Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.Ukisoma kitabu cha KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU cha mwandishi Harith Ghassany unakaribia kulia ukijua kwamba kumbe Mapinduzi ya Zanzibar si kama tunavyoyajuwa.Kwa upande mwengine kumbe uongo ni kitu kibaya sana kinacholeta maangamizi katika jamii.
Mwandishi anastahiki sifa kubwa ya kuwa mtafiti aliyebobea.Amehojiana na watu muhimu walioshiriki kuipindua serikali ya Zanzibar ambao wengi wala si wenye kusikika.
Nyerere anaonekana ni shujaa mno.
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.
Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Kazi Iendelee!.
Paskali