mzee wa kasumba
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 1,440
- 2,952
Kwakuwa watu wengi humu hatujuani imekuwa ni kawaida sana kila mtu kujitutumua na kujimwambafai sana katika hili jukwaa. Utasikia ooo nimempiga mtu mawashi, sijui nimemfanya mtu hivi na hivi ilhali siyo kweli (kwasababu tu hatukujui)
Twende kwenye point. Nini sababu ya kuandika uzi huu?
Ebwana leo katika pitapita zangu za kuzuga mjini hapa na pale (leo sikwenda kazini), nilipofika maeneo flani hivi nikamkuta demu mkaaali kasimama akiwa peke yake. Kutokana na kimbelembele changu bwana nikaona hebu ngoja nimsogelee nijaribu kumuimbisha maneno mawili matatu. Kwa bahati nzuri demu alionesha ushirikiano mzuri tu, huku na huku akatoa namba ya simu.
Ebwana kumbe yule mwanamke anamsubiri bwana (mchepuko) wake ambaye alikuwa ametoka kidogo. Kwa bahati mbaya zaidi, yule bwana alitokea kwa nyuma yangu mimi sikumuona. Nakuja kushitukia jamaa amenizaba bonge la kibao cha kichwa. Khaa! ile kutuliza wenge jamaa akawa ananambia kuwa "we unadhani kila mwanamke ni malaya tu fala we, Qumer makoh"
Sijakaa sawa jama kanibamiza ngumi ya kifua, sijakaa vema akarusha tena konde (gang) la uso ila nikaliona. Duuh! nikasema leo naumbuka aisee. Nikaona siyo kesi hebu ngoja tuzikinge kidogo (twende ringi) huku na huku nikam taimu nikamzawadia teke la mbupu moja maridhawa sana likamfanya mpaka akafika chini kwa uchungu.
Baada ya kuona jamaa yupo chini ikabidi tu nisepe wakati huo demu anapiga simu kwa watu wake wa karibu na watu walikuwa wameshaanza kujaa eneo la tukio.
KUSEMA KWELI:
Jamaa alinipiga (yaani nilipigwa vizuri tu) lile teke kama nilifanya kubahatisha baada ya kuona jamaa anataka kunidhuru sana. Sina sababu ya kusema najua kupigana wakati nafsi yangu inanisuta.
Ndugu yenu nimechezea kipondo kitakatifu, nashukuru tu sijavimba wala sijatoka damu.
NILICHOJIFUNZA LEO:
1. Kuna haja ya kuwa mazoezi ya self-defence japo kidogo, kama ningekuwa boya kabisa jamaa angeniuwa.
2. Jamaa uliyenipiga. Mwanangu nisikufiche, demu wako nitahakikisha ninamla.
Na nyie wanawake kama una bwana wako ukisimamishwa na mwanaume mwingine si uwe muwazi tu. Matatizo ya nini?
Sisi wengine ni wababe kitandani tu jamani, ngumi hatujui tutakuja kuuana bure.
mzee wa kasumba
Tiririka...