CYBERTEQ
JF-Expert Member
- Feb 11, 2012
- 7,341
- 4,067
Wakuu, pork ni miongoni mwa nyama zinazopendwa sana hapa Tanzania, lakini maandalizi yake yanawapa tabu watu wengi na hivyo kupelekea wengi kuifuata katika Bar au sehem zingine wanazochoma kitimoto. Hata hivyo kitimoto inaweza kuandaliwa vizuri nyumbani kwa gharama ndogo tu. Kwa vile mapishi ya nyama hii yapo aina nyingi, basi ningeomba tuwe tunabadilishana ujuzi katika uzi huu. Mimi nitaanza na pishi nilipendalo, sijui linaitwaje lakini nalipenda kwa sababu nyama hailowekwi kwenye mafuta kama sehemu nyingi wanavyofanya.
Mahitaji: (Inategemea na wingi wa walaji)
-1kg pork isiyo na mafuta wala ngozi
-Chumvi kiasi
-Pilipili Manga kiasi kijiko kimoja
-Bia (beer) moja aina yoyote uipendayo, napenda Serengeti Lager kwa sababu ya radha na rangi
-Soy sauce au sause nyingine uipendayo
-Garlick ya chenga vijiko viwili
Maandalizi:
1. Kata nyama yako katika mapande kadhaa, yawe membamba kiasi.
2. Changanya pilipili manga, garlick na chumvi kwenye bakuli.
3. Nyunyiza mchanganyiko wako kwenye mapande yako ya nyama.
4. Tia nyama yako kwenye mfuko clear wa plastic kisha seal (unaweza pia kutumia plastic container inayofunga vizuri)
5. Weka nyama yako kwenye friji kwa muda wa masaa manne au uovernight ili ilainike.
6. Baada ya hapo toa nyama yako na iweke moja kwa moja juu ya jiko la kuchomea nyama lenye moto mkali
7. Geuza pande zote mpaka ianze kuiva
8. Changanya bia yako na sauce
9. Ipua nyama yako kisha itie kwenye "bakuli ya aluminium foil" kama zile za take away (siyo za karatasi!)
10. Mimina mchanganyiko wa bia na sauce juu ya nyama yako kisha funika vizuri kwa aluminium foil
11. Sogeza mkaa pembeni na uweke nyama hilo bakuli juu ya jiko, upande usiokuwa na moto, acha ichemkie namna hiyo na moto kidogo sana kwa muda wa saa moja.
12. Ipua nyama yako, itoe kwenye bakuli la aluminium kisha iweke juu ya jiko kwa muda wa dk kama tatu huku ukigeuza pande zote!
13. Tia kwenye sahani ya chakula na iache kwa dk3 hivi huku ukiiandalia mboga za majani pembeni tayari kwa kutupia na kitu cha sembe, chipsi au hata kawali mwanawani!....daaaah mate yananitoka!

Anayejua mapishi mengine atupie hapa banaa, siyo lazima kula hotel wakuu, siku zingine mnapika na watoto nyumbani!