Ghibuu, unapoamua kudanganya na kupotosha historia ya Zanzibar, basi angalau sema uwongo unaokaribiana na ukweli.
Umedanganya kihusu asilimia ya Waislamu Zanzibar kuwa ni asilimia 100% kwa 100%. Kimahesabu maana yake asilimia ya Wakristo ni 0.00% jambo ambalo si kweli!.
Naomba kukumbusha, hao waarabu unaowashabikia na kuwasujudia, nao ni watu wa kuja tuu huko Zanzibar, Sultan Said Said alitoka zake Oman na kuhashia makazi yake Zanzibar katika karne ya 17. Hapo Zanzibar alipakuta kuna wenyewe ambao ni wenyeji wa asili wa Zanzibar, jee unajua aliwafanya nini?. Unakijua kilicho wakuta?. Unajua ni kwa nini hawatajwi popote?.
Hilo na tuliache. Katika karne ya 18 jee unafahamu Zanzibar ndio ilishamiri kwa biashara ya utumwa?. Jee una taarifa watumwa waliopelekwa nchi za India na nchi za Kiarabu wote walitoka soko la Zanzibar?.
Jee unafahamu watumwa waliopelekwa nchi za Marekani na Ulaya walitoka soko la Afrika Magharibi?,
Unajua kilichowapata watumwa walipelekwa Arabuni na bara Hindi?,
Jee unafahamu baada ya kusimamishwa kwa biashara ya utumwa, watumwa wote waliokuwa sokoni na waliopenda kurejeshwa barani Afrika walirejeshwa?.
Watumwa wa soko la Marekani walirejeshwa nchini Liberia na wale wa Ulaya wakarejeshwa nchini Sierra Leone, jee wale wa soko la Zanzibar walirejeshwa wapi?.
Baada ya kusitishwa kwa biashara ya utumwa hata Zanzibar, jee wajua kuwa watumwa waliikwisha nunuliwa ili wawe huru, ilibidi wagombolewe kwa wanunuzi kurudishiwa fedha zao?, Jee wajua waliowagomboa ni kina nani na watumwa waliogombolewa walipelekwa wapi hapo Zanzibar?,
Jee wajua eneo lilipokuwepo soko kuu la watumwa Zanzibar enzi hizo leo pana nini?.
Majibu ya maswali hayo yatapunguza uwongo na utakatifu wa Waarabu unaowasujudia na kwa kwa vile ndio babu na bibi zako upande wa kikeni, then hakika wee uu mmoja wao?,
Mkuu.
Hakuna nchi ambayo isikuwa na na biashara hio ya utumwa,unaposema waarabu walifanya utumwa basi pia weusi na weupe wazungu walishiriki,na wanunuaji wote walishiriki,usisukumize mzigo kwa waarabu tu hata mababu zetu walishiriki asilimia mia moja.
kwa sababu waarabu walipokuwa wakitaka watumwa,wakiende katika vijiji,zamani maiak hio kabla ya utawala wa wa kidemocracy na kisiasa,kulika na watawala wa vijiji kama wafalme,hao wafalme wa vijiji mababu zetu walikuwa wakipewa viyoo,au sufuria,wakiwatoa kaka zetu kwa waarabu au wazungu kwa kuwahadaa vitu vidogo.
Mababu zetu hawakufahamu nini mazumuni ya kuwauza vijana hao wazee wetu,na walichukulia kama ni suala la kiwaida,miaka nenda nenda miaka rudi mambo yakabadilika,wenzetu walisoma waliweza kuturubuni,kwanza naweza kusema utumwa hasa ulibebeba sana katika north africa kulika huku east africa,tukubali kila kitu kilikuwa na hasara na faida. lakini naweza kusema faida tulio ipata kwa waarabu japokuwa walitufanya utumwa waliweza kuleta mabadiliko makubwa katika dunia hii,mana kama sio wao ingelikwa Uwengereza hakuna mtu mweusi,uwarabuni hakuna mtu mweusi,marekani hakuna mtu mweusi,ingefika time tungeliuwana baina ya waarabu,weuzi weupe wazungu,haya yote ilikuwa ni kama game tu ,kila jamabo lilienda kwa wakati.
Lakini suala hili la nyerere kuimaliza zanzibar halikuwa na kiutumwa bali lilikuwa la kisiasa,unajua zanzibar ilipata uhuru wake 1963 kuwa mwanachama wa UN ? Unajua kuwa mwanachama wa UN sheria zake ? Soma nyakati mtu wangu,moja ya sheria zao ni humaina right,humain afair. Na ndio ilikubaliwa kuwa mwanachama wa UN.
Tanganyika haikuwa kuwa mwanachama wa UN,na kitu ambacho kinachotumiwa na Tanzania /Tanganyika katika UN ,ni kiti cha zanzibar.
Nyerere roho ya uchoyo ndio iliyomtoka zanzibar TU.