Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Amri hiyo ya Mahakama kuanza kesi ya mapingamizi ya Mwijaku kabla ya kesi ya msingi ya Kipanya, imetolewa Jumanne wiki hii na Mhe Jaji Ngunyale baada ya kupokea hati ya utetezi ya mawakili wa Mwijaku kutoka kampuni ya uwakili ya Jundu & Adadi Co. Advocates iliyowasilishwa mahakamani na Wakili Gideon Opanda.
Mawakili wa Kipanya kutoka kampuni ya uwakili ya Haki Kwanza Advocates, wakiongozwa na Wakili Alloyce Komba walikubaliana na amri hiyo ya kusikilizwa kwanza kesi ya mapingamizi.
Pamoja na Wakili Komba mawakili wengine wanaomtetea Kipanya ni Gerson Mosha na Rose-Shubi Mutakahwa ambao wanajiandaa kukabiliana na mapingamizi ya mawakili wa Mwijaku wanaoiomba mahakama ifute kesi ya msingi kwa gharama kutokana na kasoro za kisheria walizobaini.
Mapingamizi ya Mwijaku yanahusu uwezo wa mahakama kusikiliza kesi hiyo, makosa ya uthibitishaji maelezo ya mdai, kukosekana usahihi wa vielelezo na kutozingatia kanuni za mwenendo wa mashitaka ya kashfa za mwaka 2019.
Katika kesi ya msingi Masoud Kipanya anaiomba Mahakama Kuu kumtaka Burton Mwijaku amlipe sh bilioni tano na milioni mia tano kwa kumkashifu kupitia ukurasa wake wa FB na mitandao mingine ya kijamii kwamba yeye amekuwa akijihusisha na biashara haramu na amekuwa akihongwa kuwachafua viongozi wakuu wa Serikali akiwemo Rais.
Mwijaku hivi sasa anatetewa na Kampuni ya mawakili ya viongozi wastaafu: Jaji Kiongozi Mstaafu, Abdallah Rheno Jundu na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Mstaafu, Balozi Adadi Rajabu.
Pia soma:
~ Mahakama yampa Mwijaku siku 21 kuwasilisha utetezi wake katika kesi dhidi ya Kipanya
~ Masoud Kipanya amfungulia Mwijaku Kesi ya Madai ya Tsh. Bilioni 5 kwa kumtuhumu kufanya biashara haramu