Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Salaam Wakuu, natumai kaubaridi mwororo kawapapasa vyema huko mliko, twende kwenye mada.
Sehemu yoyote mjini inachukuliwa kama sehemu ya kutolea ushamba, kutokana na kupiga hatua kwenye mambo mengi na muingiliano mkubwa na watu kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni. Naona ndio hata mababu zetu wakaja na ule msemo mjini shule, shamba kilimo!
Mara ya kwanza kuja mjini jiji lilikupokeaje? Nini lifanyika ambacho ukifikiria leo unacheka sana nakusema kweli nilikuwa mshamba wakati wakati ule?!
Mimi mzaramo wa hapa hapa, kipindi kile walikuwa wanaita jiji la Makamba, ila kuna tukio lilitokea jamaa yetu mmoja, kipindi kile nilikuwa mdogo sana kuelewa kwanini baba na wengine walikuwa wanacheka wakati nasikia mtu kaibiwa, ila ndio jinsi jiji lilivyompokea na kumtoa ushamba!
Jamaa alikuwa katoka kijijini akiwa na mbuzi wa kutosha kuja kuuza Dar kwenye mnada, akafika salama na kuuza mbuzi wake vizuri akiwa na kitita chake cha milioni kadhaa. Sasa akawa anakuja home asalimie na kuangalia utaratibu wa kugeuza kurudi nyumbani kwake kesho yake au kesho kutwa yake.
Jamaa akakutana na vijana wa mjini, wawili, wana kichupa chenye vipande vya vitu vinanyong'aa wakimwambia ni dhahabu. Wakasema wanatafuta mteja ili warudi zao machimboni kuendelea na shughuli zao, wakampiga bei ya juu kidogo zaidi ya pesa zile alizonazo, jamaa amesikia sikia kuhusu madini na akawa na uhakika kile kichupa kitampa zaidi ya mara 10 ya pesa aliyopata kwenye kuuza mbuzi, akaingia tamaa.
Akawaambia jamaa mimi nina kiasi hiki hiki tu hakitoshi kununua chote, wakamwambia hamna shida tupe hiyo itafaa, tumezunguka mda mrefu kutafuta mteja, hata hii si mbaya ili turudi zetu machimboni. Jamaa akaona ameula, akachukua pesa zote akawapa.
Basi jamaa akaja nyumbani na bashasha kweli kweli kuwa amenunua almasi na sasa yeye ni tajiri, na amenunua kwa pesa ndogo tu, akaanza mpaka kupiga mahesabu ya jinsi atakavyonunua vitu kujenga nyumba na nk.
Sasa wakati stori zinaendelea mimi nikawa nimeshika hiko kichupa nakibiruarua na kuangalia dhahabu inayosemwa ikoje, mara pah, nikaangusha kichupa kikapasuka, kila kitu kikatawanyika, sio ndio "Almasi" yote ikamwagika, kuangalia ilikuwa vipande vya chupa (transparent) vimejazwa humo!
Jamani mzee alikufa mbavu mpaka machozi🤣🤣🤣, akaambiwa bwana mdogo karibu mjini, umepigwa hapa hakuna kitu, mama na wengine wakaungana kwenye vicheko, pole zikaja baadae sana. Aisee jamaa alinywea, na ndoto zote zikazima, aliyumba na kupata stress kiasi, kila akiniona anakumbuka tu nilivyovunja kichupa chake!
Wewe kwako ilitokea tukio gani ukikumbuka unasema kweli hapa nilikaribishwa mjini, kwakweli nilikuwa mshamba?