Mapinduzi ya Zanzibar - Januari 12, 1964

Mapinduzi ya Zanzibar - Januari 12, 1964

paskali mbona historia ya mapinduzi ya znz inachanganya sana kila mtu kila jamii kila kikundi kila kabila kila dini ina historia yake tofauti ivi tuamini ipi na kwanini haichukuliwi juhudi ya pamoja kuunganisha hizi historia ili ipatikane historia kamilifu isiyo na utata?
Hili haliwezekani, kwa sababu mpaka kesho hakuna msimamo wa pamoja kati ya waliopindua na waliopinduliwa!. Waliopindulliwa mpaka kesho wana machungu, wanasingizia waliyepindua ni wabara!.

Wakati wengine wakiyaita ni Mapinduzi Matukufu ya 1964!, kwa wengine ni Mauaji ya Kimbari ya 1964!.

Ili kupata historia moja iliyotukuka, tuanze na tume ya ukweli na upatanishjo, "truth and reconciliation committee" nani alifanya nini, wasameheane, washikane mikono, wakae chini waandike historia moja!, tena saa hizi, waliokuwepo, waliopanga na waliotekeleza ni wakuhesabika!, wengi wao, imeishakuwa jioni!.
Pasco.
 
kajirita,
Field marshall John Okelo ni shujaa wa kutengenezwa kwa Mara ya kwanza alisikika pale tu alipopewa microphone awatangazie wazanzibari kuhusu mapinduzi Kabla ya hapo hamna aliemjua inasemekana hata Aboud Jumbe aliuliza "huyu kijana ni nani"

pale alipomuona Mara ya kwanza pale raha leo(radio station),sasa jiulize kama hao vinara wa mapinduzi walikuwA hawamjui huyu John Okelo cha kujiuliza huyu field maershall Okelo alikuwa anawaongoza akina nani na nani alimpa uwezo wa kupindua Zanzibar wakati yeye sio mzanzibari
 
Field marshall John Okelo ni shujaa wa kutengenezwa kwa Mara ya kwanza alisikika pale tu alipopewa microphone awatangazie wazanzibari kuhusu mapinduzi Kabla ya hapo hamna aliemjua inasemekana hata Aboud Jumbe aliuliza "huyu kijana ni nani" pale alipomuona Mara ya kwanza pale raha leo(radio station),sasa jiulize kama hao vinara wa mapinduzi walikuwA hawamjui huyu John Okelo cha kujiuliza huyu field maershall Okelo alikuwa anawaongoza akina nani na nani alimpa uwezo wa kupindua Zanzibar wakati yeye sio mzanzibari


Mkuu,
Narudia!

Je,ni vipi John Okello alipata nguvu ya kuunda baraza la kwanza la mawaziri baada ya mapinduzi?

Je,ni kwa nini John Okello ndio alikuwa akitoa hotuba pale Raha leo baada ya mapinduzi matukufu?(Hotuba kama zile za JK za mwisho wa mwezi)

Je,ni kwa nini yeye ndie aliyemchagua rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Karume alipokimbilia Dar es Salaam siku yalipotokea mapinduzi hayo labda kwa kuogopa au kwenda kumpa taarifa JK Nyerere(kama alivyodai) na kumuita kwa mamlaka "popote ulipo urudi kuchukua nafasi yako ya urais"?

Je,ni kwa nini kwenye hotuba ya kwanza ya Mzee Karume alisema wazanzibar wamtambue John Okelo kama mtu muhimu sana aliyesaidia kufanyika na kufanikisha kwa mapinduzi hayo(rejea hotuba ya kwanza kabisa ya karume kama rais wa nchi)?

Naomba unijibu maswali hayo tu,au umtafute yule aliyekwambia Aboud Jumbe alisema "huyu kijana ni nani?" akusaidie !!!!!

Asante!
 
waliozoea ujanja ujanja Tanganyika wengi ni hawa wajiitao wagalatia , kwa maana wamezoea kugeuzwa kondoo makanisani

kondoo lakini tunawatawala! sasa nyinyi mtakuwa ma.bwe.ge kiasi gani kutawaliwa na Kondoo?
 
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
 
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
Utukufu unaongozwa na umwagaji damu usio na hatia hauwezi kuwa utukufu,uteuzi hautafutwi hivyo kilaza.

Sent using tecno tochi
 
Waso Haya wana mji wao. Rasimu ya pili imetoka na Tanganyika inarudi. Sijui kama tutakuwa na Tanzania lakini jitayarisheni maana sisi hatutaki tena muungano bandia. Na kura ya maoni ya kujitenga tunaifanyia mipango kabambe.


Sidhani kama itawezekana itakuwa kama IRAN na USA
 
Utukufu unaongozwa na umwagaji damu usio na hatia hauwezi kuwa utukufu,uteuzi hautafutwi hivyo kilaza.

Sent using tecno tochi
[/QUOTE


Hakuna haki iliyopatikanaga bila kumwaga damu yakhheee Mapinduzi yasingefanikiwa bila Okello na timu yake kupiga mapanga na mikwara Huo ndio uwanaume
 
kajirita,
wewe hata hujui chochote kuhusu Zanzibar

unasema Sultan alivyokuja hakukuta watu Zanzibar , hivi hata umesoma au kusikia chochote kuhusu Zanzibar ?? ni bora ukajikita kuikomboa Tanganyika kutoka kwa Dictator JIWE na mafia yake ya CCM kuliko kuchupia nchi zilizovamiwa na kanisa katoliki
 
Mshume Kiyate,
Watu hawa walisalitiwa au walisaliti?
Nimenukuu baadhi ya maneno humu kwenye Andiko lako

Okello alikuwa ni adha, kitisho, kichekesho na fedheha kwa Zanzibar. Viongozi wapya wa nchi walichoka naye na wakaamua kumchukulia hatua.

Babu, Ali Mahfudhi, Badawi, Hanga,Othman Sharif,Twalla waliuliwa,na hatimae 1972 Karume Mwenyewe kuuwawa pia,
Aidha 1984 Jumbe Kulazimishwa kujiuzuli na uwekwa kizuizini hadi kifo.

Hebu tuelezeni nani hasa aliyekuwa KEY PLAYER WA MAPINDUZI?
na NI NANI ALIYEFAIDIKA NA MAPINDUZI KATI YA Zanzibar na Tanganyika?ikiwa maneno hayo ya kusalitiana ni kweli!
TANBIHI
Tatizo kubwa la Zanzibar litabaki kuwa ni kwa Wazanzibari kukubali kuhadaiwa na wanasiasa uchwara kuendelea kuwa wafungwa wa historia ya kisiasa iliyoigawa jamii katika makundi ya kikabila na kinasaba.
 
P...

MWANAHISTORIA ANAYACHAMBUA MAPINDUZI NA MAANA YAKE

Ayatollah Mohammed Said: Radio Uhai FM

SWALI:
Sherehe za mapinduzi kadri tunavyoendelea kuziadhimisha vizazi vinavyokuja vinajifunza kitu gani?

JIBU
Kwanza ni kuwa watu wengi washajua ukweli wa mapinduzi. Na hayana nguvu au umuhimu kama viongozi wetu wanavyodhani. Watu wanataka maendeleo na utangamano, wamepiga kura hapa ya serikali ya umoja wa kitaifa, umeona matokeo yake, watu wengi wamepiga kura kutaka serikali ya umoja wa kitaifa.

Sasa yale mambo ya mapinduzi, ya sijui tulikuwa tukifanywa hivi na vile, hakuna mtu sasa anayetaka kusikia hivyo. Mambo hayo yanepita. Watu wanataka kutizama mbele. Na kuona nchi inatoka kwenye umasikini inakwenda kwenye maendeleo. Kadri tunavyokwenda ndio hawa wana mapinduzi wanavyozidi kupoteza nguvu.

Kama nilivyokuambia mwanzo kama kweli haya mapinduzi yana nguvu hivyo mbona wanashindwa kushinda uchaguzi huru na haki??

SWALI:
Uligusia pale mwanzo sheikh Mohammed kwamba kuna swala moja kubwa sana kila unapotazama historia ya kweli kabisa iliyoandikwa kuhusu mapinduzi yanazungumzwa masuala ya mauaji makubwa sana ambayo yalitokea. Hiyo inabaki kuwa ni kumbukumbu kubwa sana. Haya mauwaji yalitokana na msigano wankitu gani. Nini sababu hasa?

JIBU:
Ndio, Profesa Ibrahim Noor akaandika kitabu kile "Propaganda na udini Tanzania", akaonesha tarekh yake. Zile propaganda za kuwa Waarabu walikuja kukamata watumwa. Utumwa umefanywa na mataifa mengi. Hakuna utumwa mbaya kama ule wa Trans Atlantic Slave Trade - unaotoka Afrika magharibi na kuvuka bahari kwenda Marekani. Ule ndio unyama mkubwa. Hakuna utumwa mbaya kama wa Ubelgiji Kongo. Hawayasemi hayo. Wao kila siku wanawasingizia Waarabu tu. Na ukiwapeleka huko huwa hawana la kusema, wananyamaza kimya. Hizi propaganda ndizo zilizosababisha mauaji makubwa sana kutokea baada ya miaka zaidi ya 150 kuondolewa kwa biashara ya utumwa.

Miaka kama 20 iliyopita tusingeweza kufanya kitu kama hiki watu wakatusikiliza. Leo hivi tunazungumza bila ya matatizo. Na vijana wetu wanatakiwa waelezwe ukweli wa historia. Kuwa hii ni historia. Na usemwe ule ukweli. Watu wanaelewa. Na ndio maana kwa kuelewa kwao huko wanamapinduzi wanashindwa kushinda chaguzi huru.

SWALI:
Hebu nisaidie kunifumbua kidogo hata kwa jinsi ulivyosoma tu. Turudi nyuma zaidi ya 1964 kwanzia miaka ta 1952 uliozaliwa wewe kwenda nyuma, je maisha ya Zanzibar yalikuwa ni ya namna gani?

JIBU:
Nitakwambia kitu kimoja. Kulikuwa na watu wana nafasi zao katika jamii ya Waarabu hili huwezi kuliepuka. Haya yote ni katika madhara ya ukoloni. Na Sultan alikuwa hana nguvu hivyo. Nguvu zote alikuwa anazo Muingereza.

Kulikuwa na Waarabu masikini wakifanya kazi za vinyozi, wakilima, wakiuza kahawa mitaani, na wengine wakifanya kazi za utopasi zile za kutapisha choo, zamani vile vyoo vya shimo wanakuja kupakuwa na wakibeba kwa mapipa kwenda kumwaga. Si kama Waarabu wote walikuwa katika hali ya juu. Walikuwepo masikini. Wakitumikishwa kazi kama anavyotumikishwa Muafrika. Ukisoma kitabu cha Profesa Ibrahim Noor utayakuta haya yote. Na hizi chuki wanazosema ni za kupandikiza. Sultan aliondoka Zanzibar bila ya kuuwa raia wake, aliondoka mikono misafi haina damu ya mtu yeyote. Damu imeanza kumwagika baada ya hao wanaoitwa wanamapinduzi kushika serikali. Ndio wakaanza kuuwa watu na kuwaweka kwenye jela za mateso. Nadhani nimelijibu suali lako.

#Pray4Zanzibar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,
Kama kuna siku umeongea maneno ya Kinabii ni leo,
Yakupasa sasa utazame mbinguni umshukuru Mungu kwa kukufunulia yale ambayo wengi bado kuyaona.
Amani Karume na Maalim Sefu walisha paona hapo,lakini Mzee Sefu Idi na Sheni bado Hasama Inawapwita kama vile alivyo Mkapa na maparish wa kanisa la Mkunazini
.
UKWELI NI KWAMBA ''Zanzibar ya leo haina tena hali zile za zamani ,isipokuwa kuna watu wamechukua 'contract' kuzifufua na kuzihamasiha hisia za kibaguzi ili kupata maslahi fulani ,na hasa wale jamaa zetu wenye hofu na Uzanzibari wao,wakidhani kuwa damu ile iliyomwagwa itaendelea kuwalilia masikioni mwao, na kukataa kwao kutubia.

Mbele za Muungu Mapinduzi yale dhulma na dhambi kuu ,yalifanywa kwa mauaji ya watu wasiokuwa na hatia.Kitendo kile cha mauwaji ya kimapinduzi kinaweza kumnyima mtu haki ya kuingia katika ufalme wa milele mbinguni, labda watubie na kujut. 'ILA KISIASA ,KWAO MAPINDUZI NI MATUKUFU NA HALALI KWA VILE WALIPATA UKUU WA DUNIA HII HATA KWA NJIA ZA DAMU ZA WENGINE WASIOSTAHIKI, DAMU ZA WANAWKE, WATOTO,WAZEE WASIOKUWA NASILAHA, WALIOTIWA KWENYE MATANURI YA KUOKEA MBATA .' HUU NDIO UTUKUFU?
 
Back
Top Bottom