Mapishi ya Kitimoto (Pork)

Mapishi ya Kitimoto (Pork)

Hahahaha, usiondoke hivivhi mkuu, japo sunna!

wee wee aaargh!unanitia dhambi afu wewe utaibeba unajua?kwani huyo nanihii ladha yake ikoje naona munamsifia kweli,oh basi siendelei kusoma huu uzi ngoja niondoke lakini muweke na picha nyingi tihi hi hi hii!
 
Wakuu, pork ni miongoni mwa nyama zinazopendwa sana hapa Tanzania, lakini maandalizi yake yanawapa tabu watu wengi na hivyo kupelekea wengi kuifuata katika Bar au sehem zingine wanazochoma kitimoto. Hata hivyo kitimoto inaweza kuandaliwa vizuri nyumbani kwa gharama ndogo tu. Kwa vile mapishi ya nyama hii yapo aina nyingi, basi ningeomba tuwe tunabadilishana ujuzi katika uzi huu. Mimi nitaanza na pishi nilipendalo, sijui linaitwaje lakini nalipenda kwa sababu nyama hailowekwi kwenye mafuta kama sehemu nyingi wanavyofanya.

Mahitaji: (Inategemea na wingi wa walaji)

-1kg pork isiyo na mafuta wala ngozi
-Chumvi kiasi
-Pilipili Manga kiasi kijiko kimoja
-Bia (beer) moja aina yoyote uipendayo, napenda Serengeti Lager kwa sababu ya radha na rangi
-Soy sauce au sause nyingine uipendayo
-Garlick ya chenga vijiko viwili

Maandalizi:
9. Ipua nyama yako kisha itie kwenye "bakuli ya aluminium foil" kama zile za take away (siyo za karatasi!)
11. Sogeza mkaa pembeni na uweke nyama hilo bakuli juu ya jiko, upande usiokuwa na moto, acha ichemkie namna hiyo na moto kidogo sana kwa muda wa saa moja.
12. Ipua nyama yako, itoe kwenye bakuli la aluminium kisha iweke juu ya jiko kwa muda wa dk kama tatu huku ukigeuza pande zote!

Mkuu katika hizo steps mimi sijakuelewa vizuri. Bakuli za alumium foil ndio zipoje hizo.
Na hayo maelezo ya step ya 11 ndio sijakuelewa kabisaaaa.
Naomba unifanunulie vzr,mana nimevutiwa na mapishi ya hii nyama.
 
Kusema ule ukweli,hii nyama imebarikiwa kwa utamu wajameni..
 
Nyama ya nguruwe ni nyama laini na yenye ladha nzuri inapopikwa vizuri, nyama hii inamapishiina tofauti tofauti na leo nawaletea mapishi ya rosti.
Mahitaji

  • Nyama ya nguruwe 1/2 kilo
  • Nyanya zilizoiva 6
  • Karoti 2
  • Pilipili hoho 1
  • Ndimu 1 kubwa
  • Chumvi kiasi
  • Mafuta vijiko 2 vikubwa
  • Vitunguu saumu 2
Matayarisho
1. Safisha nyama kisha kata kata vipande vidogo kiasi kulingana na unavyopendelea na kisha weka kwenye chombo kikavu
2. Menya vitunguu saumu na vitwange.
3. Changanya nyama yako na vitunguu saumu, kamulia ndimu na weka chumvi kiasi cha kutosha.
4. Bandika kikaango chako jikoni kisha weka mafuta kiasi kama nyama yako haina mafuta ya kutosha na yakianza kuchemka weka nyama yako.
5. Ukiwa unasubiria nyama ikauke na kuwa ya kahawia ( kumbuka kuigeuza geuza lakini usiifunikie), kwangua nyanya zako na karoti kwa kutumia grater au blender (kwangua nyanya tofauti na karoti) na kata kata pilipili hoho katika vipande vidogo vidogo.
6. Nyama ikiwa imeshabadilika rangi na kulainika vizuri weka karoti yako uliyoikwangua na koroga ichanganyike vizuri na nyama, acha iive kwa muda mfupi kisha weka na hoho zako. Vikilainika weka nyanya yako uliyoisaga na kukoroga vizuri kisha acha ichemke bila kuifunikia huku ukiwa unaigeuza geuza.
7. Ikiwa tayari epua na iandae ikiwa bado moto. Inaweza kuliwa kwa ugali, ndizi za kukaanga, viazi vya kikaanga, viazi vya kusaga n.k
Enjoy!View attachment 137740

Umenitamanisha sana yaan acha tu!!!!
 
Lunch yangu leo nimepika k/moto rost na ugali wa sembe. Ahsanteni wadau kwa kuweka hatua za mapishi ya hii nyama..
 
Mkuu katika hizo steps mimi sijakuelewa vizuri. Bakuli za alumium foil ndio zipoje hizo.
Na hayo maelezo ya step ya 11 ndio sijakuelewa kabisaaaa.
Naomba unifanunulie vzr,mana nimevutiwa na mapishi ya hii nyama.

Hizo bakuli za aluminium foil ni kama zile wanazowekea ukichukua take away.
 
Back
Top Bottom