Kuna watu walikuwa safarini wakaharibikiwa na gari usiku maeneo flani hapa jirani. Kwa sababu ni kamji kadogo hawakuweza kupata huduma ya service kwa muda ule, wakaamua walale garini. Basi wakawa wanatafuta sehemu watakayoweza kupata chakula, sehemu nyingi zikawa zimeshafungwa na vibanda vya chips navyo vikawa vimefungwa, basi ikawa kila wanakopita hamna chakula, baba mmoja akawaambia kama hawatojali basi awape chakula cha home kwake, wale jamaa wakakubali (japo ilishangaza), yule baba akamuita mkewe akamuuliza kama kuna chakula kilichobakia coz kuna wageni, walikuwa wanaume watano, mke akasema kipo lakini kwa idadi yao hakitoshi, yule baba akamwambia mkewe akipeleke hicho hicho watulize njaa pakuche... Naskia wale watu walikula wakashiba na wakasaza... Naskia walishangaa kweli, kila wakila wanaona chakula kipo pale pale hakisogei..
Mwenyewe ilikuwa ngumu kweli kuelewa hilo tukio..