kinje ketile
JF-Expert Member
- Dec 12, 2015
- 5,089
- 9,664
Nimekuwa shuhuda siku ya leo majira ya alasiri wakati timu ya Platinum kutoka Zimbabwe ikipokelewa uwanja wa ndege JNIA.Ukweli zile mbwembwe na amsha amsha kutoka kwa wenzetu 'Wananchi' kwenye mapokezi hasa za timu za nje zinapokuja kupambana na 'mnyama' sikuziona.Jambo hili haliwezi kupita hivi hivi bila kupongezwa na limeonyesha dalili za wazi kabisa kuwa wananchi sasa wangependa wazimbabwe WAFE pale kwa Mkapa.
Zipo sababu za wazi kabisa kwa wananchi kuonyesha uzalendo. Mojawapo iwapo FC Platinum akitolewa stage hii Simba itaingia hatua ya Makundi na pia iwapo Namungo atapenya automatically Tanzania itarejesha zile nafasi 4 michuano ya CAF ijayo. Maana yake nini? Wananchi hata wasipochukua Ubingwa wa VPL jambo ambalo lina uwezekano mkubwa kutokea bado watajihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa. Kwa hili,Kongole kwao 'Wananchi'.