Mapinduzi ya Zanzibar na Nyerere

Mapinduzi ya Zanzibar na Nyerere

Ukisoma kitabu cha KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU cha mwandishi Harith Ghassany unakaribia kulia ukijua kwamba kumbe Mapinduzi ya Zanzibar si kama tunavyoyajuwa.Kwa upande mwengine kumbe uongo ni kitu kibaya sana kinacholeta maangamizi katika jamii.
Mwandishi anastahiki sifa kubwa ya kuwa mtafiti aliyebobea.Amehojiana na watu muhimu walioshiriki kuipindua serikali ya Zanzibar ambao wengi wala si wenye kusikika.

Nyerere anaonekana ni shujaa mno.
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Kazi Iendelee!.

Paskali
 
i Hakuna ubishi kuhusu ushujaa wa Karume kwenye Mapinduzi ya Zanzibar ila kutokuwepo kwakwe kusisingiziwe ni Nyerere.

Karume aliwachukua wanae Amani na Ali usiku wa manane, wakasafiri kwa mtumbwi kuja bara. Wakashukia Bagamoyo.

Ukweli ni kwamba, Karume aliyakimbia Mapinduzi kuokoa nafsi yake na wanaye just incase mapinduzi yale yasinge faulu, japo sababu iliyotolewa sio kwamba Karume alikimbia bali eti alikuwa anawapeleka shule wanawe Amani na Ali walikuwa wakisoma shule nchi alikozaliwa baba yao, Malawi!.

Maadam mapinduzi yamefanikiwa, Karume alirejea Zanzibar na ni shujaa wa mapinduzi!.
Mwana JF, Paskali, anakutakia wewe na familia yako HERI YA SIKUKUU YA MAPINDUZI MATUKUFU
YA ZANZIBAR!
Paskali
 
Back
Top Bottom