Mapokezi ya Nyerere huko Uingereza

Unajua, nchi za magharibi zina watu wanaoangalia mambo kwa mtazamo mpana.

Ukiangalia hotuba yake , alivyomaliza ukumbi wote ulisimama kwa round applause.

Yaani hata wasiokubaliana naye wanakubali anajenga hoja na wanajifunza.

Hivyo, alipokuwa anawasema si kuwa aliwasumanga bali aliwaonyesha the other side of the coin

Akiongelea human diginity, hii ni matra kwa nchi za magharibi, sasa Mwalimu alikuwa anawaeleza ' they should walk the talk' hapo ndipo alipokuwa anawapata.

Kwamba kama diginity ni suala muhimu sana, vipi ubaguzi kama ule wa Afrika kusini

Ziara nzima imenigusa kwasababu ilikuwa ya ki-Rais hasa.

Hata kama ningelikuwa UK wakati huo, ningejitokeza na bendera yangu licha ya ufukara, uchanga na udhaifu wa taifa letu miaka hiyo.

Ningejivunia sana kuwa na kiongozi anayeonyesha dunia' it's matter of time' tutakuwa wazuri tu.

Nadhani hapo ndipo wengi walipo focus kuwa taifa hili kama lina kiongozi wa namna hii lina bright future

Siku hizi hata kujitambulisha tunaona aibu maana hakuna tunachojivunia zaidi ya kupitisha bakuli na kulia lilia miaka 50 baada ya uhuru.

Ukiangalia video utaona tofauti ya Tanzania tuliyoifikiria na Tanzania tuliyo nayo! so sad
 

Je ulifaidika nini na ziara za Nyerere nje? Investments katika kipindi chake zilikuwa zinapungua kila mwaka na misaada ya kujikimu iliongeza.
 
Kimweri,

..intelect.

..eloquence.

..passion.

..hayo mambo ma-3 ndiyo yanayomtofautisha Mwalimu na waliomfuatia.

..katika kizazi cha sasa yuko kiongozi mmoja anaweza kumfikia Mwalimu but he needs more "polishing."
 
Last edited by a moderator:
Though sikupata bahati ya kuishi katika uongozi wake na hata alipofariki nilikuwa mdogo sana ila kupitia vitabu, makala mbalimbali na maoni ya watu mbalimbali waliokuwa katika uongozi wake na waliofanya naye kazi baba wa taifa hakuwa corrupt leader, alikuwa mkweli na hata kama kuna sehemu alisema uongo basi ni sehemu chache sana katika maisha yake ukilinganisha na ukweli aliousema katika uhai wake. Aliwapenda kwa dhati wale aliowaongoza, Aliishi kwa mujibu wa itikadi alizoziamini bila kujali zitawapendeza watu au la aliishi ukweli alioumini na aliishika sana imani yake hakuwahi kuyumbishwa, hakuwahi kutetereka hata kidogo na hata alipoona wengi hawapo tayari kuwa pamoja katika imani yake aliweza kuwaachia nafasi ili watu waishi kile walicho kiamini huku yeye akiwa pembeni na imani yake, Mtu mwenye tabia hii uheshimika sana bila ya kujali anatenda mema au mabaya mfano mzuri ni Adolf Hitler, Mugabe pamoja na kuwa na misimamo ambayo imeumiza watu wao lakini bado wanaheshimika sana tu. Na unyonge wetu huu na umaskini wetu viongozi wetu wataweza kupata heshima hii kama kwanza hawatakuwa corrupt, wawe wakweli, wenye umoja na wananchi wao na wenye kuishi imani zao sio unafiki kiongozi akiamini nyeupe ni nyeupe, na akasema nyeupe ni nyeupe, akaishi kwa kumaanisha nyeupe ni nyeupe hata aende wapi hatodharaulika katu.
 
Thanks NN! This is how we should be proud on our leaders , president with presidsntial all the the manners and materials .
 
Kimweri,

..intelect.

..eloquence.

..passion.

..hayo mambo ma-3 ndiyo yanayomtofautisha Mwalimu na waliomfuatia.

..katika kizazi cha sasa yuko kiongozi mmoja anaweza kumfikia Mwalimu but he needs more "polishing."

Kiongozi gani huyo?
 
Kimweri,

..intelect.

..eloquence.

..passion.

..hayo mambo ma-3 ndiyo yanayomtofautisha Mwalimu na waliomfuatia.

..katika kizazi cha sasa yuko kiongozi mmoja anaweza kumfikia Mwalimu but he needs more "polishing."

Jokakuu;

Lakini hizo sio characteristics of an effective leader. Hizo ni za poet.
 

Nyerere anaweza kutoka nje ya nchi mara moja au mbili kwa mwaka.
Alikuwa anajua kile anachokifanya iwe kwa kusoma au kuandika.
Nadhani Nyerere alikuwa kiongozi pekee wa tanzania aliekuwa anajitambua kifikra ndio maana misimamo yake hasa congress na house of commons walikuwa wanaitambua na kuiheshimu.
 

Na ziara moja ni lazime ilikuwa ya kwenda China.
 

Kitengo kilitakiwa kiweke mizani yakumpima rais kwa standards za Nyerere.
 
Jamani mambo yamebadilika sana siku hizi. Miaka ya zamani kumuona rais mweusi ilikuwa big dili.

Hivi kwanini Nyerere hakutengeneza Nyerere wengine wa miaka 50 ijayo?
Sasa Tanzania tunasumbuka na marais wa ajabu sana.
 
Hivi kwanini Nyerere hakutengeneza Nyerere wengine wa miaka 50 ijayo?
Sasa Tanzania tunasumbuka na marais wa ajabu sana.

Alianzisha taasisi za kuendeleza siasa zake. Mojawapo ni chuo cha chama cha Kivukoni. JK ni mmoja wa wahitimu kama sitakosea.

Tatizo ni kuwa siasa zake na hazilipi. Na mabadiliko ya kisiasa duniani yalipotokea, wale waliokuwa kwenye siasa hawakuwa na profession yoyote ya ku-survive nje ya siasa. Hivyo wamebaki kuwa mafisadi, case in point Lowassa, JK etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…