Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,Sagini Jumanne ameliagiza jeshi la polisi na msajili wa madhahebu kuchunguza kundi linalodaiwa kutumia dini kutapeli wananchi kijiji cha Mwanza Buriga wilayani Butiama na itakapobainika ni moja ya makanisa yaliyosajiliwa nchini usajili wake utafutwa
Wananchi kijiji cha Mwanza Buriga wilayani Butiama, wamemuomba Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni mbunge wa Butiama Jumanne Sagini kuwasaka na kulikamata kundi la watu linalodaiwa kutumia kivuli cha dini kutapeli wananchi katika kijiji hicho na kutokomea kusikojulikana
"Kuna kundi lilikuja hapa kijijini Mwanza Buriga wilayani Butiama na limekuwa likichukua sh. 2,000 kwa kila mwananchi kama usajili wa kujiunga na kanisa na kuahidi kuwapatia kilo 90 za mchele, mafuta na sabuni. Wanapochukua fedha hutokomea kusikojulikana"Khamis Kombe, mwanakijiji