Mara ya kwanza kupata kazi ($410) kwenye site ya Freelancer.com

Mara ya kwanza kupata kazi ($410) kwenye site ya Freelancer.com

GLOBAL CITIZEN

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2014
Posts
767
Reaction score
1,657
Blessed Saturday everybody!

Leo kama kawaida nipo hapa kukupatia darasa litakalokusaidia kuongeza maarifa ili upate pesa ukifanya kazi kama Online freelancer.

Hapo nimetumia neno maarifa kwasababu bila kufanya haya mambo kama professional itakuwa ngumu sana kupata hizi kazi. Binafsi nafanya kazi nyingi kama Online Freelancer toka mwaka 2016.

Kwa wanaofuatilia makala nazoandika hapa JF wanafahamu nilimeanidika sana kuhusu freelancing site ya UpWork. Nimeonyesha kazi ninazofanya (recently I’m working on $1,000 gig) lakini pia ninasaidia yeyote yule anayetaka kuanza vizuri carrier yako mpya kama Online freelancer.

Jana my brother kutoka hapa JF nilimsaidia kwa mara ya kwanza kufungua Account itakayokuwa approved UpWork baada ya yeye kusumbuka kwa muda mrefu akituma maombi na kukataliwa.

Unajua ukifanya kitu chochote kile inabidi ufanye kwa ukamilifu wake. Ni nadra sana UpWork wakiona profile yako imeandaliwa vizuri watakataa application yako. Mimi nimeona profile za watu. Wengi wao hawajui hata wanaenda kufanya nini wanapojisajili kwenye. It is crazy.

Ok. Si lengo langu kuongelea UpWork.

Leo nipo hapa nataka nikonyeshe jinsi unavyoweza kupata kazi katika site ya freelancer..com

Kwa kuanza niweke message niliyopokea tar 13 novermber 2019 toka kwa client akitaka Nipigie kazi ya Kiswahili. Hii kazi ni $410.

IMG_7068.JPG


Ok.

Jana nikapewa maelezo ya mwisho.

IMG_7069.JPG


Hii ni mara yangu ya kwanza kupata gig inayozidi $200 freelancer.com

Kwahiyo Hii maana yake freelancer.com nao wapo vuzuri na inawezekana kutengeneza pesa kutumia hili jukwaa ukiwa unafahamu nini unafanya.

Iwapo bado huelewi sana na haufahamu utaweza vipi kuwa freelancer usisite kuniandikia kwenye Email yangu ya kazi makingmoneyonlinetz@gmail.com nitakupatia Course + mentorship.

Na niseme tu sasa hivi ninaendelea kufundisha baadhi ya watu walio committed na kila kitu kinaenda vizuri.

Lengo langu ni kuunda network na vijana wengine hapa TZ na kwakufanya hivi tunaweza kutasaidiana sana iwe kwa kupeana opportunity au kufundishana Skills mpya zitazasaidia watu kupata pesa.

Trust me unavyosaidia watu wengi zaidi ndivyo pesa inavyokuja. Na jambo zuri ni kwamba kila mmoja anaweza kumsaidia mwingine. Iwe wewe ni mjuzi sana au ndiyo unaanza. Kuna kitu ninachoweza kujifunza kwako hata kama unadhani hakuna. Ndiyo ipo hivi.

Kwa kizungu tunasema Each one teach One.

Ok sasa tuangalie Mambo matatu unavyoweza kufanya ili upate kazi yako ya kwanza katika site ya freelancer

1 • Jifunze kuwa authentic/original unapo andika cover later wakati unaapply hizi kazi.

Unajua nini.

Watu wengi hawajui kuandika.

Client akisoma tu cover later anajua huyu hajielewi.

Kama nilivyosema mara nyingi hapa. You don’t need to tell client about your university degree. No one cares about that.

Kwanza kuwa na university degree si skill.

Skill ni uwezo wakupiga kazi iwe uliishia lasaba B Arumeru Primary School au Stanford University USA [emoji631]

It doesn’t matter.

Sasa hapa ili kufahamu candidate gani anaweza kupiga kazi mara nyingi client anaangalia jinsi ulivyo original katika maandishi yako.

Watu wengi wanaokurupuka ukisoma wanachoandika mara nyingi utagundua tu hawana uwezo na wanachokisema. Kwasababu hawaandiki kama experienced.

Maneno wanayoandika hayana uzito. Hayana uhalisia.

Na hii ndiyo sababu hujibiwi na hupati kazi.

2 • Apply kazi zile tu unazoona upo na nafasi kubwa kupata.

Yes man.

Usiwe na pupa.

Good things come to those who wait.

Yani kama simba vile. Unatakiwa uwinde windo unalodhani ni rahisi kukamata.

Nafahamu baadhi ya freelancers wakishajisajili wanakimbilia ku-apply kazi yoyote iliyo mbele yao wakidhani Ndiyo kupiga kazi kwenye huko.

Nop. That is wrong.

Lazima uwe Strategic. Apply kazi zile tu unazoweza kuzifanya kwasababu kitu unachoweza kweli kukifanya hata katika maneno yako utatambulika tu.

Kama huna skill yoyote nakushauri Jifunze skill mpya. Na hapa niseme tu unaweza kujifunza skill mpya kwa muda mfupi tu kwasababu kazi zinazopatikana katika haya majukwaa ya Online freelancing hayahitaji uende chuo ukajifunze. Ni wewe tu na ujanja wako. Niandikie email ninaweza kupendekeza ni nini hasa unaweza kujifunza kwa muda mfupi.

3 • Kuwa Mvumilivu na usikate tamaa.

Wakati nilipoweka uzi wangu hapa kuhusu kazi nazoendelea kuzifanya UpWork baadhi ya watu waliuliza kuhusu site ya freelancer..com Nikasema ni kiasi cha muda tu. Nitapata kazi freelancer..com na nitakuja hapa kuweka ushahidi.

Unajua nini mtu wangu?

Inabidi uwe mvumilivu kwenye kila jambo unalofanya kwasababu ni mara chache mambo yataenda kama unavyotaka. Sasa hapa usipokuwa mvumilivu mambo mengi yatakuwa yanakupita kwasababu wewe ni kigeugeu.

Inabidi kila jambo unalofanya ulipe muda.

Ndiyo ipo hivyo. Huwezi kubadilisha hili.

Never give up.

Hii ni siri watu wengi wanapuuza kwasababu hawaelewi.

Sasa hivi umeshafahamu. Usikubali kukata tamaa na kuanza kulalamika ukilaumu.

Alright. Kwa leo namba niishie hapa. Hopefully umenufaika na uzi huu.

Tukutane tena siku nyingine katika darasa lingine amazing kama hili. Pia iwapo unataka niandike kuhusu njia fulani yakutengeneza pesa Online niajulishe kwenye comment.

Cheers 🥂
 
Kiongozi naomba msaada wako tafadhali mimi baada ya kusikia hizo Online earning money freelance nikatia miguu na Nika pakua zangu truelance chap na kwa vile ni mtu naye penda sana graphics logo na editing nikaona labda nami piah ntaweza make hizo money ila kila job ya aina hiyo hiki tokea na nik2ma purposal cpati kazi hivi labda na kwama wapi.
 
kiongozi naomba msaada wako tafadhari Mm baada ya kusikia hizo Online earning money freelance nika Tia miguu na Nika pakua zangu truelance chap na kwa vile ni mtu naye penda sana graphics logo na editing Nikaona labda na mim naeza make hizo money ila kila job ya aina hiyo Hiki tokea nikituma purposal wapi cpati kazi Hivi labda na kwama wapi

Ndiyo hupati kazi kwasababu inaonyesha unakurupuka.

Ingekuwa rahisi hivi basi kila mtu angekuwa anapiga pesa tu.

Inabidi uwe strategic.

Na hili lenyewe ni darasa kamili.

Pia inabidi upate right mindset.

Nimetoa Email hapo unaweza niandikia
 
Kuna vitu vingi sana umevieleza kwenye post yako vinavutia sana.

Ila nahisi wanaoelewa ni wale ambao labda wanaufahamu na hiyo online freelance au labda wameshawahi kusoma mada zinazohusiana na hicho kitu.

Binafsi nimevutiwa na hii kitu ila niwe muwazi tu natamani sana ningeleewa kwanza aina ya kazi zinazopatina huko, skills ambazo mtu anatakiwa kuwa nazo,nk

Kama kuna uzi kama huo humu itakuwa vizuri ukitupa link sisi wapya kwa hii Taaluma tukasome halafu baada ya kuelewa ndo tumiminike huko kwenye email sasa ili tusije na upya wetu tukaleta maswali mengi huko
 
Daa hii freelancer inanifanya nife njaa hapa mjini. Hii ni baada ya kutaka kutoa hela sasa kwenye kufanya verification number ikawa inazingua. Nikawacontact customer support baada ya muda wakadiable wakadisable account yangu. Wakanitumia email kuwa nimevilolet TOS na hela yangu watanicontact baada ya siku 90 ili niitoe. GLOBAL CITIZEN,
 
Daa hii freelancer inanifanya nife njaa hapa mjini. Hii ni baada ya kutaka kutoa hela sasa kwenye kufanya verification number ikawa inazingua. Nikawacontact customer support baada ya muda wakadiable wakadisable account yangu. Wakanitumia email kuwa nimevilolet TOS na hela yangu watanicontact baada ya siku 90 ili niitoe.

Weka hapa screenshot kama unazo.

Na je ulikuwa unatumia Platform gani?

Ndiyo lazima kila kitu kiwe verified hasahasa identity yako.

Kumbuka site kama Freelancer.com au UpWork lazima wathibitishe ni wewe kweli unayemiliki Account ya bank husika.

Mbona ni rahisi tu kama ukitimiza taratibu zote?
 
GLOBAL CITIZEN, Nilikua natumia fiverr. Kwenye identity nimeupload hadi kitambulisho cha taifa na selfie kama walivyoniagiza. Lakini mwisho wa siku wakadisable
 
GLOBAL CITIZEN,
Wewe unataka kula hela za hawa vijana masikini bure bure tu? Uwe na huruma aisee, wapatie hayo maarifa hapa hapa kama kweli una nia njema. Waonee huruma wenzio, tayari CCM imeshawachapa viboko vya kutosha, na wewe tena?
 
Wewe unataka kula hela za hawa vijana masikini bure bure tu? Uwe na huruma aisee, wapatie hayo maarifa hapa hapa kama kweli una nia njema. Waonee huruma wenzio, tayari CCM imeshawachapa viboko vya kutosha, na wewe tena?

Wewe acha kukurupuka.

Unadhani mimi ni mgeni hapa?

Go and hung yourself in shame!

Stupid
 
Nilikua natumia fiverr. Kwenye identity nimeupload hadi kitambulisho cha taifa na selfie kama walivyoniagiza. Lakini mwisho wa siku wakadisable

Kwahiyo baada ya hapa ukaamua kususa?

Mkuu hiyo haisaidii.

Lazima utakuwa ulifanya makosa au kuna kitu hukukamilisha.

Fiverr ni jukwaa kubwa na salama hawawezi kukataa kukupatia pesa ambayo ni halali yako.

Fiverr inaaminiwa na millions kwahiyo hilo si tatizo la fiverr. Inabidi ufanya mambo yako kwa uhakika zaidi.
 
Ndo hivyo tuu mkuu hamna nilichokosea sababu first time naregister account namba ilikua verified sasa nimepiga kazi nyingi tuu kwenye kutoa hela ndo mshike mshike ukaanzia hapo. Ila ngoja nisubirie hizo siku 90 zikiisha nione kama nitaweza kuwithdraw hizo hela. Na kingine kimewauliza kama naweza kufungua account nyingine wakasema haiwezekani. Wanazingua kishenzi yani.
Kwahiyo baada ya hapa ukaamua kususa?

Mkuu hiyo haisaidii.

Lazima utakuwa ulifanya makosa au kuna kitu hukukamilisha.

Fiverr ni jukwaa kubwa na salama hawawezi kukataa kukupatia pesa ambayo ni halali yako.

Fiverr inaaminiwa na millions kwahiyo hilo si tatizo la fiverr. Inabidi ufanya mambo yako kwa uhakika zaidi.
 
Back
Top Bottom