Mara: Wananchi walizwa elfu ishirini ishirini kwa kivuli cha dini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,Sagini Jumanne ameliagiza jeshi la polisi na msajili wa madhahebu kuchunguza kundi linalodaiwa kutumia dini kutapeli wananchi kijiji cha Mwanza Buriga wilayani Butiama na itakapobainika ni moja ya makanisa yaliyosajiliwa nchini usajili wake utafutwa

Wananchi kijiji cha Mwanza Buriga wilayani Butiama, wamemuomba Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni mbunge wa Butiama Jumanne Sagini kuwasaka na kulikamata kundi la watu linalodaiwa kutumia kivuli cha dini kutapeli wananchi katika kijiji hicho na kutokomea kusikojulikana

"Kuna kundi lilikuja hapa kijijini Mwanza Buriga wilayani Butiama na limekuwa likichukua sh. 2,000 kwa kila mwananchi kama usajili wa kujiunga na kanisa na kuahidi kuwapatia kilo 90 za mchele, mafuta na sabuni. Wanapochukua fedha hutokomea kusikojulikana"Khamis Kombe, mwanakijiji


 
sasa ndugu zangu wana mara hivi kweli utoe 2000 upate kilo tisini za mchele na sabuni kweli inakuja hiyo huwezi jiuliza kabla ya kutoa,kingine kwa bwana hakuna kuwahi wala kuchelewa hivyo subirini mtaletewa mlichoahidiwa kwa muda ambao bwana ataona mnastahili
 
Unapewa vipi kwa kuomba / kuombewa au physically ?

Haya mambo ya imani haya shida tupu.., ukienda deep sana utapeli ni mwingi sana (ila ni imani za watu who am I to say otherwise)
 
Kila kitu upewa kulingana na nia yako...

Walitoa kwa Nia ya kupata zaidi basi wazidishe Imani huenda masihi atarudi navyo hyo sku kutoka kwa bwana...

IMANI BILA AKILI NI LAZIMA ITAKUDHURU (NI UJINGA)
 
Labda awakuelewa,watapewa ila mpaka siku watakayofika mbinguni mura.
 
Hao kondoo nao si walijipeleka wenyewe!!!

Hii haina tofauti na betting
 
Hahahah wabongo mkuu ni hatari na hili ongezeko la bei kwa mama inabidi tu watanzania wawe wabunifu hahaha kilo 90 za ubwabwa na haragwe zake.
 
Dah Mara imekuaje tena , huko si ndio kanda maalum hawataki utani...wanatapeliwa kizembe hivyo
 

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwa elfu 2 upate kilo 90 za mchele seriously? Hebu kuleni ugali nyie wazanaki acheni utani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…