Mapokezi Ya FC Platinum: Hatimaye 'Wananchi' Waonyesha Uzalendo...!!!

'Wananchi' kwenye mapokezi hasa za timu za nje zinapokuja kupambana na 'mnyama' sikuziona.Jambo hili haliwezi kupita hivi hivi bila kupongezwa
Walipenda wawapokee, ila wamesutwa na yale madongo ya akina Edo Kumwembe na Shaffih Dauda kuwa kuwapokea wageni ni ushamba na dalili za ukosefu wa ajira
 
Walipenda wawapokee, ila wamesutwa na yale madongo ya akina Edo Kumwembe na Shaffih Dauda kuwa kuwapokea wageni ni ushamba na dalili za ukosefu wa ajira
Hapa ni pa kuweka mkazo 'KUWAPOKEA WAGENI NI USHAMBA NA DALILI ZA UKOSEFU WA AJIRA' ......!
 
Hivi wakati ule wa kuwapokea Plateau ni kweli waliwaibia simu au yalikuwa maneno tu ya watani wa jadi kutaniana? Kama ni kweli Plateau waliibiwa simu basi safari hii watakuwa wameogopa kwenda kwani inawezekana na vibaka wajkjichanganya humo humo kati yao halafu kashfa zikaenda kwao. All in all ni mwanzo mzuri wa kujitambua.
 
Jamaa kajikaza haoni hata noma, mtamaliza ligi bila ya kufungwa ila kombe watabeba simba. Sijui km ishawahi kutokea. Itakuwa historia ya ulimwengu pia

Ishatokea Mara nyingi tu, Mwaka 1977/78 Perugia ya Italia ilimaliza Series A unbeaten lakini ikawa ya Pili.

Huo ni mfano mmoja IPO mingi
 
Kwa wanaomuelewa mheshimiwa Rais,alichukizwa na kitendo cha watu fulani kwenda kuwapokea wageni na kuwashangilia.Ndio maana alitamani hivi vilabu viwili vife kabisa.
 
ile droo na prisons imewanyong'onyesha. wanawaza simba akishinda viporo vyote anaongoza league kwa magoli
 
Bado wanakumbuka aibu waliyoipata kwa Plateau, unadhani wao wajinga waendelee kuabika na mijezi yao. Jana tuu wameopolewa kwenye tope na Jamburi
 
Washajua kitakacho tokea wazimbabwe watakufa nne bila shikeni maneno yangu...
OyaaaπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ..
Umetisha mkuu.
Au wewe ndo yule mganga alokamatwa jana nni.
 
Hawana cha uzalendo hao, walishajua matokeo. Somo kutoka kwa Plateau lilishawaingia.
 
Dah...nikikumbuka ile amsha amsha siku wale wanigeria Plateau wanapokewa pale JNIA....Hakika waswahili hawakukosea waliposema 'Hasidi Hana Sababu' ..... !
Wakati wa Plateau, 'wananchi' walikuwa "provocked"! Huwezi kutumia maneno yale na bado ukahitaji kuungwa mkono na mtani wako! Utani wetu uwe kwenye mechi za ndani, tukienda nje tuwe wamoja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…