Mapungufu haya yafanyiwe Kazi ili Simba SC ya Msimu ujao iwe Moto na tusizoeleke kuishia Robo Fainali CAFCL

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mapungufu haya yafanyiwe Kazi ili Simba SC ya Msimu ujao iwe Moto na tusizoeleke kuishia Robo Fainali CAFCC

1. Kocha Robertino asiwe Mzito au Muoga kufanya Sub kama anavyoonekana na alivyofanya Jana na Kutugharimu.

2. Kuwe na Zoezi maalum la Kupiga Penati mara kwa mara katika Uwanja wa Mazoezi.

3. Usajili Kabambe ufanywe kwa Nafasi za Beki wa Kati, Kiungo halisi wa Ukabaji, Kiungo Mchezeshaji na Mshambuliaji hatari.

4. Timu iwe ( iajiri ) Mtaalam wa Saikolojia kwani kuna nyakati unawaona Wachezaji wa Simba SC wameathirika na Tukio / Hali fulani inayowatoa Mchezoni upesi.

5. Wachezaji wa Simba SC waambie Simba SC Kwanza na Umaarufu wao baadae.

6. Klabu iwe na Utaratibu wa Kucheza Mechi za Kirafiki na Vilabu Vikubwa mno Barani Afrika ili Kujiimarisha zaidi.

7. Klabu iwe na Chief of Scout wa Kuvaa Viatu vizuri vya Marehemu Zakaria Hanspoppe ( Mapama ) ambaye atakuwa anatuletea Wachezaji wa Kucheza na siyo Wachezaji wa Majaribio na wa 10% ambao Wanatugharimu.
 
Kiungo mchekeshaji basi simba ndo itakua timu ya kwanza duniani kuwa na kiungo mchekeshaji.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Kiungo anaye wapa raha...

Kiungo fundi...

Sio kiungo wa asilimia 10...

Uki ambiwa kiungo Mkata umeme unaelewa nini? Kiungo shoka?
 
Kiungo mkata umeme ni kaliba ya Gersoni Fraga au Mzamiru Yassin wao kazi zao ni kuharibu mipango ya mpinzani tu kwa Simba Mzamiru amefanya vizuri sana Ila kwa sasa umri umemtupa mkono benchi la ufundi la Simba linatakiwa lianze kuandaa mrithi wa nafasi ya mzamiru mapema iwezekanavyo.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Kiungo mkata umeme ni kaliba ya Gersoni Fraga au Mzamiru Yassin wao kazi zao ni kuharibu mipango ya mpinzani tu kwa Simba Mzamiru amefanya vizuri sana Ila kwa sasa umri umemtupa mkono benchi la ufundi la Simba linatakiwa lianze kuandaa mrithi wa nafasi ya mzamiru mapema iwezekanavyo.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Je kiungo mchekeshaji/mchezeshaji?
 
Kwenye sub kocha hana makosa kwa sababu walioko nje asilimia kubwa hawana uwezo kuwazidi walioko ndani with respect to the game demand.

Hii inakupa tafsiri kwamba hatuna kikosi kipana
Napingana na wewe asilimia 100. Huwezi kusema kwenye sub kocha hana makosa nafasi ya saidoo ilimuhitaji zaidi sakho kwakua ntibanzokinza alishindwa kabisa kufanya mikimbio ambayo ingeweza kuleta madhara kwa mpinzani, aina ya uchezaji ya sakho ingemfavour zaid kwakua anauwezo mzuri wa kudrible mpira na kusababisha hatari karibu na lango la mpinzani kitu ambacho simba walikikosa kwa saidoo.

Pia phiri alikua na nafasi kubwa sana ya kuingia katika ule mchezo kama winger wa kushoto kutokana na aina ya uchezaji wake. Kama kigezo ingekua ni match fitness basi ni sahihi ila kama kigezo ni asingeweza kuleta matokeo uanjani nakataa.

Ubora wa Wyidad kwa misimu ya hivi karibuni umeporomoka ukilinganisha na misimu kadhaa nyuma. Hivyo simba walihitaji kupunguza temple ya mchezo na kufanya mashambulizi ya kasi kuelekea gorini. Kama utagundua simba waliogopa kabisa kupiga direct corner wakihofia counter attack lakini endapo wangerisk baadhi ya nafasi huenda wangeweza kuondoka na gori mbili ugenini.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Simba yahitaji fumuliwa haswa ila kocha abaki

Nyoni
Mkude
Mwenda
*Onyango
*Phiri
*Chama
Banda
Okwa
Okrah
Akpan
Outtara
Bocco
Sawadogo

Kwa kuangalia tu kwa ufupi timu yahitaji mabadiliko mengi

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Je kiungo mchekeshaji/mchezeshaji?
Kiungo mchezeshaji kazi yake ni kutengeneza nafasi kwa mshambuliaji kuweza kuleta madhara katika lango la mpinzani. Lakini pia kwa asilimia kubwa kiungo mchezeshaji ndio huamua mchezo uwe wa aina gani pindi awapo uanjani. Ikitokea kiungo mchezeshaji hayupo katika ubora basi itakua ngumu kwa timu husika kupata matokeo mazuri.

Kiungo mchezeshaji anatakiwa angalau awe na uwezo wa kupunguza wachezaji kuanzia wawili na kuendelea kwani endapo atafanikiwa kua na uwezo huo basi itakua rajisi kwake kuwalisha mipira washambuliaji au mawinger wanaotokea pembeni na kutengeneza madhara. Kwangu Mimi aina ya wachezaji hawa ni kama vile Feisal salum cloutas Chama japo kwa Tanzania inaonekana tuna viungo wakabiaji wengi ila tunaupungufu mkubwa wa viungo wachezeshaji.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Simba yahitaji fumuliwa haswa ila kocha abaki

Nyoni
Mkude
Mwenda
*Onyango
*Phiri
*Chama
Banda
Okwa
Okrah
Akpan
Outtara
Bocco
Sawadogo

Kwa kuangalia tu kwa ufupi timu yahitaji mabadiliko mengi

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Ndugu upo sahihi kwa hao uliowaorodhesha lakini kumbuka kila mchezaji hufit kulingana na maelekezo ya mwalimu au pengine hali ya majeraha. Kwa mtazamo wangu Sawadogo namtazama Kama mchezaji mzuri japo changamoto kubwa kwake anakosa speed kwa uchezaji wa sawadogo hautofautiani kabisa na uchezaji wa Khalid aucho tofauti ni kwamba wachezaji wa yanga wanakasi sana ndio maana Aucho anaonekana kua bora niamini Mimi sawadogo akiwekwa katika kikosi cha yanga huenda akaperform vizuri. Ila hao wengine wameshakua malegend wa simba ni muda wao sasa wa kuangalia maisha mengine ila ningekua kocha banda na phiri ningewabakisha.

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Mapungufu haya yafanyiwe Kazi ili Simba SC ya Msimu ujao iwe Moto na tusizoeleke kuishia Robo Fainali CAFCC

1. Kocha Robertino asiwe Mzito au Muoga kufanya Sub kama anavyoonekana na alivyofanya Jana na Kutugharimu.

2. Kuwe na Zoezi maalum la Kupiga Penati mara kwa mara katika Uwanja wa Mazoezi.

3. Usajili Kabambe ufanywe kwa Nafasi za Beki wa Kati, Kiungo halisi wa Ukabaji, Kiungo Mchekeshaji na Mshambuliaji hatari.

4. Timu iwe ( iajiri ) Mtaalam wa Saikolojia kwani kuna nyakati unawaona Wachezaji wa Simba SC wameathirika na Tukio / Hali fulani inayowatoa Mchezoni upesi.

5. Wachezaji wa Simba SC waambie Simba SC Kwanza na Umaarufu wao baadae.

6. Klabu iwe na Utaratibu wa Kucheza Mechi za Kirafiki na Vilabu Vikubwa mno Barani Afrika ili Kujiimarisha zaidi.

7. Klabu iwe na Chief of Scout wa Kuvaa Viatu vizuri vya Marehemu Zakaria Hanspoppe ( Mapama ) ambaye atakuwa anatuletea Wachezaji wa Kucheza na siyo Wachezaji wa Majaribio na wa 10% ambao Wanatugharimu.
Namba moja hapo, kuwa mzito wa kufanya Sub unatokana na waliko sub hawana quality huenda hawafit kwenye mipango yake na yeye hapendi kubet
 
Kiungo mchekeshaji basi simba ndo itakua timu ya kwanza duniani kuwa na kiungo mchekeshaji.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Ukikazwa pia huwa unakuwa na Umakini hivi hivi wa kugundua Makosa ya Mkazaji?
 
Mapungufu haya yafanyiwe Kazi ili Simba SC ya Msimu ujao iwe Moto na tusizoeleke kuishia Robo Fainali CAFCC

1. Kocha Robertino asiwe Mzito au Muoga kufanya Sub kama anavyoonekana na alivyofanya Jana na Kutugharimu.

2. Kuwe na Zoezi maalum la Kupiga Penati mara kwa mara katika Uwanja wa Mazoezi.

3. Usajili Kabambe ufanywe kwa Nafasi za Beki wa Kati, Kiungo halisi wa Ukabaji, Kiungo Mchezeshaji na Mshambuliaji hatari.

4. Timu iwe ( iajiri ) Mtaalam wa Saikolojia kwani kuna nyakati unawaona Wachezaji wa Simba SC wameathirika na Tukio / Hali fulani inayowatoa Mchezoni upesi.

5. Wachezaji wa Simba SC waambie Simba SC Kwanza na Umaarufu wao baadae.

6. Klabu iwe na Utaratibu wa Kucheza Mechi za Kirafiki na Vilabu Vikubwa mno Barani Afrika ili Kujiimarisha zaidi.

7. Klabu iwe na Chief of Scout wa Kuvaa Viatu vizuri vya Marehemu Zakaria Hanspoppe ( Mapama ) ambaye atakuwa anatuletea Wachezaji wa Kucheza na siyo Wachezaji wa Majaribio na wa 10% ambao Wanatugharimu.
Jana kwa mfano mchezaji Gani aliwagharimu?
 
Back
Top Bottom