Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Kutokana na changamoto wakati mwingine unajikuta upo kazini mambo hayajakaa sawa hata pesa ya Lunch hamna.
Mara ya kwanza ilipotokea nilichukulia tu kuwa ni coincidence haikuwa na lolote jipya.
Ofisini kwangu nafanya kazi na raia wa nchi mbali mbali hasa za asia na kiarabu. Siku hiyo nimeenda kazini nina pesa ya nauli tu. Hata sikuweza kwenda na gari sometme mambo yanakuwa tight sana ndugu zangu. Basi mchana akaja dada mmoja mwenye asil ya kihindi akaniletea chakula toka kwao. Nikamshukuru sana. Nikala na kingine nikaenda nacho home.
Siku zikapita kuna siku tena ikatokea nipo majalala mchana hauelewek na njaa inauma sana.mida ya saa tano na nusu akaja dada mwingine akaleta msosi akaniwekea mezani pangu akaondoka. Nikamshukuru Mungu pia maana ulikuwa muujiza.
Siku nyingine ikatokea tena hivyo hivyo hali mbaya kiuchumi sina pesa ya kula. Akaja mama mmoja ambaye yeye anatokea nchi za kiarabu.ilikuwa siku moja baada ya Eid akanikabidhi mfuko mkubwa. Kuwa hiyo ni zawadi yangu ya sikukuu....maskini mpaka machoz yalikaribia kunitoka maana kiukweli sikuwa na pesa na nlikuwa na njaa mchana umekaribia sisi wengine tunakula mara tano kwa siku ukikosa chakula mchana unachanganyikiwa. Nikapiga msosi birian,nyama na makando kando mengine. Mwingine nikagawa kwa jamaa zangu na kidogo nikabeba.
Leo ndo imebidi niwashirikishe wenzangu kuwa miujiza ipo na Mungu anaweza walisha watu wake. Sina hili wala lile najua mchana ukifika sina pesa mfukoni sababu nliyokuwa nayo kuna mtu nlimpa kwa dharura. Mara nakuta mezani pangu ofisin pana mfuko. Nikaweka pembeni maana sikujua ni wa nani.nikaendelea kutumia computer yangu. Mara akaingia dada mmoja akanambia ule mfuko una lunch yangu maalum.nikachukua nikamshukuru Mungu.
Nashukuru kwa mambo haya ambayo kwa mtizamo wa kibinadamu ni kama madogo sana. Lakin ukitizama kwa undani unagundua ni mambo makubwa na si kwamba ni coincidence.