Mapishi ya Maboga

Mapishi ya Maboga

Rubi

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Posts
1,615
Reaction score
331
Habari zenu wapenda wa hili Jukwaa.

Naombeni mwenye kujua mapishi mbalimbali ya maboga anisaidie mie najua kuchemsha tu na maji kidogo pamoja na kutia chumvi kidogo.

Naomba mwenye kujua. p'se
 
Habari zenu wapenda wa hili Jukwaa.

Naombeni mwenye kujua mapishi mbalimbali ya maboga anisaidie mie najua kuchemsha tu na maji kidogo pamoja na kutia chumvi kidogo.

Naomba mwenye kujua. p'se

MAPISHI YA MABOGA

MAHITAJI

120 gram mbegu za alizeti au unaweza tumia mbegu za ufuta

1 Boga dogo, menya, toa mbegu na katakata vipande

1 kitunguu kikubwa kilichokatwa katwa

5 gram kitunguu thomu

1 karoti kubwa, kata kata vipande vya ukubwa kama kwenye picha

240 gram paneel cheese au unaweza tumia ( mushrooms/uyoga )

1 kijiko kikubwa cha chakula korosho za kuoka zilizokatwa katwa

1 fungu la corriender na parsley kwajili ya kupambia

5 gram chumvi

5 gram pilipili manga

Muda wa Kuandaa😀akika 30


Jinsi ya kuandaa fuatilia picha na maelezo hapa chini

chef%20issa%20maboga%202.jpg



Weka maboga katika baking pan, nyunyizia mafuta kiasi pamoja na pilipili manga

chef%20issa%20maboga%203.jpg



Roast katika oven kwa moto wa 400F(204.4C) kwa muda wa dakika 20 hadi 30 hakikisha inaiva na ukibonyeza inabonyezeka yaani laini wastani.
chef%20issa%20maboga%204.jpg



Kisha weka mafuta katika kikaango na kikishapata moto weka kitunguu, karoti na paneel cheese pamoja na chumvi na kitunguu thomu endelea kukaanga.
chef%20issa%20maboga%205.jpg


Kisha weka maboga yaliookwa kwenye oven pamoja na mbegu za ufuta au mbegu za alizeti pia unaweza tumia hata mbegu za maboga endelea kukaanga na onja kama chumvi au pilipli manga haitoshi ongezea kiasi.
chef%20issa%20maboga%206.jpg



Kisha mwagia kwa juu majani ya korrienda na parsley kuongeza ladha na kuongeza rangi katika muonekano wa chakula chako.
chef%20issa%20maboga%207.jpg



Chakula hiki ni safi sana kwa afya ya mlaji kwani hakina mafuta kabisa pia ni tajiri sana kwa virutubisho, kumbuka kumwagia kwa juu zile korosho za kuokwa kabla ya kumpatia mlaji.
chef%20issa%20maboga%208.jpg


Chakula hiki unaweza kula kama kilivyo au ukaongeza nyama, samaki, chapati au mkate na ukafurahia mlo huu wewe na familia yako.

NI RAHISI SANA KUANDAA NA HAKINA GHARAMA KABISA WAANDALIE FAMILIA YAKO CHAKULA BORA NA WEWE!

NB:usiwaze sana kuhusu baadhi ya mahitaji yako hapa kama korosho na ufuta au alizeti, vyote vinapatikana supermarket na kwenye masoko.

Wajingawatu karibu maana hiki hakina mafuta
 
ameline na Chuma Chakavu mbarikiwe naona sasa nitazidi kubadilisha mlo kwa uhodari wa mapishi.
 
Last edited by a moderator:
Boga la Sukari

Boga 3/4 kg lililokwata vipande
chumvi 1/2 tsp
sukari 3/4 cup
Hiliki iliyomenywa na kusaga 1/2 tsp
Nazi 2 glasses


Chukua maboga chemsha na kwenye maji 3 glass, yakikaribia kuiva tia sukari, hiliki na nazi yako ilichujwa. Acha ichemke tena, hakikisha kuwa kuwa yameisha usiache mpaka yakawa laini sana.

Mlo tayari
 
Boga la Sukari

Boga 3/4 kg lililokwata vipande
chumvi 1/2 tsp
sukari 3/4 cup
Hiliki iliyomenywa na kusaga 1/2 tsp
Nazi 2 glasses


Chukua maboga chemsha na kwenye maji 3 glass, yakikaribia kuiva tia sukari, hiliki na nazi yako ilichujwa. Acha ichemke tena, hakikisha kuwa kuwa yameisha usiache mpaka yakawa laini sana.

Mlo tayari[/QUOTE madame hiyo sukari vipi mbona yenye tayari huwa na sukari asilia? nitarajibu nione yanavyokuwa.
 
Last edited by a moderator:
Rubi

Boga linakuwa na sukari ya asili? usinidanganye bwana ya kijiji chetu hayawi hivyo. Anyways sisi watu wa pwani ndio tunavyokula maboga.
 
Last edited by a moderator:
Rubi

Boga linakuwa na sukari ya asili? usinidanganye bwana ya kijiji chetu hayawi hivyo. Anyways sisi watu wa pwani ndio tunavyokula maboga.
Ha Madame Basi inategemea na eneo na udongo maana ya huku nilipo ya utamutamu kama viazi vitamu au mamung'unya watu Iringa wanajua.
 
Last edited by a moderator:
Ha Madame Basi inategemea na eneo na udongo maana ya huku nilipo ya utamutamu kama viazi vitamu au mamung'unya watu Iringa wanajua.

Inaonekana nipo mawazoni mwako sana,....ila ndo fresh Rubi.
pumpkinfeatured.jpeg

Tchaooooooooooo
 
Last edited by a moderator:
Leo nimepika supu ya boga nimeiona tamu balaa asanteni kwa kunifungua macho;

nilichukua nyama ya kusaga nikaichemsha kidogo kisha, nichanganya vitunguu thomu, vitunguu maji, ndimu, chumvi nikaacha viendelee kuiva, bila kukausha supu nikakata vipande vya maboga vidogo sana ili iwe rahisi kupondaponda nikachanganya kwenye ule mchanganyiko wa nyama ya kusaga nikaacha viendelee kuiva nikaongeza na Olive oil kiasi.

vilipoiva nikaweka karoti na hoho nikavipondaponda mpaka vika uji mzito. nimefaidi kwa kweli huu mtori mtamu kuchemsha maboga sasa ni kupenda, zion daughter jaribu.

Halafu nilichogundua kwa wale wenye mgogoro wa kwenda mahudurio makubwa (constipation na gesi tumboni) wapendelee kula maboga ni mazuri.
 
unaweza pia ukapika maboga kama unavyopika mihogo au ndizi, yaani ukaunga na nazi, nyanya, vitunguu,......
kwa sababu ni rahisi sana kuiva, usichemshe kabla ya kukaanga viungo.
 
Back
Top Bottom