Mapolisi msiikumbatie CCM, fuateni sheria na weledi mliofundishwa -Wananchi watawaelewa hata mkifukuzwa kazi

Mapolisi msiikumbatie CCM, fuateni sheria na weledi mliofundishwa -Wananchi watawaelewa hata mkifukuzwa kazi

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Polisi muache kujipitisha kwa kuikumbatia CCM hata mnafika kuvunja sheria ,mkae mkijua kikinuka Miccm haitawasaidia kitu na watakaa mbali sana na nyinyi,mnamuona Sabaya? Mnawaona wale mapolisi ambao miezi michache walitesa watu kule Zanzibar na kuwagaragaza ,waliokuwa wakilindwa (CCM) wote wamesema sheria ifuate mkondo wake maana hawakuwatuma mapolisi kutenda udhalimu.

Basi hivyo ndivyo inavyokuwa ni bora ufukuzwe kazi kwa kutotenda uovu unaotumwa kuwashughulikia wapinzani,CCM wanawakaanga kwa mafuta yenu wenyewe mkiunguwa wanaruka mita mia, wananchi watawaelewa na kuwa pamoja nanyi kwani mmekataa kutenda uovu ili kuwalinda wachache waliopo madarakani.

Tanzania inahitaji mabadiliko na moja ya mabadiliko ni kwa nyinyi mapolisi na vyombo vyote vya ulinzi na usalama kujielewa na kujitathmini na kuwa wa mwanzo kubadilika msingojee mabadiliko kuwakuta ikiwa bado mnatesa raia.
 
Usituingilie tutapandishwa vyeo na mawe juu.

Jiulize RPC kamuhanda ilikuwaje baada ya tukio la Mwangosi
 
Una matumaini kuwa watakuelewa kwa wito huu sasa?

Hatuna cha kuwafanya hawa wakalazimika kufuata sheria wanataka au hawataki?

Tunasubiria utashi na hisani zao?

Ndiyo hivyo?
 
Ulimwenguni huko wengi waliichoka na kuwacha kuikumbatia serikali ,naamini kuna siku watawaelewa wananchi ,juzi amekuja mmoja kuniomba chunvi na kiberiti. akasema mama (Maisha magumu)
 
Katiba imetoa mamlaka kwa serikali kuunda chombo vya Dola kwahiyo unataka Polisi wapingane na aliyemuunda?

Hivi Polisi wasipowazuia wanaotaka kufanya fujo matokeo yake itakuwa nini? hata kama nia ni kutaka nchi isitawalike haiwezekani kuwaacha wahuni wafanye kila wanalolitaka.

Naungana na Polisi Sheria iliyopo inawaruhusu kufanya hivyo msikubali kuingiliwa au kupangiwa na makundi ya watu wachache wenye nia mbaya kwa manufaa Yao binafsi sisi wananchi hatujawatuma hao.
 
Usiwastue ujue wanatusaidia kuisagia kunguni CCM na Serikali yake, Wenyewe kwa akili zao za kushikiwa wanaona wanaisaidia CCM.
 
Back
Top Bottom