rafiki wa mtaani, shuleni, chuo, n.k. mlikuwa washikaji sanaaaa kujuliana hali kila siku, muda mwingi mpo wote, kushare siri, n.k. lakini leo mmebaki kuchunguliana view stutus,
Halafu hata mkikutana ni salam za dakika 2 tu, baada ya hapo kila mtu anajidai yupo bize, mnabadilishana za kuchunguliana status,
Nje ya marafiki tunaoishia kuangaliana status nina visa hivi
Kuna siku flani nilikuwa napoteza muda naendesha gari mtaani nilikuwa nimerudi kusalimia mkoani nilikokulia, nikamuona rafiki yangu tuliwahi kuwa mabesti sana primary, vile nilivyomona na yeye aliniona ila akazuga kama hajaniona (niligungua badae) , nikaona niende kupaki gari sehemu ya mbele kidofo maana mazingira hayakuruhusu, nilivyopaki nimeshuka namuona mtu kaongeza mwendo wa kutembea kaingia njia nyingine, nikawasha gari fasta niende mtaa wa barabara atayotokea, mara hii macho yaligongana hakuweza kunizuia, tulisalimiana kidogo ila akaniambia ana haraka, namba aliyonipa haipatikani, sijui sababu lakini labda pengine ni gepu la maendeleo niliambiwa hali yake si nzuri
Niliwahi kuwa na rafiki tuliekuwa mbali kwa mwaka moja tu, lakini tunatazamiana status na kupeana hi mara kadhaa japo mara chache, alikuwa ameenda mafunzo idara ya ulinzi akabahatika kupata kazi, aliposti video anavishwa cheo kwenye bega, nilimpa hongera ila hakujibu (Blue tick), mara ya pili niliwahi kumpa heri ya mwaka mpya ila hakujibu, damn ! baada ya mwaka na mimi nilibahatika kwenye shughuli zangu, napenda sana magari nilinunua nikajipost status nikiwa safarini ndipo aliponijulia hali "za siku kaka naona mambo yamejipa" nilibaki na maswali mengi