chini ya usimamizi maalumu wa TFF na wizara Kwa ujumla na itasaidia kuvutia mawakala kuja kuchukua vipaji kwaajili ya kujiendeleza ndani na nje ya nchi.

4. Elimu kwa Wazazi: Kuna haja kubwa kwa wizara ya michezo kuandaa programu za elimu kwa wazazi juu ya umuhimu wa michezo kwa watoto zinaweza kusaidia katika kubadilisha mitazamo na kukuza ushiriki wao katika kusaidia vipaji vya michezo vya watoto wao. Hii inaweza kufanikiwa Kwa kushirikiana na vyombo vya habari na watu wenye ushawishi katika nchi Kwa kuandaa matangazo mafupi na jumbe mbalimbali zitakazowashawishi Wazazi juu ya kuwaingiza watoto wao katika shule muhimu za vipaji(academy).

HITIMISHO
Katika kufanya mabadiliko haya, ni muhimu kwa serikali, mashirika ya kibinafsi, mashabiki, na jamii kwa ujumla kufanya kazi pamoja kwa lengo la kukuza tasnia ya michezo nchini Tanzania. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kufikia uwezo kamili wa michezo, na haswa soka, katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
 
Upvote 7
Bandiko zuri mkuu wakubwa wakifanyia kazi inawezekana kumleta athari chanya
 
Back
Top Bottom