#COVID19 Mapokezi ya chanjo ya Covid-19 yapo hasi sana kwa Watanzania

Tulizoea mzigo unaotoka nje na kupokelewa na rais kwa bashasha ni madreamliner na mairbus. Tuliyonunua kwa pesa zetu wenyewe.

Siku zinaenda kasi sana asee! Sasa naona kuna photo-op inayohusisha viongozi wakuu wa kitaifa kupokea na kuipa promo chanjo ya msaada. Chanjo yenyewe isiyokuwa na uwezo wa kuwalinda watakaoibugia dhidi ya kirusi wao wanaita delta variant. J.&J. Vaccine May Be Less Effective Against Delta, Study Suggests

Omba Mungu akunyime vyote ila akupe utajiri wa roho na akili ya kupambanua.
 
Mama Samia naye anachoma kesho, wasiwasi wangu isije ikawa anachoma tu panadol atuaminishe kuwa kachoma chanjo sie wengine tuingie kichwa kichwa tuwe mahanithi ni mtazamo wangu tu wa kipemba yakheeee
 
Mnataka kuachia kirusi kingine nn?
 
Juzikati niliangalia taarifa ya habari TBC (Kwa bahati mbaya), alialikwa mama mmoja mtaalam wa maswala ya chanjo. Alichokiongea mle kilinisikitisha sana.
 
Hii sio bongo tu, na wala msimlaumu magufuli, hadi wazungu wasomi wanaikataa na wanaandamana kuipinga.
Sasa kama ww unataka, nenda tu kafanye mwenyewe
Ndio maana mie nauliza humu haya mawazo ya kufikiri kuwa wasiotaka chanjo ni wale wasio na uelewa wamepata wapi? kuna madaktari huko kwa wenzetu wanapinga hizi chanjo ila huku bongo ukipinga chanjo unaonekana umepumbazwa na Magufuli.
 
Mwendazake ameharibu akili za wengi hasa kwa kuzuia hoja kinzani.
 
Ndio maana mie nauliza humu haya mawazo ya kufikiri kuwa wasiotaka chanjo ni wale wasio na uelewa wamepata wapi? kuna madaktari huko kwa wenzetu wanapinga hizi chanjo ila huku bongo ukipinga chanjo unaonekana umepumbazwa na Magufuli.
They are called the CoronaBros ...They shill so hard for the vaccine....
 
β€œMamilionea wanakimbilia kuchanjwa halafu wewe mwenye balance ya zero kwenye akaunti yako umekomaa eti wanataka kukuua LOL, wakuue juu ya nini sasa? β€œ From Unknown. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ. This made my day...πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ
 
Unaweza kuweka hapa hizo unazoita "evidence speaks, the vaccines are not safe"?!

Btw, not safe in which grounds?! Kama ni side effect, suala la side effect ni jipya kwenye medical world?!

Unahoji ikiwa akina Gwajima na Magu wao ni wajinga; the answer is YES, na bora wangebaki na ujinga wao lakini wanawalisha watu huo ujinga!!

UK imechanja over 55% ya watu wake!! Unataka kusema UK Government ni wajinga kutoa chanjo isiyo salama kwa zaidi ya nusu ya watu wake?

Kwa USA, zaidi ya watu 160M wamechanjwa....


Je, unataka kusema US Government ni wapumbavu hata itoe chanjo isiyo salama kwa wananchi wake?

Ukiangalia na baadhi ya nchi zingine, mamilioni nako wamechanjwa...



Je, unataka kusema hayo mataifa ni wajinga?!

Huyo Gwajima ana maabara iliyochunguza hizo chanjo na kutoa majibu kwamba sio safe?!

Huyo JPM ni yupi kama sio yule yule ambae alifikia hata hatua ya kupiga marufuku kutolewa takwimu za COVID-19

Kama ilivyokuwa kwa JPM, Rais wa Brazil alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliokuwa wanawalisha ujinga wananchi wao, na Wabrazili walipukutika kweli kweli!

Wakati wameshakufa sana, leo hii Wabrazil wameshtuka kwa kumuona President Jair Bolsonaro anakusudia kuendesha mauaji ya kimbali dhidi ya wananchi wake kupitia corona manake

 
Zote zimepitishwa na WHO haijarishi ipi inatumika wapi,wenzetu wanatumia chanjo aina tatu mpaka nne nchi moja.Hakuna la ajabu hapo.
 
siyo tu hasi. hatutaki ujinga. wanasiasa wa nchi hii ifike mahali waheshimu maoni ya wananchi. ilipaswa wapitishe kura ya maoni kwanza kabla ya kutuletea hii chanjo.

yaani huyu Samia anajikuta ni mama yetu wa kutuzaa anaenda kwa mabeberu kutununulia chanjo? pathetic!
 



exposure inaendeleaje uko mkuu
 
Mi sina muda wa kujaza ma evidence hapa, mi si mjinga, najua chanjo hiyo ina matatizo makubwa virologist kibao with impeccable credentials wameongea against covid vaccination. Again, me and my friends and family hatutachanjwa, kachanjwe wewe.
 
balance yake ipo kama frequency za redio
 

 
Alisemaje?
Alisema chanjo kama chanjo, mtafiti anapopewa kibali kwa ajili ya kufanyia utafiti chanjo kwanza anaanza na kikundi kidogo si chini ya watu 50 ambapo anafanyia utafiti wake kwa muda usiopungua miaka 2, baada ya hapo anaidhinishwa kufanya utafiti kwa idadi kubwa zaidi ya wwtu, ambapo atafanya utafiti wake kwa muda usiozidi miaka 2 lakini pia unaweza kuwa mwaka na kuendelea, kwa maana hiyo kila hatua ya kundi la watu kuna muda, mpaka chanjo kuja kuthibitishwa inakuwa utafiti umechukua si chini ya miaka 5 hadi 10, hivyo kila stage chanjo inapofanyiwa utafiti kuna uthibitisho wa ufanyaji kazi ndani ya muda wa utafiti.
Ukiangalia kwa makini utagundua tangu Covid ianze na muda chanjo imetoka ni chini ya muda wa utafiti, je utafiti wake umefanyika kwa muda gani.
 
 
ni kweli tunashangaa, tulitegemea mapokezi yawe kama yale ya Dreamliner... sijui kwa nini sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…