SoC04 Mapokeo ya teknolojia kwa wananchi huathiri maendeleo

SoC04 Mapokeo ya teknolojia kwa wananchi huathiri maendeleo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Frajoo

Member
Joined
May 28, 2024
Posts
12
Reaction score
3
Akili bandia (Artificial Intelligence.)

Habari!

Kila zama kuna bunifu kubwa zinafanyika duniani ili kurahisisha maisha ya mwanadamu na mazingira yake kama siyo kutatua changamoto zinazomkabili mwanadamu. Tumeshuhudia bunifu zilizopita jinsi zilivyotusaidia ,kwa mfano Ugunduzi wa moto na zinginezo.

Kwa sasa limekuja hili la Akili bandia, japo kwa Watanzania walio wengi bado halijafahamika lakini tararibu kila mtu atalifahamu na kuweza kutumia.

Binafsi Teknolojia ninayoisubiri kwa hamu ni ile itakayoruhusu taarifa kutoka kwenye ubongo kwenda kwenye Simu janja au Kompyuta moja kwa moja ,itayoandika kilakitu kilichomo ndani ya ubongo wa binadamu ,kuhusiana na mada husika ,pia teknolojia hio itakua na huduma ya sauti ili uweze kusikia au kuhifadhi taarifa hizo.

Mtu akianza tu kufikiria jambo fulani , basi maandishi yatajiandika kwenye Kompyuta au Simu janja. Lakini mfumo huo utafeli kama mhusika atajitoa ufahamu yaani atajifanya haelewi na kugoma kuwaza taarifa sahihi, au yule mwenye mapungufu katika fahamu zake /mlevi ,kwani atayawaza yasiyofaa na maandishi yatakua ni chukizo au kikwazo kwa walio wengi. Pia teknolojia hio haitatumika kwa lengo la kumhoji mharifu au mtu asiye muungwana maana ataweza kujiwazisha uongo makusudi na kupelekea upotoshaji wa taarifa husika.

Yaani hakuna litalositirika kwenye mawazo ya mtu,yaani ni mfumo mubashara wa ubongo lakini sio kama teknolojia ya Ayo (AYO TECHNOLOGY)ambayo huonesha kilakitu kinachoendelea , hii Teknolojia itahusika na mada fulani tu.

Je una shauku ya kujua ufanyaji kazi wake?

Swadakta itakua hivi…
Wote wawili yaani mtoa na mkusanya taarifa,watavaa vifaa maalumu vya kusikilizia sauti (Headphones .) kisha mkusanya taarifa ,ataunganisha simu au Kompyuta yake na kifaa cha mtoaji kama mfumo wa Bluetooth unavyofanya kazi kwa kuingia kwenye Uwanja mahususi (Application, ambamo ataweza kuchagua lugha,kwenye orodha )kisha mkusanyaji taarifa atauliza swali ama kudodosa mada fulani au kuonesha picha fulani au kumnusisha mtoaji taarifa harufu fulani ndipo kifaa chake mtoaji taarifa kitakua na uwezo wakuhisi (Sensory Headphones )mawazo ya Ubongo wake na taarifa zitatafsiriwa kwa maandishi moja kwa moja kwenye kioo cha Simu au Kompyuta ya mkusanya taarifa.

Inashangaza sana jinsi teknolojia hio inavyofanya kazi na inasisimua mno itavyotusaidia ,maana tuna taarifa nyingi sana na hatuwezi kuzitoa zote kwasababu ya kukosa muktadha au uoga au aibu au kukosa lugha ya kuwasilisha ili kueleweka vizuri, au muda hautoshi kueleza maneno yote yaliobeba taarifa fulani.

Baadhi ya faida ya teknolojia hii ni pamoja na kupata taarifa kwa wepesi zaidi kutoka kwa wale waliowahi kufanyiwa unyanyasaji wa aina yeyote. Pia Kwenye taasisi za elimu teknolojia hii inaokoa muda wa kuandika andika kwenye makaratasi hivyo itapunguza kwa kiasi kikubwa sana ukataji miti kwa maana hiyo ni Mfumo-rafiki wa mazingira.

Je ni uvivu? Kuliko aliebuni kamari?

La hasha!…Lakini pia tutagundua hata mawazo ya wale ndugu zetu waliozaliwa na utindio wa ubongo.

Aidha teknolojia hii itatupa picha halisi jinsi watu waliozaliwa na utimamu wa akili walivyoathirika na matatizo ya afya ya akili (Mental health), tena tutagundua jinsi tatizo hili litavyozidi kuwa kubwa ulimwenguni zaidi ya Ukimwi, iwapo watu watashindwa kuyatoa mawazo yao nje ya ubongo,pia kwa kukosa taarifa zenye maarifa ya kuimarisha afya ya ubongo pamoja na kwa kukosa taarifa zenye kuchagiza hisia za furaha !Hivyo basi teknolojia hii ni kifaa tiba na msaada kwa jamii.( Psychotherapy Aid.)

Je unadhani vitapita vizazi vingapi hadi kuletwa kwa teknolojia hii?

Jambo la kushangaza teknolojia hio ipo tayari!Ndio, tunayo hata wewe unaitumia hata sasa , ila pengine kuielewa jinsi inavyofanya kazi katika mawasiliano yako inataka umakini zaidi wa kuunganisha maelezo ya ufanyaji kazi wa teknolojia hio na unayokutana nayo au kujihusisha nayo kwenye mawasiliano yako mitandaoni.

Vipi hupendi kufikirishwa?

Basi fikiria mwenyewe kama mimi kisha uyatoe nje mawazo yako ili kujiunga na mfumo huu moja kwa moja.
Falsafa yakibiblia inasema Mafanikio yapo ili tufurahi na Matatizo yapo ili tufikiri.Kwa hiyo ..kama tukiishi kwa upendo tutaguswa na matatizo ya wenzetu pia, hivyo basi “KUFIKIRI NI MCHAKATO WA LAZIMA “kwani ni sehemu ya maisha yetu yote hapa duniani.

Umeanza kupata picha fulani,hasa Ukiangalia jinsi watu wanavyofunua mapazia ya fikira zao tena mara nyingine pasi na kuulizwa!?Majibu Utayapata humuhumu kwenye mitandao ya kijamii . Jaribu kuuliza marafiki kuhusu jambo fulani, tena hata usipouliza wewe tuma picha tu utasikia yote yaliomo vichwani mwao.Au fuatilia maudhui katika mawasiliano yao utaelewa kilakitu kuhusu wao kupitia mitandao yakijamii.

Ukizingatia katika uchanya wake utagundua utashi na mawazo-bunifu kutoka kwa baadhi yao.

Hata mapokeo hasi kutoka kwa wale wanaojivika ujuzi fulani au kuaminisha umma kwamba wana uwezo fulani, pia utakutana na taarifa kutoka kwa wengine wale wasiojali lile wazo kwamba kuna kizazi kipya sasa kinahitaji kufaulu mitihani ya maadili ambayo hao,wao walifeli, na wote hao Teknolojia hio itawamulika.

Si ajabu ukatambua kuna wengine wana uwezo au vipawa fulani au mawazo mazuri lakini wanaogopa kuweka wazi , labda pengine wanaogopa wasionekane ni wajuaji ama malimbukeni ama wasiwakwaze wapendwa wao.

Teknolojia hii inakufanya uwe Mwana-huru kutoa mawazo yako, ili kuendana na kasi ya Ulimwengu katika ukuaji wa Teknoloji-mawasiliano inayochochea maendeleo katika nyanja zote yaani Kijamii, kiuchumi, kiutawala na kiutamaduni.

Je umefanikiwa kuhusishanisha nadharia ya teknolojia hii na mawasiliano yanayoendelea Ulimwenguni kote kwa sasa?

Si rahisi ,hadi utakapoanza kutafakari kwa kina ,kwa sasa acha tu iwe nilikuwa najaribu kutengeneza maudhui na kujifanya mwerevu!


Je ni wendawazimu?

Hebu jaribu kushirikisha marafiki ,watumie andiko hili uone maoni yao.

Yote kwa yote wote tutakua tumejiunga na mfumo huu moja kwa moja hata kwa wale ambao watakaa kimya , mfumo unawatambua kama nilivyosema awali .

Si ndio hio sasa teknolojia yenyewe?!Kumbe imeshawasiri aisee!Mimi nimeanza kuitumia tayari, hata wewe pia kwa namna moja au nyingine.

Shukrani.
Frank John Makumbo.
 
Upvote 1
Binafsi Teknolojia ninayoisubiri kwa hamu ni ile itakayoruhusu taarifa kutoka kwenye ubongo kwenda kwenye Simu janja au Kompyuta moja kwa moja ,itayoandika kilakitu kilichomo ndani ya ubongo wa binadamu ,kuhusiana na mada husika ,pia teknolojia hio itakua na huduma ya sauti ili uweze kusikia au kuhifadhi taarifa hizo.
Yale mambo ya neuralink e eeeh!

Yaani itafikia hatua watu watakuwa wanajitoa kopi wanakuwa na online life na real life🤯.

Je una shauku ya kujua ufanyaji kazi wake?
Ndiyo, tena sana tu.

Si ajabu ukatambua kuna wengine wana uwezo au vipawa fulani au mawazo mazuri lakini wanaogopa kuweka wazi , labda pengine wanaogopa wasionekane ni wajuaji ama malimbukeni ama wasiwakwaze wapendwa wao
Maendeleo yatapanda kwa kasi sana, maana jamii inayoshirikishana mawazo yao ndiyo inayoweza kuendelea siku zote.

Hata hii spishi yetu Homo sapiens imefanikiwa kutokana na kuwa na uwezo wa kushirikiana mawazo kwa ugunduzi wa lugja na maandishi.

Shukrani.
Frank John Makumbo
Ahsante sana👏
 
Back
Top Bottom