Mapungufu yaliyopo kwenye video ya Ally kiba (Mwana Dsm)


Mkuu tupo pamoja wacheni kwanza kila kitu kitakuwa poa, ni holiday season ni wakati wa bataz mpaka kuku waone gere.

Baada ya christmas tunadondosha thread la kufa mtu likiwa na TBS zote ni total package. Issue yote iko kwa uongozi na haki isipotendeka JF si baba wala mama yangu nitatoa msimamo wangu.
 
Nimemwambia nifah asikujibu ulichouliza.
Ova
basi sawa, nahisi jana humu ndani ilikuwa pata shika, ila kama zile threads zimefungwa, lets go for good kwani hazikuwa za kujenga, binafsi nilishaacha kuingia huko na ndio maana nimepitwa na yaliyotokea, ila ombi langu kwa wana JF wenzangu, kama kuna mwenye wazo la kuanzisha uzi wa kuwajadili hawa watu, asianzishe uzi wa kichonganishi, aanzishe wa kuwapatanisha mashabiki wa hawa wasanii wawili kiba na mondi, then wahusika watapatana automatic kwa influence zetu.
 
Last edited by a moderator:
Nimemwambia nifah asikujibu ulichouliza.
Ova

acha ujinga mkuu, dont take these matters too personal, tumekuja share feelings hapa.
Sasa tabia gani hzo, eti mtu asimjibu mwenzie.

Kuwa critical thnker, unafkiri kwenu hapa. Mambo ya ki primary hayo.
 
Last edited by a moderator:
Mleta uzi una elimu ya upagaji picha na uongozaji picha mtembeo, mpaka utoe "hukumu" kwa video ya Mwana?

nimeitazama video hiyo zaidi ya mara tatu na hivi ndio nivyoviona;

1. abstract story - katika sanaa kuna kitu kinaitwa "abstract" ambapo huoni maana au ujumbe moja kwa moja mfano kama unatembelea maonesho ya sanaa za uchoraji, ukitazama abstract paint kama huna elimu ya sanaa hiyo huwezi jua maana.
nirudi kwenye "video ya Mwana abstract meaning"... hadithi ni juu ya maisha ya kila siku ya guru/mfalme wa jukwaa/mwanamuziki ambaye kila akiamka huongea na "the man on mirror" kama sehemu ya kujiuliza alipotoka na anapokwenda. Philosophy inatu-encourage tujiulize maswali kila siku kama sehemu ya kufahamu muelekeo wetu sahihi juu ya yale yanayotukabili. kuongea peke yako katika kioo ni moja ya semhemu ya kujipa "confidence".

mfalme/guru huyu mbali na umaarufu wake anatembea kwa miguu na yuko "free from stresses" anajiamini kile anachofanya na wala hajali nani atasema nini juu yake "anacheza muziki barabarani"

Anajua kazi yake viivyo na anaongoza kwa mifano "anakuta dancers wanabishana anawafundisha kucheza hiyo choreography vizuri na wanafurahi kuelekezwa". Mfalme/guru huvishwa na hilo tunaona mrembo akimvisha Kiba.
scene za mwisho mostly ni kuonesha au kutoa hitimisho kuwa huyu mtu ni mfalme au guru wa wawapi? tunaona performance na audience wakimshangilia kwa kile anachefanya sahihi, inaonekana huyu ni mtu maarufu hapa na anafanya kazi yake vyema.
Cutaways za kiti ni ishara ya utukufu/mafanikio/where he belongs. kusimama juu ya kitu kirefu inamaanisha "he is on top of the World" he is above everything in his sphere/World/career/game.

2. KISS (Keep it Simple and Short) Writers, Directors, DoP, n.k katika industry ya film wanaamini kuwa unapofanya sanaa simple and short watu wengi wanaelewa na inapendwa. mfano, kwa nini filamu ya 12 years a slave ilfanya vizuri katika tuzo za Oscar kuliko Wolf of Wall Street? mwaka huu Maleficent ya Angelina Jolie na A Milion Ways to Die in the West hazipo hata kwenye orodha ya tuzo za Golden Globe zitakazofanyika January 2015 na hizi ni block buster films hadithi ya kawaida kabisa katika film kama Selma au Grand Budapest Hotel zinafanya poa. siri ni moja tu hadithi nzuri ambayo kila mtu anaielewa ndio hadithi inayofanya vizuri. Video ya mwana Hadithi yake imekaa vizuri kwa kua ni rahisi kueleweka na ni maisha ya kila siku.

3 Kwa nini haonekani huyo mwana aliyeimbwa? swali linaloumiza akili za wengi, jibu ni rahisi kuwa Ali Kiba ametaka kuonesha umahiri wake, kuwa yeye ni nani kwenye muziki hivyo ameamua kuonesha zaidi kuwa "mfalme amerudi" pale anapotakiwa kurudi ndio sababu kuu ya kutumia "abstract" meaning zaidi. so, relaxxx filming imepiga hatua sio neno kwa picha ila ni beauty/aesthetics na meaning!!!

4. binafsi nimeridhika na upigaji picha, matumizi ya taa, lenses na hata filters. DoP amefanya kazi yake, Director amefanya majukumu yake, wadrobe dept + Hair & make-up dept wamefanya majukumu yao.

video inanifanya mimi kama mtazamaji nivutiwe kuiangalia mara kwa mara, kwa kuwa hadithi yake ni maisha yangu ya kila siku hata kama sijui kinachoimbwa.

Akhsante kwa leo, ila Director wa video za Diamond Platnumz ni mzuri pia na anajua anachofanya. kabla ya ku-judge ni vyema tukajifunza taaluma zenyewe.

REFERENCES:
Cinematography Theory and Practice (SECOND EDITION) - Blain Brown; Focal Press (2012)
Filming the Fantastic - Mark Sawick; Elsevier Inc. (2007)
 
Haya atayafanyia kazi ila video nzuri mumuache ally jaman khaaaa
 
Yale mahedifoni kutembea nayo na kujichezesha....
 
mwanaapolo ametoa elimu kubwa sana hapa tena bure. Nakuheshimu sana. Tunahitaji watu wa namna yako ili kufanya watu wakija JF wawe wamepata kikubwa cha kujifunza. Hongera sana, kama hawatajifunza hapa basi hawatajifunza tena. Watu hawataki kutambua aina za music videos.
nifah unakumbuka kitu nilikueleza PM? Jamaa ameandika toka ndani ya moyo wangu, cha kuongeza mimi nilitaka kuweka screen capture ya kila scene aliyoielezea, ambazo jana nilikuwa nazicapture na kuziweka kwenye thread ya Kiba pale. Jamaa kanikosha sana.
Ova
 

Niliona nikataka nikuite sijui nimesahau vipi.Jamaa katisha kweli yani.
 
Akhsante kwa ku-value mchango wangu. Nilijifunza hivi vitu kidogo na sipendi kuona hii fani inachukuliwa poa poa. niamini film ni moja kati ya kazi ngumu hivyo critism zisizokuwa na maana ni vyema tukazirekebisha.
 
Akhsante kwa ku-value mchango wangu. Nilijifunza hivi vitu kidogo na sipendi kuona hii fani inachukuliwa poa poa. niamini film ni moja kati ya kazi ngumu hivyo critism zisizokuwa na maana ni vyema tukazirekebisha.

Kufanya film/video ni taaluma, ndio haiko kwenye Basata, iko kwenye bodi iliyo chini ya Wizara, ambayo huitwa Bodi ya Filamu.
Watu wanachanganya sana haya mambo, hawajui kwanini jina la Godfather hutangulia pale kabla hata msanii husika.
Nashukuru umeelezea vizuri sana.
Ova
 
Hii video wengi wetu tulikuwa tunaisubiri kwa hamu sana , hasa pale tulipopata habari ali-kiba na yeye kaenda kushoot video kwa hawa jamaa god-father wa south africa wanaotoa video kwa kiwango cha juu, ile imetoka tu jana nikaingia youtube kuicheki, DAH!!! kiukweli video imemalizika nikawa najiuliza mbona ujumbe wa audio na kinachooneshwa kwenye video haviendani!

Nlitegemea kuona mengi kama kumwona huyo mwana dsm alivyoharibikiwa na jiji, lakini hadi video inaisha ni ally kiba kavaa headphone kubwa anatembea na kucheza tu,

Nani alaumiwe hapa management, ally kiba au god father ni heri tu angeshot huku huku bongo kwa nisher
 


Kwahiyo unataka awepo wa kulaumiwa sababu+

Hujamuona mwana?
Kavaa headphone kubwa?
Kwenda kushoot video kwa god-fadher?
Kwa sababu hajashoot kwa nisher?
 
Mbona video kali tu, hamna w kulaumiwa au sababu inaimba Habari za mwana wa dar es salaam halafu ikaenda kishootiwa kw madiba??
 
Fasihi ni pana, muziki kama sehemu ya fasihi una maudhui mengi mf kuelimisha, kuburudisha, kuonya n.k. Wimbo wa mwana kwa maoni yangu Audio yake imekidhi vyote hiv, ila video yake haijakidhi dhima hzo zaid ya kuburudisha tu kwa hailingani kabisa na kilichoimbwa kwenye Audio...hivyo haijakidhi matarajio ya wengi,ila Ni quality video.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…