Mara: Abiria 16, Dereva na Kondakta wakamatwa kwa tuhuma za kumpiga Askari wa Usalama Barabarani

Mara: Abiria 16, Dereva na Kondakta wakamatwa kwa tuhuma za kumpiga Askari wa Usalama Barabarani

kichapo chake ni kikali sana
 
Attachments

  • a3f2cb96-1f44-4f71-b27d-72cce2fb3781.jpeg
    a3f2cb96-1f44-4f71-b27d-72cce2fb3781.jpeg
    442.3 KB · Views: 1
Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu 18, wakiwemo dereva, kondakta na abiria 16, kwa tuhuma za kumpiga askari wa usalama barabarani aliyekuwa akikagua gari walilokuwa wamepanda. Tukio hilo lilitokea Septemba 18, 2024, saa 12 jioni katika mkoa wa Mara.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Ofisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Trafiki Kuu, Butusyo Mwambelo, amesema kuwa askari huyo alikumbwa na kipigo wakati akijaribu kushusha abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari. Hata hivyo, kondakta wa gari hilo alifunga mlango na wote waliokuwa ndani ya gari, akiwemo dereva, kondakta, na abiria, walianza kumshambulia askari huyo.

ā€œAskari wetu alikuwa akitekeleza wajibu wake wa kuwataka abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari washuke. Lakini ghafla walimzonga kwa maneno ya kebehi, na kondakta kufunga mlango wa gari. Ndipo dereva, kondakta na abiria wao wakaanza kumpiga askari akiwa ndani ya gari. Je, kweli tumefika hatua hiyo kama Watanzania?ā€ alisema Mwambelo.
=============
Wananchi wanahasira sana hadi kufikia hatua ya kumtwaga askari mh tunapoelekea sasa ni balaa tupu!

Soma Pia: Abiria watakiwa kupaza sauti kwa Madereva wasiofuata Sheria za Usalama Barabarani

Waendelee kupigwa tu..safi
 
Style mpya ya maandamano, waandamanaji wanajazana kwenye dadala police ukijilengesha tu, wakufungulia mlango kisha wanafunga then wakikufungulia utachagua moja, kuendelea na hiyo kazi au kuacha, hahahahaha..... Hii mama itakua hajaipata kutoka kwa makachero wake.
🤣 🤣 🤣
 
Sasa kuna faida gani na wanaenda kufia jela na huyo jamaa atafungiwa leseni yake na lastly sahii watakuwa wametepeta vibaya sana, sasa kuna faida gani? hivi ni sifa mtu kuvunjwa kiuno halafu akabaki kilema maisha yote kwa kuwa tu amepata heshima ya kuingia kwenye clashes na serikali?.
Hakuna sifa wala heshima kwa kupigwa kisa umeingia clashes na serikali. Ila pia hakuna anayetafuta sifa wala heshima kwa kuingia clashes na serikali, hao raia nahakika hawakufika tu na kkusimamisha gari na kuanza kumuadhibu askari.

Tatizo la nchi hii, askari na baadhi ya wafanyakazi wa serikalini wanajiona wapo juu ya sheria, na kuwakosea adabu wengine kwa makusudi kabisa, na hapo ndipo raia wanachukua sheria mkononi kufanya kama kilichofanya na hao jamaa wa Mara.
 
"Lkn pia traffic wanatabia ya kujipiga na kujiumiza ili wapate huruma.
Btw, kipigo ni kipigo tu."

QUOTE OF THE DAY : "This is a time to bury our differences, and be one as a nation," - SAMIA SULUHU HASSAN #quote #quoteoftheday #tanzania #siasa #africa #politics #diplomacy #umoja
 
Maafande watakua wamekuza tu kesi uyu atakua alipigana na konda au dereva na abiria wakashangilia akaona awaonyeshe nguvu ya dola , huwezi kupigwa na watu 18 kwa pamoja ndani ya gari miundombinu na physics inakataa kabisa
Atakutana na Kibatala
 
Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu 18, wakiwemo dereva, kondakta na abiria 16, kwa tuhuma za kumpiga askari wa usalama barabarani aliyekuwa akikagua gari walilokuwa wamepanda. Tukio hilo lilitokea Septemba 18, 2024, saa 12 jioni katika mkoa wa Mara.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Ofisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Trafiki Kuu, Butusyo Mwambelo, amesema kuwa askari huyo alikumbwa na kipigo wakati akijaribu kushusha abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari. Hata hivyo, kondakta wa gari hilo alifunga mlango na wote waliokuwa ndani ya gari, akiwemo dereva, kondakta, na abiria, walianza kumshambulia askari huyo.

ā€œAskari wetu alikuwa akitekeleza wajibu wake wa kuwataka abiria waliokuwa wamesimama kwenye gari washuke. Lakini ghafla walimzonga kwa maneno ya kebehi, na kondakta kufunga mlango wa gari. Ndipo dereva, kondakta na abiria wao wakaanza kumpiga askari akiwa ndani ya gari. Je, kweli tumefika hatua hiyo kama Watanzania?ā€ alisema Mwambelo.
=============
Wananchi wanahasira sana hadi kufikia hatua ya kumtwaga askari mh tunapoelekea sasa ni balaa tupu!

Soma Pia: Abiria watakiwa kupaza sauti kwa Madereva wasiofuata Sheria za Usalama Barabarani

pamoja na kutekeleza majukumu,hekima na heshima kwenye ofisi ya wenzio ni lazima,sasa kwa sababu wewe ni askali basi uanze tu kuwashusha watu wewe unafikiri inakuwaje?mfano watu tayari walikuwa wamefika mbali tayari na kituo walichoanzia safari inakuwaje kwa mfano? hata mimi nisingeshuka
 
Kwamba ukikutwa unabaka ila unakaribia kumwaga uachwe sababu unakaribia kuridhika.

Hizi akili wengi ndani ya hilo gari mngelala mahabusu badala ya kuwahi mnakokwenda.

Nyie wabongo bana mshibe mpate nguvu za kutype kwenye mitandao ila wengi wenu ufikiri wenu huwa ni wa mashaka sana.hapo jamaa angesema achukue elfu 2 kuna fala tena angetoa ifinix yake aaanze kumrekodi,kaamua sheria ifatwe tena mnampiga mawe.
 
Back
Top Bottom