Mi nawaomba mnielekeze namna ya kuondoa gas katika maharage. Kipindi hiki cha mfungo napenda sana kula maharage yanawekwa sukari...nazi...hiliki yanakuwa matam sana. Tatizo yananisumbua kwa kujaza gas tumboni. Msaada tafadhali
thanks farkhina
Thanks Fakhrina. Nikiloweka asubuhu nimwage yale maji au
na nikiweka hizo recipe zote kwenye maharage bila kueka pasta ksi sawa tu?
Mi nawaomba mnielekeze namna ya kuondoa gas katika maharage. Kipindi hiki cha mfungo napenda sana kula maharage yanawekwa sukari...nazi...hiliki yanakuwa matam sana. Tatizo yananisumbua kwa kujaza gas tumboni. Msaada tafadhali
Naimani sote humu tushawahi kula hiki chakula/mboga ya maharagwe. Binafsi ni mpenzi sana wa chakula hiki, na huwa nafurahiaga sana kikipikwa vyema kwani kina ladha isiyo kifani.
Kuna sehemu nilialikwa nikakuta maharagwe matamu mno yameandaliwa, hayakuwa ya nazi, ila ladha yake ilifanana kama kuwa na tangawizi hivi.
Yaliandaliwa na chapati, siye tulikuwa tunatoweza katika chapati katika maharagwe hayo. Kuna yeyote anayefahamu kupika vyema hiki chakula aweke ufundi wake hapa.? Nahitaji niduplicate hiki kitu weekend hii.
Cc: farkhina, king'asti n.k
Maharage nayapenda sana ila hayo ya sukari ndi siyawezagi kabisaa
Kuna hii CURRIED BEANS PASTA (MCHUZI MAHARAGE PASTA)....
MAHITAJI
1)Maharage robo....
2)pasta upendazo
3)kitunguu maji 1
4)nyanya 2....
5)maziwa glass 1....
7)saumu iliyosagwa 1/2 teaspoon
8)tangawizi 1/2 teaspoon...
9)hoho kipande...
10)karot 1
11)curry powder 1 teaspoon
12)chumvi kiasi...
13)bizar ya pilau
NAMNA YA KUTAARISHA
1)Chemsha maharage hadi kuwiva bakisha maji kiasi....
2)katika sufuria nyengine chemsha pasta hafi huwiva then mwaga maji...weka pembeni
3)kaanga vitunguu vikaribia kuwa brown weka saumu na tangawizi na spicea zpye
4)weka nyanya hoho na karot na nyanya ya kopo kaanga....
5)mimina maziwa wacha ichemke iwe nzito then mimina maharage na maji ya maharagwe kiasi kutokana na wingi wa pasta ili zisiwe dry sana...
6)mimina pasta weka chumvi.....koroga kwa dakika 5 ili sizigande tayar kwa kuliwa
Nakumbuka ile siku ya mabomu mbagala nilikuwa home mama alienda kkoo shopping, nikaachiwa jiko niwapikie wadogo zangu,. Nikaanza na maharage.
Nikajaribu mapishi yangu
Nilichemsha maharage kama kawa, badae nikayaunga kwa vitunguu maji, vitunguu saumu kidogo sana na tangawizi. Nikachanganya na karoti nikakata vipande vidogo sana nikachanganya. Yalikuwa matamu sana ila ugali ndo uligoma kuiva, hadi mama akaja kuupika jion alivyorudi
Utoto shida sana
Too much requirements!!
Most of people can't affrod them or find them.
Jaribu kuwa realistic.
hizo pasta za maharage zinapatikana wapi dada hapa bongoNi requirements kwa hilo pishi.
Nipo realistic sana labda mawazo yako tu
hizo pasta za maharage zinapatikana wapi dada hapa bongo