round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Rafiki wa mtaani, shuleni, chuo, n.k. mlikuwa washikaji sanaaaa kujuliana hali kila siku, muda mwingi mpo wote, kushare siri, n.k. lakini leo mmebaki kuchunguliana view stutus,
Halafu hata mkikutana ni salam za dakika 2 tu, baada ya hapo kila mtu anajidai yupo bize, mnabadilishana za kuchunguliana status,
Nje ya marafiki tunaoishia kuangaliana status nina visa hivi
Kuna siku flani nilikuwa napoteza muda naendesha gari mtaani nilikuwa nimerudi kusalimia mkoani nilikokulia, nikamuona rafiki yangu tuliwahi kuwa mabesti sana primary, vile nilivyomona na yeye aliniona ila akazuga kama hajaniona (niligungua badae) , nikaona niende kupaki gari sehemu ya mbele kidofo maana mazingira hayakuruhusu, nilivyopaki nimeshuka namuona mtu kaongeza mwendo wa kutembea kaingia njia nyingine, nikawasha gari fasta niende mtaa wa barabara atayotokea, mara hii macho yaligongana hakuweza kunizuia, tulisalimiana kidogo ila akaniambia ana haraka, namba aliyonipa haipatikani, sijui sababu lakini labda pengine ni gepu la maendeleo niliambiwa hali yake si nzuri
Niliwahi kuwa na rafiki alikuwa anapenda kunitembelea sana kupiga story, yeye alishatoboa tangu akiwa 22 tayari alikuwa na gari yake, sijui hata kilichotokea mara paap mawasiliano yakapungua, off course mpaka leo tukiwa kwenye 30s bado tunachekiana ila ni zile kupeana heri ya mwaka mpya, story imeisha,
Niliwahi kuwa na rafiki tuliekuwa mbali kwa mwaka moja tu, lakini tunatazamiana status na kupeana hi mara kadhaa japo mara chache, alikuwa ameenda mafunzo idara ya ulinzi akabahatika kupata kazi, aliposti video anavishwa cheo kwenye bega, nilimpa hongera ila hakujibu (Blue tick), mara ya pili niliwahi kumpa heri ya mwaka mpya ila hakujibu, damn ! baada ya mwaka na mimi nilibahatika kwenye shughuli zangu, mimi napenda sana magari nilinunua nikajipost status nikiwa safarini ndipo aliponijulia hali "za siku kaka naona mambo yamejipa" nilibaki na maswali mengi
Nimefikia muafaka kukubaliana na ukweli mchungu, hakuna marafiki wa kudumu, marafiki huja na kuondoka kutokana na mazingira mapya, tabia mpya, nyakati za maisha, n.k. hawa wengine tunaishia kuchunguliana status tu.
Too bad kuna wengine wanapoteza marafiki wote maana kujenga urafiki mpya ni kitu kizito kwa wengine