GARETHBALE
Member
- Dec 22, 2013
- 76
- 333
Kesi ya Bernad Membe dhidi ya Musiba kusikilizwa tar 31 Machi, 2020 hii ni baada ya mapingamizi ya awali yaliyokuwa yamewasilishwa na Musiba na wenzake kutupwa na Mahakama Kuu.
Leo tar 27 Desemba, 2019 Mahakama Kuu Masjala ya Dar es Salaam imetoa uamuzi dhidi ya mapingamizi matatu yaliyokuwa yamewasilishwa na Cyprian Majura Musiba na wenzake baada ya kusikilizwa na Mahakama hiyo tar 03 Oktoba, 2019.
Katika Shauri hilo namba 220 la mwaka 2018 Bernad Membe anawakilishwa na Wakili Jonathan Mndeme. Akieleza kuhusu mapingamizi hayo Wakili Mndeme alisema kwamba mapingamizi hayo yalijikita katika hoja tatu;
1. Kwamba Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo na kwamba malalamiko ya Mdai yalitakiwa kupelekwa kwenye Baraza la Habari kwa mujibu wa Sheria ya huduma za Habari ya mwaka 2016.
2. Kwamba, hakuna kesi ya msingi dhidi ya Waidaiwa.
3. Na kwamba kesi ya msingi inakiuka Kanuni 6 Kanuni ndogo ya 3 ya Sheria ya mwenendo wa makosa ya madai ( Order VI Rule 3 of Civil Procedure Code Cap. 33).
Kuhusu pingamizi la awali la kwanza Mahakama Kuu imekubaliana na hoja za Wakili Mndeme kwamba sheria ya huduma za Habari ya mwaka 2016 kifungu cha 26, 27 na 28 hailazimishi mashauri ya kashfa kupelekwa kwenye Baraza la Habari na kwa hiyo Mahakama Kuu inayo mamlaka ya kuendelea kusikiliza shauri hilo.
Hoja zilizobaki Mahakama Kuu imetupilia mapingamizi yote kama yalivyowasilishwa na Mdai na kuona kwamba hazina msingi na kwa hiyo itaendelea kusikiliza shauri hilo tar 31 Machi, 2020.
Uamuzi huo umetolewa na Mheshimiwa Jaji De Mello na kusomwa na Mheshimiwa Msajili R. MASSAM mbele ya Mawakili wa pande zote mbil.