Sahihi kabisa, kwa mtazamo wa mke, CHAKO CHENU, CHAKE CHAKE!Mkuu mwanamke si ndg Yako ni kama rafiki mmekutana nae ukubwani, usimzingatie na kujipa matarajio sana itakuumiza mbeleni, na jitahidi kujiwekea plan b ya ulinzi wa kiuchumi ambayo unaijua peke Yako tu ambapo hata ikiyumba huku unakuwa na pa kuchomokea. Mfano Mimi plan yangu ni kuhakikisha Nina trust funds ya akiba kubwa na hiyo nitaendelea kuidunduliza kimya kimya mpka uzeeni
Ukweli mchungu ni kwamba Wanaume wengi hawafi kwa ajali wala magonjwa wala vita. Wanaume wengi wanakufa kwa msongo wa mawazo, ukimya, na presha ya maisha.
Mwanaume haambiwi pole, haambiwi utashinda, haambiwi jipumzishe kwanza badala yake, kila mtu anamuangalia kama kiwanda cha miujiza – cha kutoa pesa, upendo, msaada, faraja, na subira bila kuchoka.
Anapoamka asubuhi, anawaza:
“Leo watoto wale nini, Leo watoto watatibiwa vipi, Niwapelekee nini wazazi, Kodi ya nyumba imeisha, umeme umeisha, nina kiatu kimoja nacho kimechakaa
Lakini bado atavaa tabasamu.
Ataandika "good morning" status.
Ataambia watu, “tuko vizuri tunaendelea vizuri "
Hawajui kwamba mwanaume huyu usiku analala kitandani lakini hapati usingizi, akiwaza kesho itakuwaje. Anaota ndoto ambazo hazitimii. Anavuta pumzi nzito lakini hakuna anayemsikiliza. Ataomba ushauri, atadharauliwa. Ataomba msaada, ataambiwa “we si mwanaume wa kweli, jikaze mwanaume, mwanaume ni kupambana.
Na mbaya zaidi...
Wanaume wengi wanajitahidi sana kwa wanawake ambao hata hawathamini wala kutambua mchango wao. Wanatoa kila walichonacho kwa mtu ambaye hayuko tayari hata kumshika mkono wakati anadidimia.
Mwanaume anapokata tamaa, halii. Ananyamaza. Akinyamaza – anaumia. Akiumia sana –anapata msongo wa mawazo, anaanza kufa kidogo kidogo tena anakufa kimya kimya.
Hebu leo hata kama bado mwanaume wako hajafanikiwa, msalimie mwanaume kwa upendo. Muambie unathamini sana juhudi zake na unautambua mchango wake. Mtie moyo, msaidie hata kwa neno. Usingoje afe ndio umwite “shujaa”.
Mwenyekiti nasisitiza tena, Mheshimu sana mwanaume wako, wanaume wanapitia magumu mengi sana katika maisha. Tunaelewana lakini?
View attachment 3445807
Sahihi mkuu... Imagine una mil 50 UTT AMIS, hapo stress utajitakia mwenyeweSahihi kabisa, kwa mtazamo wa mke, CHAKO CHENU, CHAKE CHAKE!
Life is not fair madume.
Mshana Jr uzoefu wangu umenionesha kuwa wanawake mungu aliwaumba kuwa na kinyongo na kisasi kisicho cha kawaida! Hicho kisasi ndicho kinaleta hayo yote. Maana hata ukimwambia kuwa hiyo nguo haikupendezi, umeshauchimba! Atakusubiri hata iwe miaka 10 hadi alipize.Preamble: For the sake of humility and a long, healthy life, ni busara ndoa zikaangaliwa kwa pande mbili. Moja as perfect intimacy na mbili as disaster against humanity. Ukipata mwenza sahihi, heaven itahamia chini ya dari lenu. Ukikosea kupata mwenza sahihi hakika kuzimu itawafurahia sana na itajidhihirisha kwenu. Msanii
Nimeipenda sana hiyo nukuu ya Msanii kwenye uzi wake kuhusu ndoa yake... Imetoa majumuisho muhimu sana katika uhalisia wake! Very short and very clear
Sasa huko ndoani kuna haya magumu/ mapito mengine nawili kwa wanaume
1. Ukipitia changamoto cha kipato ajira na kazi.. Mwenza wako anaweza kukuvumilia na kukutia moyo lakini kaa ukijua haitazidi miezi mitatu
Mwanzoni mambo yataanza kwa kificho lakini taratibu yataanza kujiinua na kujiweka wazi zaidi
Zitaanza dharau ndogondogo
Vitafuatia vijembe katikati ya utani
Yatafuatia masimango ya kificho na hatimaye ya wazi
Kisha sasa yatakuja matusi na kashfa za wazi..
Kusemwa bila kosa.. Kuvunjiwa heshima, kunyimwa unyumba, kuitwa najina mabaya nknk..!
2. Ukizeeka hali mwenza wako bado ana nguvu
Umetumia nguvu zako maishani kumhudumia na kuihudumia.. familia ukafanya kila la kumfurahisha na kumliwaza kwa uwezo wako! Sasa umezeeka.. Huna nguvu tena za kuhudumu chumbani wala sebuleni.. Mwenza uliyempenda sana na kumpa kila kitu anakuona sasa wewe ni mzigo usiye na faida tena kwake!
Anaweza kukufanyia mambo ambayo hata shetani mwenyewe akiyaona anakimbia... Wengi wamekufa mapema kutokana na hii changamoto ya pili.
Kuchapiwa
Kusimangwa
Kunyimwa vyakula vyote
Kukashfiwa
Kutohudumiwa nknk .. Ni baadhi tu ya mambo yanayoweza kukutokea uzeeni
Naomba nikatishe mada yangu na kurudia nukuu ya Msanii
For the sake of humility and a long, healthy life, ni busara ndoa zikaangaliwa kwa pande mbili. Moja as perfect intimacy na mbili as disaster against humanity. Ukipata mwenza sahihi, heaven itahamia chini ya dari lenu. Ukikosea kupata mwenza sahihi hakika kuzimu itawafurahia sana na itajidhihirisha kwenu.
Sana sana sana!Ukishakua mkubwa na ukaanza majukumu yako ya kifamilia ndio unazidi kumheshimu na kumuelewa mshua aliyekulea na kukukuza
Hapo safii!Sahihi mkuu... Imagine una mil 50 UTT AMIS, hapo stress utajitakia mwenyewe
Hatari sanaHapo safii!
Ila akijuwa valangati lake mpaka kwa mjumbe!
Aise nimeshuhudia best akiraruria na makucha home nilipowaalika bbq, jamaa alijifanya kumpitisha mke kwenye kiwanja alichomficha miaka, halafu ndio wakaja home, mwanamke baada ya kammweso ka kutosha aligeuka TIGER!
Jamaa alivaa shati jeupe, lote lilijaa damu! A scene I would never forget in my life!
Boss mimi ilitakiwa nipeleke "mahali" mwezi ulio pita niliwapa taarifa ukweni j4 kwamba j2 nakuja kutoa walicho hitajiDah Jana tu ndo nimetoka kupeleka barua ya uchumba sehemu na kitangulizi cha mahali..... (True story)
Halafu Leo post ya kwanza nakutana na hii🥺
Mpaka nafsi imekufa ganzi
Mifumo mingi ya dunia ipo Against na mwanaume.. yaani sisi tunafight wenyewe kama wenyeweMaisha ya mwanaume mara nyingi ni kama mfano wa kopo la chooni......ni agharabu sana kuthaminiwa baada ya matumizi bali wengi hutendwa vibaya baada ya kutimia kwa makusudio........
Na unyama mwingi kwenye hayo upo kwenye gereza la ndoa ambapo kwa nyakati hizi ni agharabu kumpa mwenza mwema mwenye kuhifadhi na kuweka kumbu kumbu ya fadhila vifuani mwao.........
Mwanaume unaweza kujitahidi kuyabeba majukumu kwa kadri ya uwezo wako lakini ni nadra sana kunufaika na jitihada hizo zaidi ya dhihaka, kejeli na madharau kutoka kwa wale uliotumia muda wako mwingi kuwapambania!!!
Kwa kweli dunia ni nzito kwa mwanaume.....dunia ni kambi ya mateso kwa mwanaume!!
Mungu awajaalie na kuwabariki wenza na wake wote wanaotambua, kuthamini na kuuenzi wema, mchango na juhudi za waume zao!!!!