AXIOM APEX VERBOSE
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 13,769
- 23,676
Okello aliwaambia wenzie kwamba tunapofanya haya mapinduzi ueni vijana wa kiarab/kiasia kuanzia miaka 18 hadi 25 ila wajawazito na wazee msiue wala msiwabake mabinti mabikra.. sasa unajua nini kilifuata? alipowaambia waelekee Stone Town, Capital City of Zanzibar ambako Sultan alikua anaishi.. jamaa yaan [wafuasi] wa Okello (sio Okello) ukiacha mbali kuharibu mali na kuchoma majumba [waliwabaka] wanawake wengi sana ikiwemo mabikra.. ugomvi wa Karume na Okello.. siku ya Mapinduzi sio Karume wala sio Babu waliokua wanajua kuhusu Mapinduzi maana Karume na Babu wote walikua Dar.. Okello akafanya yake akatangaza redioni Sultan aiue familia yake kisha na yeye mwenyewe ajiue la sivyo Okello atamsaidia kufanya hivyo.. Okello baada ya kuzinguana na Karume baada ya Karume kua Rais alimtimua Okello Zanzibar kwa sababu Zanzibar ni Wapemba na Wazanzibar akatakiwa kurudi kwao Uganda.. Okello akapitia Kenya, Zaire kisha akaingia Uganda.. Okello anaenda kukutana na Mtiti wa Iddi Amini Dada wa Uganda.. baada ya kutoka Zanzibar kwa kutimuliwa na Karume alipokua Zanzibar Okello alijipa u-Field Marshal baada ya kumpindua Sultan kwa hio km [pongezi/zawadi] baada ya kuonekana [ha-fit] kwenye masuala ya kisiasa alipewa title ya Field Marshal Okello na Rais Karume baada ya kuzinguana nae tarehe 11 March akavuliwa u-Field Marshal sasa alipofika Uganda na kukutana na Iddi Amin [akamtania] Iddi Amini ambae pia alikua anajiita Field Marshal kwamba "sasa Uganda ina ma-Field Marshal [wawili].." Iddi Amini kusikia hivyo akainusa hatari akaona isiwe kesi (akampoteza Okello) akiwa na miaka 33 kuelea 34 baada ya kuonekana na Iddi Amin Okello hakuwahi kuonekana tena.. mwaka 1971 ndio mara ya mwisho Okello kuonekana baada ya kuonekana na Iddi Amin na ndio mwaka Iddi Amin alijitangaza u-Field MarshalLakini aliyempindua Sultan Jamshid ni John Okello. Ambae hakufaidi hata kwa tone mapinduzi ya Zanzibar.