Mapinduzi ya Zanzibar yasiyo na shukrani kwa John Okello


IDADI YA WATU WALIOUWAWA SIKU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NI 13,635 Tarehe 12January1964.
(John Okello)

Historia ni somo linalohusu matokeo mbalimbali katika vipindi mbalimbali katika mambo Mbalimbali yanayohusu nchini kwetu..!
Kujuwa historia yetu ni matokeo yaliotokea huko nyuma kutatusaidia kujua tulikotoka, tunapokwenda na tulipo hivi sasa.

Mapinduzi ya tarehe 12 Jan, 1964 yalioongozwa na John Okello.
Okello aliajiriwa kutokana na ukatili wake tarehe 11 Jan, 1964 Okello alihutubia makundi ya wavamizi aliyoyaita Freedom Fighters Akawaambia Hivi..:

"Mwenyezi Mungu Ameniteuwa mimi kufanya Mapinduzi kwa Ajili ya ukristo....!
Na kisha Akasema maneno ya Ndani ya Biblia ili kuhalalisha Dhamira yake ya kufanya mapinduzi Alisema maneno haya :

" Na sasa sikilizeni Enyi Matajiri lieni na kuomboleza kwasababu ya Tabu zitakazo kujieni, Mali zenu zimeoza na nguo zenu zimeliwa na nondo, dhahabu yenu na fedha vimeota kutu hiyo itakuwa ushahidi dhidi yenu, nitakula miili yenu kama vile moto.
Ninyi mumejilundikia Mali katika siku hizi za mwisho hamkuwa lipa mishahara watumishi waliofanya kazi katika mashamba yenu, sikilizeni malalamiko yao, kilio cha hao wanaovuna mashamba yenu kimefika masikioni kwa BWANA, Mwenyezi Mungu. Mumeishi Duniani maisha ya kujifurahisha na ya anasa. Mumejinenepesha tayari kwa siku ya kuchinjwa mumemuhukumu mtu asie na hatia nae hakuwapigeni. JAMES 5: 1- 6

Okello Aliendelea kuwahutubia Askari Mamluki kabla ya kuanza Mapinduzi yaliopoteza Roho za watu wengi sana visiwani zanzibar.

"Wapenzi ndugu zangu, nimesimama mbele yenu na Naapa kwa Mchana na Usiku kuwa Nipo Tayari kuwaonesha vipi tutaweza kujitawala.
Mababu zenu, baba zenu na sasa nyinyi wenyenu munateseka na ukandamizaji wa waarabu kwenye Visiwa hivi...!

Mnajuwa kuwa matumbo ya mama zenu yalifunguliwa ili mabibi wa kiarabu wapate kuona namna ya mtoto anavyokaa ndani..?.
Mnajuwa mababu zenu walichinjwa chini ya miti hii ili mabibi wa kiarabu wapate kuona namna ya binaadamu waliokufa wanavyoanguka si mahala hapa hapa...? waliokandamizwa Babu zenu?

Nitaendelea kuwakumbusha kuwa masoko ya utumwa pamoja na vyuma na minyororo waliokuwa wakifungiwa ndugu zenu bado inaonekanika kisiwani, pamoja na makaburi ya halaiki walimozikwa waafrika waliouliwa, wao wenyewe wameonesha mapango mengine ambayo damu ya waafrika ilimwagika juu ya ardhi.
Damu ya mababu zenu ilimwagika chini ya utawala wa kiarabu, mnataka kuona damu za watoto wenu zikimwagika pia. !

Nani ataweza kunambia vipi waarabu waliingia kunako visiwa hivi na vipi walivyovitawala....?

" Amkeni Enyi watu weusi, kila mmoja achukuwe Panga na Bunduki na risasi na kuanza kupambana dhidi ya mabaki yoyote ya ubeberu katika visiwa hivi.
Revolution in Zanzibar ukurasa 143.

Na akawaamrisha makundi yake na kuwaambia waarabu wenye umri kati ya miaka 18-55 lazima wauwawe
(must be killed)
Page 126 Revolution in Zanzibar.

Okello amekiri wazi wazi kwenye kitabu chake cha Zanzibar Revolution UK 119, 130- 131 kuwa hakuwaamini wazanzibari na wengi waliopi dua walitoka nchi jirani.

Aliwaambia:
"Mtaona jinsi tunavyowanyonga watu na kuwachoma kama kuku wengine watakatwa vipande vipande na kutandazwa mitaani wengine watatupwa baharini na wengine watafungwa kwenye miti na kupigwa risasi.

Okello alituma ujumbe kwa kutumia redio na kusema; "Mawaziri wa Zanzibar wa serikali ya ZNP/ZPPP wangenyongwa.

Okello akatuma ujumbe Redioni kwa Sultan Jamshid bin Abdalla:

"Nakupa dakika 20 uwauwe watoto wako na wake zako na kisha ujiuwe mwenyewe.

Lakini Sultan Alikwisha kimbia na kuelekea Nchini Kenya Mombasa.

Okello hapo Alikuwa Hazungumzi na wazanzibari, Bali Alikuwa Akizungumza na watu wengi wao, waliotoka Nje ya Zanzibar Mamluki (Tanganyika) kwasababu Hakuwaamini Wazanzibari.

Hotuba hiyo ndio iliyochukuwa Roho 13,635 za wazanzibari siku kama ya Leo 12 Jan, 1964....! (John Okello)
 

Ni kupokezana kijiti kwa familia ya Karume na Mwinyi kuwa marais wa Zanzibar.
Ni kweli.
Lakini aliyempindua Sultan Jamshid ni John Okello. Ambae hakufaidi hata kwa tone mapinduzi ya Zanzibar.
Mhusika mkuu wa hili ni Nyerere. Kwa hofu yake kuwa Okello angekuwa kikwazo kwa muungano akapanga na Karume, akamuita Dar, alipofika akamzuia kurudi Zanzibar na kule Karume akamtangaza kuwa mtu asiyetakiwa.
Leo hii Zanzibar inatawaliwa kisultani tena. Maana Watawala wanarithishwa.
Ni kweli.
John Okello hatajwi kabisa kama ndie aliyemuondoa mwarabu.
Wanasema eti alidandia tu. Kumbuka ule usemi wa Kiswahili usemao "lishalovuusha gogo".
 
Ni kwa sababu waliofanya Mapinduzi/ mavamizi ni watu kutoka Tanganyika
Hata majina hawana? Au ni kwamba hakukuwa na mapigano na wapinduzi walipita mitaani na kuuwa tu. Nahisi kama wapo miongoni mwa wapinduzi aliefariki January 12 wangekuwa wametajwa na kujengewa minara.
 
Nawe unaongea hizo hadithi za sauti nzito hahahaaa astakafirah walah..!!
 
Hata majina hawana? Au ni kwamba hakukuwa na mapigano na wapinduzi walipita mitaani na kuuwa tu. Nahisi kama wapo miongoni mwa wapinduzi aliefariki January 12 wangekuwa wametajwa na kujengewa minara.
Unayajua majina ya wanajeshi wa Tanganyika ?
 
Mimi siyajuwi. Just curious. Mimi naona kulikuwa na mauaji tu tafauti na watawala wanavyotuaminisha kwamba babu zao walimwaga damu zao kuikomboa Zanzibar.
 
Wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar Karume alikuwa amejificha Magogoni Dar es salaam.1964.

Mapinduzi yote yalifanyika chini ya Field Mash John Okello wa Uganda.
 
Halafu huyu Okello ndio mjukuu wa huyu kijana wa yanga
 
Kambarage alikuwa mjanja sana yaani alimtumia Okello na Kambona then akawa dampo. So sad
 
Mastermind wa mapinduzi ya Zanzibar yumkini alikuwa Mwalimu.
 
Familia yake ya watoto wengi inaishi kasikazini mwa Uganda. Serikali ya zanzibar iwashukuru na kuwapongeza kwa ujasiri na juhudi ya baba yao kuongoza Mapinduzi.
 
John Okello is unsung hero of African nationalism
 
Aliambatana na Iddi Amin na baadae Amin aliona Okello kama tishio akamuua na mwili haukuonekana hadi leo. Okello ana bahati mbaya sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…