Mapishi ya Kitimoto (Pork)

Mapishi ya Kitimoto (Pork)

Pombe yoyote ni zaidi ya uijuavyo, inaweza kuwa kiungo, inaweza kuwa dawa, inaweza kuwa kilevi na mambo kibao! Jaribu hilo pishi kaka utaniambia!
pia wakumbushe pombe ikiwekwa kwenye moto alcohol inatoka, inakuwa kama umeweka kimiminika tu, lol!
 
moyo wangu maaama!
daah!
HIII KITU BANA IWE IMECHOMWA aseee!
uuuuuuwih!
DAH!
umeileta wakti mwafakat kabisa!
WAPI GRILL !? King'asti, magauni ya offer wacha yasitutoshe tu aseee!
 
Last edited by a moderator:
mimi nafanyaga hivi
MAHITAJI:
kitimoto,
kitunguu swaum
tangawizi mbichi
kitunguu maji
hoho
karoti
chumvi
nyanya
mafuta ya kupikia kiasi
MAPISHI:
katakata kitimoto then safisha vizuri,
chemsha hadi iive ukiwa umeweka chumvi tu,
chuja maji yote,
pasha mafuta kisha weka kitimoto, kitunguu maji, kitunguu swaum na tangawizi vilivyopondwa,
kaanga hadi rangi iwe brown,
weka nyanya ulizokatakata,
koroga kisha funika hadi nyanya ziive,
malizia kwa kuweka karot na hoho na chumvi kama haikutosha. koroga kwa mda karot na hoho visiive sana kisha epua tayari kwa kula.
Huwa siweki maji then kama unapenda pilipili unaweza kuweka.
NB; lengo la kutochemsha na tangawizi na swaumu ni kwasababu ile supu haitumiki tena baadae.
Hii ni style yangu ila inakuwaga tamuuuuu hasa kwa ndizi rost mh.
 
Nenda wanakokutana na Israel. Kuna kila aina ya upishi,wewe niambie unaishi wapi nikuagizie
 
lengo la kutochemsha na tangawizi na swaumu ni kwasababu ile supu haitumiki tena baadae.
Mimi huwa naweka kwasababu inaoneza ladha vikikolea kwenye nyama. Ujanja hapa ni kuchemsha kwa maji kidogo, ukiona bado haijachemka vya kutosha na maji yameisha unaongeza kidogo kidogo mpaka uridhike alafu mwisho unaacha yakaukie. Pale unaongeza mafuta kidogo, vitunguu alafu unaendelea kama ulivyoelezea hapo juu.
 
untitled.png
 
Nyama ya nguruwe ni nyama laini na yenye ladha nzuri inapopikwa vizuri, nyama hii inamapishiina tofauti tofauti na leo nawaletea mapishi ya rosti.
Mahitaji

  • Nyama ya nguruwe 1/2 kilo
  • Nyanya zilizoiva 6
  • Karoti 2
  • Pilipili hoho 1
  • Ndimu 1 kubwa
  • Chumvi kiasi
  • Mafuta vijiko 2 vikubwa
  • Vitunguu saumu 2
Matayarisho
1. Safisha nyama kisha kata kata vipande vidogo kiasi kulingana na unavyopendelea na kisha weka kwenye chombo kikavu
2. Menya vitunguu saumu na vitwange.
3. Changanya nyama yako na vitunguu saumu, kamulia ndimu na weka chumvi kiasi cha kutosha.
4. Bandika kikaango chako jikoni kisha weka mafuta kiasi kama nyama yako haina mafuta ya kutosha na yakianza kuchemka weka nyama yako.
5. Ukiwa unasubiria nyama ikauke na kuwa ya kahawia ( kumbuka kuigeuza geuza lakini usiifunikie), kwangua nyanya zako na karoti kwa kutumia grater au blender (kwangua nyanya tofauti na karoti) na kata kata pilipili hoho katika vipande vidogo vidogo.
6. Nyama ikiwa imeshabadilika rangi na kulainika vizuri weka karoti yako uliyoikwangua na koroga ichanganyike vizuri na nyama, acha iive kwa muda mfupi kisha weka na hoho zako. Vikilainika weka nyanya yako uliyoisaga na kukoroga vizuri kisha acha ichemke bila kuifunikia huku ukiwa unaigeuza geuza.
7. Ikiwa tayari epua na iandae ikiwa bado moto. Inaweza kuliwa kwa ugali, ndizi za kukaanga, viazi vya kikaanga, viazi vya kusaga n.k
Enjoy!View attachment 137740
 
pia wakumbushe pombe ikiwekwa kwenye moto alcohol inatoka, inakuwa kama umeweka kimiminika tu, lol!

Kweli Mkuu, boiling point ya alcohol iko chini sana ikipata moto kidogo tu inaevaporate!
 
Back
Top Bottom