MARA: Akwea mlingoti wa bendera uchi kumuona mwanae hospital baada ya kuzuiliwa kumuona

online GOVT applications

Senior Member
Joined
Sep 7, 2026
Posts
185
Reaction score
182
#HABARI Mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 50 na 55 amesababisha taharuki katika Kituo cha Afya Nyasho, Manispaa ya Musoma mkoani Mara, baada ya kupanda juu ya mlingoti wa bendera ya Taifa kufuatia kuzuiwa kuingia ndani ya kituo hicho kumuona mwanawe aliyelazwa.

Mwanaume huyo, anayesadikiwa kuwa mkazi wa Bunda mkoani Mara na kufahamika kwa jina moja la Side, alifika katika kituo hicho akiwa na lengo la kumuona mtoto wake wa kumzaa, lakini alizuiwa na walinzi kwa maelezo kuwa muda rasmi wa kuwaona wagonjwa ulikuwa bado haujafika.

Inadaiwa kuwa baada ya kuzuiwa, mwanaume huyo alikasirika na kuchukua uamuzi wa kupanda juu ya mlingoti wa bendera uliopo katika eneo la kituo hicho, hatua iliyowashangaza wagonjwa, ndugu zao na wananchi waliokuwa eneo hilo.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa ni tukio la kwanza la aina hiyo kushuhudiwa katika kituo hicho. Wameeleza pia kuwa baadhi ya ndugu za wagonjwa wamekuwa wakilalamikia namna wanavyopata fursa ya kuwaona wagonjwa wao, huku wakidai kuwepo kwa upendeleo katika utekelezaji wa utaratibu wa kuwaona wagonjwa.

Wamesema kuwa endapo malalamiko kama hayo yataendelea kupuuzwa, huenda yakasababisha matukio yenye madhara zaidi kwa wahusika na kituo hicho. Taarifa zaidi kuhusu tukio hili, ikiwemo hatua zilizochukuliwa na uongozi wa Kituo cha Afya Nyasho, usikose kutufuatilia kupitia mitandao yetu ya kijamii.
 
Attachments

  • 1788954544960.jpg
    1788954544960.jpg
    72.9 KB · Views: 13
Miaka 50 kupanda iyo pole sio poa. Yuko fit.
 
Nyie wakurya ni wapumbavu kweli, mna ubishi wa kishamba. Kuona wagonjwa kuna ratiba yake, hayo majitu ta Mara ni washamba sana
 
Back
Top Bottom