Mara 3 mfululizo Simba ilinusurika kushuka ligi kuu huku Yanga ikiinusuru mara mbili kwa kukubali kuwapa sare na kukosa ubingwa

Mara 3 mfululizo Simba ilinusurika kushuka ligi kuu huku Yanga ikiinusuru mara mbili kwa kukubali kuwapa sare na kukosa ubingwa

Hii ndio maana halisi ya kaka kuwa muungwana kwa mdogo wake hata kama mdogo wake hampendi, kuna muda ilibidi kaka afanye uungwana ajishushe kumkubalia mdogo wake amshinde ili kumuokoa na kuna muda bro ilibidi ajishushe uwezo ili mpinzani achukue ubingwa ilimradi mdogo apone, yote haya yaliwahi kutokea kwenye ligi kuu ya hapa Tz, fatilia mkasa.

Mara Tatu mfufululizo Simba ilinusurika kushuka daraja,na mara mbili Yanga iliinusuru katika michezo ya mwisho kabisa ya ligi hiyo.

1989 Yanga iliinusuru Simba kushuka daraja kwa kukubali suluhu kwenye mechI ya mwisho ya iliyokuwa Ligi daraja la kwanza ( Leo ikiitwa Ligi kuu) ingetokea Simba wangefungwa tu, wangeshuka daraja na kwenda kuanzia kwenye ligi ya Mkoa.

pia msimu wa 1988 Yanga ilikubali kukosa ubingwa ili tu Simba isishuke kwa kukukubali kichapo cha 2-1 ilhali ingetoa droo tu ingekuwa Bingwa wa mwaka huo.

Halikadhalika msimu wa mwaka 1987, mwaka ambao tukuyu Stars ikiwa moto wa kifuu kwa kupanda daraja na kuchukua ubingwa mwaka huo huo, walipokutana na Simba waliwavurumishia magoli bila huruma, Huku mechi ikiwa inaendelea iliwabidi viongozi wa Simba kuyajenga pembeni na Tukuyu stars kuwaomba wapunguze spidi ya magoli na wawaruhusu wayasawazishe ilimradi wapate sare ya kuwanusuru kushuka daraja ( haijajulikana ilitumika bahasha ya kaki ama kubembeleza ), Tukuyu Stars a.ka Bhanyambala ilitoa ushirikiano na kuwaruhusu Simba kutoa sare ya 5-5, kwa bahati nzuri wakati ule tuhuma za kupanga matokeo hazikupewa uzito tulionao leo.

MUHIMU: Yanga ikikosa Ubingwa basi sanasana itakuwa ya Pili, Simba mara kadhaa wameponea Chupu Chupu kushuka daraja.

Tukuyu Stars ilipanda daraja na kuchukua ubingwa 1986.
 
msimu wa 86 uliisha lini ?
Mwaka huo huo. Kipindi kile ligi ilikuwa inaanza kati ya Februari na Machi, na ilikuwa inaisha kati ya Julai na Agosti, ilikuwa unatumia mwaka wa Kalenda (Calendar year) sio mwaka wa Fedha (Financial year) kama ilivyo hivi sasa.
 
Back
Top Bottom