P...
MWANAHISTORIA ANAYACHAMBUA MAPINDUZI NA MAANA YAKE
Ayatollah Mohammed Said: Radio Uhai FM
SWALI:
Sherehe za mapinduzi kadri tunavyoendelea kuziadhimisha vizazi vinavyokuja vinajifunza kitu gani?
JIBU
Kwanza ni kuwa watu wengi washajua ukweli wa mapinduzi. Na hayana nguvu au umuhimu kama viongozi wetu wanavyodhani. Watu wanataka maendeleo na utangamano, wamepiga kura hapa ya serikali ya umoja wa kitaifa, umeona matokeo yake, watu wengi wamepiga kura kutaka serikali ya umoja wa kitaifa.
Sasa yale mambo ya mapinduzi, ya sijui tulikuwa tukifanywa hivi na vile, hakuna mtu sasa anayetaka kusikia hivyo. Mambo hayo yanepita. Watu wanataka kutizama mbele. Na kuona nchi inatoka kwenye umasikini inakwenda kwenye maendeleo. Kadri tunavyokwenda ndio hawa wana mapinduzi wanavyozidi kupoteza nguvu.
Kama nilivyokuambia mwanzo kama kweli haya mapinduzi yana nguvu hivyo mbona wanashindwa kushinda uchaguzi huru na haki??
SWALI:
Uligusia pale mwanzo sheikh Mohammed kwamba kuna swala moja kubwa sana kila unapotazama historia ya kweli kabisa iliyoandikwa kuhusu mapinduzi yanazungumzwa masuala ya mauaji makubwa sana ambayo yalitokea. Hiyo inabaki kuwa ni kumbukumbu kubwa sana. Haya mauwaji yalitokana na msigano wankitu gani. Nini sababu hasa?
JIBU:
Ndio, Profesa Ibrahim Noor akaandika kitabu kile "Propaganda na udini Tanzania", akaonesha tarekh yake. Zile propaganda za kuwa Waarabu walikuja kukamata watumwa. Utumwa umefanywa na mataifa mengi. Hakuna utumwa mbaya kama ule wa Trans Atlantic Slave Trade - unaotoka Afrika magharibi na kuvuka bahari kwenda Marekani. Ule ndio unyama mkubwa. Hakuna utumwa mbaya kama wa Ubelgiji Kongo. Hawayasemi hayo. Wao kila siku wanawasingizia Waarabu tu. Na ukiwapeleka huko huwa hawana la kusema, wananyamaza kimya. Hizi propaganda ndizo zilizosababisha mauaji makubwa sana kutokea baada ya miaka zaidi ya 150 kuondolewa kwa biashara ya utumwa.
Miaka kama 20 iliyopita tusingeweza kufanya kitu kama hiki watu wakatusikiliza. Leo hivi tunazungumza bila ya matatizo. Na vijana wetu wanatakiwa waelezwe ukweli wa historia. Kuwa hii ni historia. Na usemwe ule ukweli. Watu wanaelewa. Na ndio maana kwa kuelewa kwao huko wanamapinduzi wanashindwa kushinda chaguzi huru.
SWALI:
Hebu nisaidie kunifumbua kidogo hata kwa jinsi ulivyosoma tu. Turudi nyuma zaidi ya 1964 kwanzia miaka ta 1952 uliozaliwa wewe kwenda nyuma, je maisha ya Zanzibar yalikuwa ni ya namna gani?
JIBU:
Nitakwambia kitu kimoja. Kulikuwa na watu wana nafasi zao katika jamii ya Waarabu hili huwezi kuliepuka. Haya yote ni katika madhara ya ukoloni. Na Sultan alikuwa hana nguvu hivyo. Nguvu zote alikuwa anazo Muingereza.
Kulikuwa na Waarabu masikini wakifanya kazi za vinyozi, wakilima, wakiuza kahawa mitaani, na wengine wakifanya kazi za utopasi zile za kutapisha choo, zamani vile vyoo vya shimo wanakuja kupakuwa na wakibeba kwa mapipa kwenda kumwaga. Si kama Waarabu wote walikuwa katika hali ya juu. Walikuwepo masikini. Wakitumikishwa kazi kama anavyotumikishwa Muafrika. Ukisoma kitabu cha Profesa Ibrahim Noor utayakuta haya yote. Na hizi chuki wanazosema ni za kupandikiza. Sultan aliondoka Zanzibar bila ya kuuwa raia wake, aliondoka mikono misafi haina damu ya mtu yeyote. Damu imeanza kumwagika baada ya hao wanaoitwa wanamapinduzi kushika serikali. Ndio wakaanza kuuwa watu na kuwaweka kwenye jela za mateso. Nadhani nimelijibu suali lako.
#Pray4Zanzibar
Sent using
Jamii Forums mobile app