#COVID19 Mapokezi ya chanjo ya Covid-19 yapo hasi sana kwa Watanzania

Highest level of stupidity....

Ndo maana Matapeli kama Askofu Rasheed huwa anawageuza watu aina yenu kuwa Chuma Ulete

Na Magu akawageuza watu aina yenu kuwa Misukule ya Kisiasa...
 
Kuna watu umeshawaona au kuwasikia baada ya kuchanjwa wamekuwa wapinga kristo? bora uchanje af utulie kama haina ufanisi lakini ulijaribu. Nawaza tu.
 
Ushahidi ni mwingi mno kuonyesha chanjo ina miyeyusho
 
Highest level of stupidity....

Ndo maana Matapeli kama Askofu Rasheed huwa anawageuza watu aina yenu kuwa Chuma Ulete

Na Magu akawageuza watu aina yenu kuwa Misukule ya Kisiasa...
Mzee we kachanje mwenye highest level of intelligence, but the available evidences speaks volume, the vaccines are not safe. Watu sio wajinga kivile, magufuli hakuwa mjinga, gwajima sio mjinga, wanaokataa chanjo vile vile sio wajinga, ila una hiari kachanje wewe na familia yako ili msituambukize. Am out.
 
Hawa watu walishaaminishwa kujikinga kwa kujivukiza tangu Covid inaingia. Leo hii bila elimu ya kutosha mnawaambia kuna kinga ya sindano.
Sio waliaminishwa ni walielimishwa kutumia njia ya asili kujikinga na corona, hiyo mikemikali mnaita chanjo ndo mnataka kuwaaminisha watu kwamba ni salama lakini hakuna utafiti wowote uliofanyika na wasomi wetu wa bongo,
ila kwakuwa mzungu kasema basi wasomi wetu wote miguu juu washakubali.

Tofauti ya kuwa clever na kuwa intelligent huwa inapatikana kwenye cross road kama hizi, wasomi wa bongo wengi ni very clever
 
Kama ni alama ya mpinga kristo, angalia mkono wako wa kulia karibu na bega uone hiyo alama
 
Nina maswali ambayo nikikuuliza huna majibu..
Kwa kifupi kachanje wewe na familia yako.
 
Exactly.....huyu Gwajima pamoja na uzushi wake kuna kitu anajaribu kutoa angalizo sio mjinga hivyo....
Leo hii watu wanambeza Magufuli lakini hawana uwezo hata robo yake......kwa kifupi suala la chanjo libaki kwa mtu binafsi na familia yake...
Kila mtu apambane na hali yake.PERIOD
 
Hii sio bongo tu, na wala msimlaumu magufuli, hadi wazungu wasomi wanaikataa na wanaandamana kuipinga.
Sasa kama ww unataka, nenda tu kafanye mwenyewe
 
Ufunuo wa Yohana 13:16
Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao...
Wenye dini yao wanasemaje
 
Hivi kwanini tunafikiri kwamba wanaopinga chanjo ni wale tu ambao hawana uelewa wa kutosha na kudhani kuwa wanaokubali kuchanjwa ndio wenye uelewa?
%kubwa huku mtaani wanaopinga chanjo ukiwauliza sababu za kupinga kwao kwamba wazungu wanataka kutuua.
Nafikili hiyo ndio sababu nazani
 
CCM imegawanyika kuhusu hili lachanjo - kuna wengine bado wana msimamo wa mwendazake ambaye hakutaka hata kusikia kitu kinaitwa chanjo toka kwa mabeberu.
 
Ni muda tu utaongea,kila manzanita atajua umuhimu wa chanjo. Haya mabishano ni mwanzo tu Kabla zoezi halijaanza rasmi. Wagonjwa wa Aina yeyote watakaolazwa hospital wataomba wenyewe wachomwe chanjo hata kama hawana Corona.

Umewahi kuona mgonjwa akitafuta tiba bila mafanikio na kujikuta ametumia kila aina ya dawa. Unapokataa chanjo je una uhakika wa kutopata ugonjwa wowote maishani.kwani wanaogua ni viumbe tofauti na wengine,
 
Tatizo viongozi wetu wanarukia tu kwenye hitimisho mchanjwe ni salama.
Walitakiwa watoe elimu kwa Watanzania kujibu hoja za Mwendazake aliyesema chanjo Zina madhara,wathibitishe kwa wananchi kisayansi kuwa hazina madhara ya muda mrefu na muda mfupi.

Kwa vile Serikali hi inawapenda Sana watu wake hata imeleta chanjo za bure,iwaeleze wananchi kuwa hata madhara ya kitokea itawalipa fidia pamoja na kuwatibu bure.Maana consent form iliyotolewa Serikali inajitoa kwenye lolote litakalotokea.
Swali hili walijibu Kama chanjo ni salama kwanini ijitoe kuhusika likitokea Jambo lolote baya?

Bila kuwaelimisha wananchi viongozi wataishia kufanya usanii tu wa kuwakusanya watu wasio na kazi na kuwapa kitu kidogo na kuwajaza kwenye vituo vya chanjo kuonyesha wananchi wamejitokeza kwa wingi ili kuhadaa wazungu waliotoa chanjo.
 
Wewe ndo utueleze ukichanjwa hataweza kuambukizwa tena? Je barakoa utaacha kuvaa?je hutaweza kufa na Corona? badala ya kuja na story za mitaani.
 
Crap
 
%kubwa huku mtaani wanaopinga chanjo ukiwauliza sababu za kupinga kwao kwamba wazungu wanataka kutuua.
Nafikili hiyo ndio sababu nazani
Tatizo kiujumla imefanywa kuwa kupinga chanjo ni ukosefu wa uelewa kitu ambacho si sahihi, kila anayepinga chanjo inaonekana kapotoshwa na Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…