KERO Mapungufu ya mfumo wa kusajiri wajasiriamali wadogo wadogo

KERO Mapungufu ya mfumo wa kusajiri wajasiriamali wadogo wadogo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
6,607
Reaction score
8,381
Jana nilienda ofisi ya kata kukutana na afisa maendeleo. Lengo langu ni kuingizwa kwenye mfumo wa wajasiriamali wadogo wadogo ili niweze kupata kitambulisho ambacho baada ya kusajiliwa unalipia 20,000 kila baada ya miaka mitatu.

Cha kushangaza ni kwamba inatakiwa niende kusajiliwa nilipojiandikishia kitambulisho cha taifa (NIDA)

Maswali yangu kwa waendesha hii program ya kusajili wajasiliamali wadogo wadogo
1. Kuna mipaka ya mtanzania kufanyaz shughuri za maendeleo ndani ya nchi yake?

2. Hamfahamu kuwa watu wanahama usiku na mchana na huko wahamiako wanakuna na firsa za kufanya ujasiriamali?

3. Hamuoni mnaikosesha serikali mapato kwa kigezo cha kusajiliwa ulipojiandikishia?

MAPENDEKEZO
Kwakua mfumo wa (NIDA) ndio unaotumika, hakuna haja ya kusajiliwa nilipojiandikishia kwasababu taarifa zipo kwenye mfumo mmoja
 
Back
Top Bottom